Author name: SW - Melkisedeck Shine

Hofu inavyo tugharimu katika safari ya ujasiriamali na Jinsi ya kuiepuka

Wengi wetu tunapenda Mafanikio, tunapenda kufika mbali tunapeda kuwa kama Mengi siku moja.

Tunavyo kuwa tunaendelea kutamani kiwa kama wakina Azam au Mengi nyuma ya pazia tuna matatizo nayo ni hofu kuu,

1. Hofu ya kuchekwa
Wengine tuna hofu ya kuchekwa kwamba tunafanya biashara gani hizi? Tuna lima kilimo gani hiki au tunafuga nini? Kuna watu hofu ya kuchekwa tu inatosha kumtoa Barabarani mazima.
Mtua leo hii anashindwa Kuanzisha project anayo peda kwa sababu tu anaogopa kuchekwa

2. Hofu ya kushindwa kabla ya kuanza
Tuna hofu za kushindwa, naona nikifuga kuku nitashindwa, naona nikilima nitashindwa tu, hofu hii inatufanya tuone bora kusubilia kwanza
Fear of Unknown inatusumbua.
Watu tunashindwa kuanzisha miradi kisa tu mtu anaogopa kushindwa.

3.Hofu baada ya kuona walioa anza wakashindwa
Hii ni kubwa sana, mtu anakuambia fulani alifuga Broiler wakafa wote, fulani alifuga layers wakamshinda, Fulani alilima nyanya kavuna debe moja tu, fulani.
Watu wengi tunashindwa kuanza kwa sababu fulani alishindwa. Sikiliza fulani sio wewe, fulani ana akili yake na wewe una akili na nguvu zako.

4. Hofu ya Elimu zetu.
Kuna walio bahatika kusoma hadi Univesity na wana Degree na Wengine Masters. Sasa elimu zetu nazo zimekuwa.kikwazo, mtu anaona kwa elimi yake hapaswi kufanya aina fulani ya biashara, hapaswi kufuga au kulima anapaswa kufungua Yard ya kuuza Magari
Elimu zetu ni.kama tulienda kusomea uoga vile.

5. Hofu ya Ndugu,jamaa, Marafiki na kadhika.
Kuna mtu mpaka sasa hawezi fuga au anzisha mradi kwa sababu tu ndugu jamaa na marafiki hawatamuelewa. Mama hatanielewa kwamba nalima na nimesoma, Mama mkwe na Baba mkwe watanishangaa sana kwamba nafuga Bata,
Mchumba hatanielewa kabisa na anaweza nikimbia mazima kwa sababu nalima Nyanya na nina Degree,

6. Hofu ya kukosa baadhi ya vitu.
Mtu anaona kuliko akose kwenda kutazama mpira na washikaji bora huo mradi usianze tu, kuliko nishindwe kwenda viwanja bora nisianze ,siwezi enda kulala shambani nikashindwa kwenda kuona npira au kucheki move.

Kwa Kifupi tuna hofu nyingi sana zinazo tugharimu.

SASA BASI

Kama unaishi kwenye hofu za aina hizo kamwe sahai kufanikiwa labda tu ukomae na ajira,

Nilazima utambue kwamba uko wewe na honor uwezo wako, ipe heshima Uwezo wako.
Ukiona hofu hizo ni kikwazo kwako na huwezi ziacha kama una mtaji basi kanunue vipande ya hata UTT na usubilia gawio, au nunua hisa za kampuni na subiliaga gawio kulingana na faida.

Kwenye ulimwengu wa Ujasiriamali lazima kwanza Uonekane mwehu, lazima second person akuone kichaa, lazima watu wakushangae ,
Ujue hata kichaa yeye huwa hajui kama ni kichaa ila second person na third ndo tunaona na tunajua kwamba fulani ni kichaa, the same na wewe kwamba lazima ifikie mahali watu washindwe kukuelewa kati ya haya yaani wajiulize maswal mengi bila majibu.
– Fulani hivi kafukuzwa kazi?
– Fulani hivi kweli alimaliza chuo? Au alidisco?
– Fulani anaongea mwenyewe barabarani
-Fulani maisha ni kama yamemkamata, hapa kisa tu huonekani viwanja.
-Fulani haonekani viwanja kabisa.
– Fulani anacheza na ujasiriamali hiyo awaachie wakina Mangi

Watu wakianza story za aina hizi basi jua uko kwenye track nzuri.

UJASIRIAMALI SIO ISHU YA KITOTO, LAIZMA UWE KAMA UKO ULIMWENGU MWINGINE KABISA

Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

1. Hauko Tayari kuthubutu na kujiunga
2. Kutokujiamini
3. Kutopata sehemu sahihi ya kupata ushauri
4. Kutokuwa na sababu za msingi au malengo ya msingi ya kupigania ndoto zetu
5. Kukaa katika shauli la wasio haki na barazani pa wenye mizaha

Hizo ni baadhi ya sababu zinazopelekea watu wengi kushindwa kuishi maisha ya ndoto zao na kuishi maisha ya kawaida tofauti na fikra zao.

Kuthubutu ni jambo la muhimu sanaaa katika maisha ya mwanadamu kwa maendeleo ya kwake ,familia ,jamii pamoja na taifa kwa ujumla hivyo ndugu zangu nawasihi tuweze kua watu wanaothubutu.

Tuondoe uwoga katika maisha yetu Kwamaana Uwoga Ndio CHANZO CHA UMASKINI WETU tukiendeleea kuogopa mazingira yanayotuzunguka na jinsi gani watu watatuchukulia na kutusema atutaweza kupiga hatua.

Changamoto ni hali ya kawaida katika maisha ya mwanadamu , kuogopa changamoto nalo ni Kosa kubwa katika maisha yetu.

…………..Mwisho kabisa nipende kusema……………

USIJILINGANISHE NA MTU MWINGINE MAANA JUA NA MWEZI HAVIFANANI VYOTE UNG’ARA KWA WAKATI WAKE. TENGENEZA MAISHA YAKO ILI WATU PIA WATAMANI KUWA KAMA WEWE.

Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu

Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.

Pasipo kutegemea dereva wa gari la taka akaanza kufoka na kutoa matusi kwa kelele kubwa!

Katika hali ya kushangaza dereva wa taxi alitabasamu na kuwapungia mkono waliokuwa kwenye gari la taka na ndipo kwa mshangao nilimuuliza; “Inakuwaje ufanye hivyo wakati walitaka kutuua na hata kuharibu mali yako?”

Akajibu kwa upole akinitazama kwa tabasamu akasema. “Katika maisha yetu, kuna watu wako kama gari la taka. Wamejaa misongo, hasira, maumivu, wamechoka kifikra, kiuchumi na kimaisha, na wamejaa masikitiko mengi. Watu hao takataka zao zinazopowazidi hutafuta mahali pa kuzitupa na haijalishi mazingira wanakozitupia.

FUNZO!
Jifunze kutogombana nao. Wapungie mkono, wape tabasamu, songa mbele. Haikupunguzii kitu. Wala usiruhusu takataka zao zikupate.”

Uliumbwa kuyafurahia maisha. Usiyafupishe kwa kuamka asubuhi na kinyongo, na hasira, na ghadhabu kwa sababu ya mtu fulani.

Watafiti wanasema 10% ya maisha ni vile ulivyoyatengeneza lakini 90% ya maisha ni vile unavyochukuliana nayo.

Jifunze kuchukuliana na maisha kuliko vile unavyoyatengeneza huku ukimtegemea Mungu.

ANGALIZO!
Ukiona umeanza kueleweka, kukubalika, kutambulika, kufahamika, kuheshimika na kupata nafasi zaidi kwa kile unachokifanya kumbuka kuendelea kuzingatia misingi, nguzo, miiko na nidhamu iliyokuwezesha kufika hapo ulipo ili uende mbali zaidi.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

Mbinu za kulima parachichi ili kupata faida

Kilimo cha Parachichi nacho kinalipa ukilima.

Jifunze namna ya kulima nimeipata pahala

Agronomy ya Parachichi

Hali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto

Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko

Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo

-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi

1. Zipo aina za kiasili

Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)

Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass

-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi

– Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte

-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu

-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana

Upandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo

-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

-Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea

-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,

-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO

-Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24

MAVUNO

-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima ‘

FAIDA

kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000=10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi

Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda.

1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni.

View attachment 332289
Jani lililoshambuliwa na Alga

View attachment 332290
Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2.Magonjwa ya matunda


-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips

DAWA
-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.

Hitimisho

Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Jinsi ya kulima vizuri zao la kabichi

Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.

Aina za kabichi

Kuna aina nyingi za kabichi na zifuatazo ni miongoni mwa aina hizo:
1. Prize drumhead

Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
2. F1-High Breed

Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 2-4
3. Duncan

Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3
4. Early Jersey wakefield

Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
5. Sugar loaf

Aina hii hukomaa mapema sana, kiasi cha miezi 2.5
6. Glory of enkhuizen

Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5

Jinsi ya kulima kabichi

Hali ya hewa

Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari.

Udongo

Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji. Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.

Kitalu cha kabichi

Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana na matakwa ya mkulima. Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja. Katika upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika mbegu.
Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche. Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani.

Kuhamisha na kupanda

Hamisha na kupandikiza miche shambani ikiwa na umri wa wiki nne, wakati huo miche ikiwa na majani manne ya mwanzoni na urefu wa kiasi cha sentimita kumi na mbili (12). Wakati wa upandaji, ni vizuri udongo ukashindiliwa kwenye kila mche. Inafaa upandaji ufanyike mara moja, na ni vizuri ukafanyika nyakati za jioni au asubuhi sana, na udongo uwe na unyevu wakati wote.

Nafasi kati ya mmea

Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati ya mstari na mstari.

Mbolea

Ni vizuri kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya samadi iliyooza vizuri katika kila shimo.

Palizi

Wakati wa palizi ni vizuri mkulima akawa mwangalifu ili asiharibu mizizi. Wakati kabichi inapoanza kufunga hufunika ardhi, hivyo, husaidia kuzuia magugu yasiote, kwa wakati huu hakuna haja ya kupalilia.

Kuvuna:

Kabichi hukomaa katika kipindi cha siku 60-100 tangu kupandwa. Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga vizuri na huwa na uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada ya kuvunwa ili isikwaruzwe na kuoza kabla ya kutumiwa. Kwa kawaida hekta moja hutoa mavuno kiasi cha tani 50-80.

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Shopping Cart