Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?

Hakuna jibu la ujumla kwa swali hili, kwa sababu tiba ya ugumba inategemea chanzo maalum cha ugumba huo kwa mhusika. Kuna matatizo ya ugumba ambayo yanaweza kutibiwa, lakini mara nyingi ni vigumu au hata haiwezekani kumtibu mwanaume au mwanamke mgumba.
Kwanza kabisa, lazima daktari atafute sababu za ugumba kwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu kwa mwanamke na mwanaume. Baada ya uchunguzi daktari anaweza akawashauri kuhusu uwezekano wa kuwatibu. Mara nyingine tiba ni rahisi, lakini matatizo mengine ni mazito na ni vigumu au haiwezekani kuyatibu.

Nifanyeje ili niepukane na kuwa mgumba?

Sababu kuu ya ugumba unayoweza kujisababishia ni kupata magonjwa ya zinaa. Unaweza kuepuka kuwa mgumba kwa njia ya kuzuia kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya zinaa unaweza kuyazuia kwa njia ya kutojamii ana au kwa njia ya kutumia kondomu kila unapojamii ana. Kuna sababu nyingine za ugumba, nyingine unaweza kuzisababisha na nyingine ni za kimaumbile yako tangu ulipozaliwa.

Je, mwanamke ambaye ana hedhi kila mwezi, inawezekana kuwa mgumba?

Ndiyo, i inawezekana kwamba mwanamke anayepata hedhi yake kila mwezi akawa mgumba. Na vilevile i inawezekana kwamba mwanamke asiyepata hedhi kila mwezi siyo mgumba.
Ni kweli kwamba kuna uhusiano fulani kati ya hedhi na uwezo wa kupata mimba. Kupata hedhi kila mwezi i i inamaanisha kuwa mwanamke anao uwezi wa kutengeneza yai kila mwezi. Hata hivyo, siyo rahisi kuwa na uhakika i iwapo mirija ya kupitisha yai inaweza kulipitisha yai hilo kutoka kwenye kokwa hadi kwenye tumbo la uzazi. Kwa hiyo hata mwanamke ambaye anapata hedhi kila mwezi anaweza kuwa mgumba.
Ili mwanamke awe na uhakika kama ni mgumba au la, ni vyema akamwone daktari kwa ajili ya uchunguzi.

Je, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga shahawa bila shida, inawezekana kwamba ni mgumba?

Ndiyo, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga mbegu bila shida anaweza kuwa mgumba. Kutokuwa mgumba kuna maana kwamba uume wa mwanaume unaweza kusimama, kwamba mwanaume anaweza kumwaga shahawa na vilevile kwamba zile mbegu ni nzima na zina nguvu za kutosha za kurutubisha yai.

Kwa hiyo, hata kama mwanaume anamwaga shahawa, i inawezekana kwamba hazipo mbegu za kutosha ndani ya shahawa au kwamba mbegu hazina nguvu za kutosha. Mwanaume huyu ni mgumba. Ni daktari tu, anayeweza kumhakikishia mwanaume kuwa au kutokuwa mgumba.

Kama wameoana mume na mke na ikatokea hawapati mtoto, je, utajuaje kuwa tatizo liko kwa mwanamke au mwanaume?

Kwa wastani i i inachukua kama muda wa mwaka mmoja kwa mwanamke kuanza kupata ujauzito, wakikutana kimwili mwanaume na mwanamke bila kutumia njia ya kupanga uzazi. Wengine wanachukua muda mwingi zaidi, na wengine muda mfupi zaidi.
Kama baada ya muda wa mwaka mmoja au mwaka moja na nusu, mwanamke hajashika mimba, watu wanaanza kushangaa na kujiuliza chanzo cha hali hii ni kipi. Kwa sababu kuna vyanzo mbalimbali, lazima mwanaume na mwanamke waende kumwona daktari i i ili wakafanyiwe uchunguzi wa kitaalamu. Halafu daktari anaweza kutambua kama tatizo liko kwa mwanamke au mwanaume au kwa wote wawili. Yaani, bila kumwona daktari haiwezekani kuwa na uhakika tatizo liko kwa nani.
Mara chanzo cha tatizo kikijulikana, daktari anaweza kuwashauri mwanamke na mwanaume kuhusu uwezekano wa kuwatibu na kuwasaidia kupata mimba.

Shopping Cart