Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Ni hatua gani zinazochukuliwa na serikali ili kukomesha vitendo vya kuwinda Albino?

Kufuatia vitendo vibaya vya mauaji ya Albino, vilivyozuka
Tanzania tangu mwaka 2007 hadi sasa, Serikali imechukua
hatua kadhaa kurekebisha hali hiyo. Hatua hizo ni pamoja
na:
â€ĸ Kuliagiza jeshi la polisi kuwatafyta na kuwakamata wauaji
wa aalbino.
â€ĸ Kumteua Albino kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Wanawake.
â€ĸ Kutangaza hadharani kuwa mauaji haya siyo utamaduni
â€ĸ bali ni uhalifu mbaya ambao lazima uchukuliwe hatua za
kisheria.
â€ĸ Kutaka mikoa yote watangaze majina ya watu wote wanahusika
na mauaji haya.
â€ĸ Kuliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwakamata
wauaji wa Albino.
â€ĸ Kuanzishwa kamati maalumu ya mahakimu ili kuharakisha
hukumu za wauaji.
â€ĸ Viongozi wa juu wote wanalaani vitendo hivi katika mikutano
ya hadhara na matukio maalumu kama wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2009.

Kwani Albino hawatakiwi kuishi duniani?

Albino ni binadamu kama alivyo binadamu mwingine na ana haki
sawa za kuishi na kufaidi kuwepo kwake hapa duniani kama
ilivyo kwa binadamu wengine. Kuua Albino kwa sababu yoyote
ile ni jambo baya sana ambalo linakemewa na serikali, dini zote,
na kila mwanadamu mwenye akili timamu na maadili ya utu na
watetea haki za binadamu.
Kitendo hiki vilevile kinapingana na haki za binadamu kwa hiyo
wavunjaji wa haki hizi wanashtakiwa kisheria.

Watu wanaoua Albino wanapata faida gani?

Hakuna uchunguzi wa kisayansi ambao umeonyesha faida
yoyote inayopatikana kwa kuua Albino.
Madai ya kuwepo kwa faida katika mauaji ya Albino ni uvumi
mtupu unaoimarishwa na imani ya kishirikina na hazina msingi.
Kwa bahati mbaya uvumi huu umeimarika katika baadhi ya
jamii na hivyo kupelekea Albino kupata madhara makubwa
ya kujeruhiwa na wakati mwingine kuuawa katika jitihada za
kupata damu au viungo vya miili yao.
Kuua na kujeruhi ni kosa la jinai linaloadhibiwa kisheria. Serikali
kwa sasa ina msimamo mkali wa kukomesha makosa haya ya jinai
kwa kutumia sheria kuhukumu watuhumiwa wanapokamatwa hii
ni pamoja na kuelimisha jamii.

Kwa nini watu wanakuwa na hulka ya kuua Albino?

Vitendo vya kuua Albino tunavyovishuhudia sasa ni mambo
mapya na kwa kila hali siyo njia sahihi ya tiba ya jadi.
Baadhi ya waganga wa jadi hutumia viungo vya wanyama na
binadamu katika sherehe zao. Kwa mfano fuvu za binadamu
huwekwa chini ya msingi wa nyumba kuleta bahati njema, au
biashara nzuri. Damu huaminika kuongeza nguvu za kiume
(urijali) na kondo la nyuma hutibu utasa na ugumba.

Inatokeaje, katika baadhi ya mazingira baba anakataa kuwa mtoto si wake?

Katika mazingira fulani, baba anapomuona mtoto ana ngozi
nyeupe anakataa ya kwamba mtoto si wake akimlaumu mama wa
mtoto kuwa amekuwa na mahusiano ya ngono na mzungu. Huu
ni upuuzi kwa sababu kila mtu anajua kuwa watoto waliozaliwa
kutoka familia za watu weusi na wazungu siyo Albino kwa mfano
Rais wa Marekani Obama ni mtoto wa mama mzungu na baba
mweusi.

Dhana hii potofu ni matokeo ya uelewa mdogo na kutoaminiana.
Watu watakapokuwa na ufahamu na uelewa kuhusu ualbino
watapunguza kuwa na hisia kama alivyofanya huyu mzazi
aliyetajwa hapa juu.

Shopping Cart