Hadithi za Watoto na Wazazi

Kisa cha mama na mwanae na mkwe wake

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda. Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote. Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu.

Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo. Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ufanisi.
Kama umeipenda, itume kwa wengine ili nao wazinduke.

Read and Write Comments

Kisa cha baba mzee na mwanae

Mtoto alifanya maamuzi ya kumpeleka baba yake ambaye alikuwa Mzee sana kwenye Makazi Maalum ya kulelea wazee ya Kanisa Katoliki iliyokuwa CHINI ya uratibu wa Padre. Alifanya hivyo Baada ya kushauriwa Na mkewe aliyekuwa akiona Ni kero kumlea baba Mkwe wake nyumbani kwao.

Ofisa katika sehemu ya mapokezi alimuomba Mzee huyo achague chumba Kama anataka chenye TV Na Kiyoyozi Au la; Mzee akasema hahitaji chumba CHOCHOTE Chenye TV wala Kiyoyozi. Mwanaye ALIPOENDA kwenye Gari kuchukua begi la baba yake; mkewe aliyekuwa muda wote kwenye Gari akasisitiza Kuwa amwambie huyo Mzee asirudi nyumbani kabisa HATA Siku Za Sikukuu Kwa sababu yeye Mke hataki usumbufu wowote wa kumhudumia.

Mtoto huyo wa pekee kwa Mzee huyo alishangaa alivyorudi Na mizigo ya baba yake alipokuta Mzee wake akizungumza Kwa bashasha Na Padre wakionekana wanafahamiana sana, maana walionekana wakiongea kwa kukumbushana mambo ya zamani ambapo Mzee alionekana mchangamfu isivyo kawaida. Mtoto akamuuliza Padre “unamfahamu baba Yangu? Maana naona mnazungumza Kwa bashasha sana Kama mnafahamiana”

Padre akajibu “Ndiyo namfahamu sana Huyu Mzee mwema; alikuja HAPA miaka 30 iliyopita tukampatia Mtoto yatima wa kiume akamlee maana Mtoto huyo hakuwa Na WAZAZI Na yeye Na mkewe hawakuwa wamebahatika kupata Mtoto”

Mabegi aliyokuwa kayashika mkononi yalidondoka, akasimama Hapo kimya bila kusema kitu ……

Kisa HIKI kinatoa funzo kubwa sana Kwa kila mtu kuhusu kuwajali Na kuwahudumia WAZAZI wetu…..

Read and Write Comments

Huruma ya mama kwa mwanae ilivyomtesa

Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake.

Hata alipokuwa shuleni hakupenda mama yake amtembelee, na ikitokea mama yake akamtembelea basi watoto wenzie watamcheka siku nzima na kumtania. Hii ilimfanya mtoto huyu kujisikia vibaya sana na wakati mwingine kujuta kuwa na mama wa aina hiyo.

Lakini mama alimpenda mwanae na hakuonesha kukasirika hata pale mwanae alipomnyanyapaa waziwazi.

Badae mtoto akakuwa akamaliza masomo yake na kupata kazi nzuri. Akafurahi kuwa sasa amepata kazi atakuwa mbali na mama yake ‘chongo’ anayemtia aibu.

Akachagua kufanya kazi mji wa mbali na alipo mama yake. Akafanikiwa kazini kwa kupandishwa cheo na akawa mtu mashuhuri mwenye mali na mwenye heshima kubwa ktk jamii yake.

Siku moja asubuhi akasikia wanae wakilia walipokua nje wakicheza.. Alipowauliza wakasema kuna mtu anawatisha.. Akatoka nje kujua nani anayewatisha wanae. Kufika akamkuta mwanamke mmoja mzee mwenye jicho moja (chongo). Kumbe wale watoto walitishwa na chongo la yule bibi.

Alipomtizama vizuri yule mwanamke akamgundua ni mama yake mzazi. Alikua amechoka na amezeeka sana. Amedhoofu mwili na anaonekana mgonjwa..

Mtoto kwa hasira akamuuliza “mama umekuja kufanya nini hapa? Kama una shida ungenipigia simu sio kuja? kwanza nani kakuonyesha ninapoishi? Na nani kamruhusu mlinzi kukufungulia mlango? Ona sasa umewatisha wanangu kwa chongo lako”

Mama yake akasema “samahani mwanangu, sikujua naomba unisamehe”. Kisha mtoto akamchukua mama yake akamtoa nje na kumpeleka kituo cha basi ili arudi kijijini.

Baada ya siku chache kupita, yule jamaa akapata taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana na anahitaji kumuona. Akaondoka kwa siri kwenda kijijini ili akasikie mama yake anataka kumwambia nini.

Alipofika akakuta watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao. Alipouliza akaambiwa mama yake alifariki baada ya kuugua sana bila msaada wowote.

Alipoingia ndani akakuta barua aliyoandika mama yake.. Barua ilisomeka hivi…

“Kwako mwanangu mpendwa wa pekee,
Naandika barua hii nikiwa kwenye maumivu makali sana na sijui kama nitapona.. Nimeugua nikakosa matibabu kwa kutokuwa na fedha. Sikuwa na mtu mwingine wa kumueleza shida yangu zaidi yako wewe mwanangu wa pekee… Lakini nilipojitahidi kuja kwako angalau unisaidie matibabu ulinifukuza na kudai nawatisha wanao kwa chongo langu ! Uliniumiza sana mwanangu sitisahau maishani mwangu ila nimekusamehe.

Baba yako alifariki ukiwa mdogo sana. Nami sikubahatika kupata mtoto mwingine. Nilikulea kwa nguvu zangu zote na umasikini niliokuwa nao ilikuwa nikitegemea badae utanisaidia lakini umenitelekeza na kunitupa kwa sababu tu mimi mama yako ni chongo ! Hivyo unaona aibu kuwa nami….

Nisamehe kwa kuwatisha wanao kwa chongo langu, nisamehe kwa kuja kwako bila ya taarifa, nisamehe kwa kukufanya uchekwe na wenzio kwa kuwa mimi mama yako ni chongo….

Lakini naomba nikupe siri ambayo hukua unaijua ewe mwanangu, wewe ndiye uliyezaliwa ukiwa chongo. Ulikua na jicho moja tu. Nikaumia sana kuona mwanangu ana jicho moja, atawezaje kuishi na kukabiliana na changamoto za maisha.. Nikaomba madaktari wanitoe jicho langu moja wakupe wewe, Niliona ni heri mimi niwe chongo kwa kuwa nimeshaona mengi sana duniani kuliko wewe..

Na ulipowekewa jicho langu nilifurahi kukuona una macho mawili nikajua utaweza kuzikabili vema changamoto za dunia hii… Na hakika jicho langu limekusaidia kwani wewe ni mtu mashuhuri na tajiri sana kwa sasa…

Lakini kwa jinsi ninavyoumwa najua nitakufa. Ila nafurahi kuwa nakufa nikiwa nimetimiza haja ya moyo wangu. Kwa kutumia jicho langu umeweza kuwa msomi mzuri na tajiri unayeheshimika na jamii yote.. Wasalimie wajukuu zangu na waambie wawe na amani hawataniona tena nikienda kuwatisha na chongo langu.. Please take care of my eye…

Akupendaye,
Mama”

Alipomaliza kuisoma barua hii akalia sana. Akatamani mama yake afufuke amuombe msamaha na amlipe kwa wema wake aliomtendea.. Lakini haikuwezekana, it was TOO LATE.!

MORAL OF THE STORY.!

Nyuma mafanikio ya kila mwanaume yupo mwanamke. Anaweza kuwa mama yako, mke wako, dada yako au mchumba wako.. Je unatambua nafasi yake katika mafanikio yako au unampuuza tu?

Wapo wanawake ambao walijitoa sadaka ili uweze kuwa hapo ulipo. Jiulize mama yako amefanya mangapi kukufikisha hapo.

Hadithi hapo juu inatueleza juu ya mama aliyetoa jicho lake kwa mwanae.. lakini jicho ni kielelezo tu cha yale wanayofanya mama zetu.

Kuna wengine jicho lao ni vibarua alivyokua anafanya ili wewe usome.. Pengine jicho lake ni namna alivyokua akijinyima kwa kuvaa nguo moja mwaka mzima ili upate ada ya shule na mahitaji mengine.. Je umewahi kumshukuru mama yako kwa kutoa jicho lake kwa ajili yako??

Mpende sana mama yako.. Wapende wanawake wote, waheshimu, walinde, wajali. Wanapitia magumu mengi sana ili kutufanya sisi wanaume tuwe kama tulivyo.

Read and Write Comments
Shopping Cart