Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Kwa nini watu wengine hupenda kujamiiana na watu wa jinsi sawasawa? mapenzi ya jinsia moja

Ni vigumu kutoa jibu kamili kwa nini hisia hii i ii inatokea kwa watu wengine, kwa sababu wataalamu bado wanalifanyia utafiti.

Siku hizi, wataalamu wanafikiri kwamba kuvutiwa kimapenzi na jinsia ya aina moja kunasababishwa na mambo mengi, ambayo ni pamoja na maumbile au kwa kurithi. Vilevile jamii i ii inaweza kuchangia. Hata hivyo, wataalamu wanakazia kwamba suala hili bado halijafanyiwa utafiti wa kutosha na hivyo inawezekana kuna sababu nyingine.

Je, ni sahihi kuzungumza na wenzio/ marafiki juu ya uhusiano wangu wa kimapenzi?

Kama unavyohusisha rafiki zako katika mihemuko mingine, inaeleweka kama utataka kuwashirikisha katika uhusiano wako wa kimapenzi.

Hii i ii inaeleweka kabisa, ali mradi i uheshimu usiri na msimamo wa mpenzi wako.Hii i ii ina maana kuwa utawahusisha marafiki zako wa karibu na siyo hadharani na pia ni vema kama utafanya hivyo basi usitumie maneno ya kujigamba juu ya uzoefu au hata kukuza vitimbwi ambavyo kweli havikuwepo. Tumia maneno ambayo mpenzi wako naye angependa kuyasikia, yaani maneno ambayo hutaogopa kuyarudia kama angekuwepo na wewe hungejali kama yeye angetumia. Hii i ii itakusaidia kutunza siri na kuwa msiri.

Kumaliza ashiki au hamu ya kufanya mapenzi

Kwa vijana mara nyingine siyo rahisi kufahamu afanye nini mara anapopata ashiki (hamu) ya kutaka kujamii ana. Unaweza ukajaribu kujisahaulisha kwa kufanya mambo mengine kama kucheza michezo kujifu-nza, kujisomea, kuwasaidia wazazi kazi za nyumbani au kuungana na vijana wen-zako katika shughuli za vikundi katika jamii . Vijana wengine huoga maji ya baridi kuondoa ashiki.

Kujisikia hamu ya kutaka kujamii ana au uume kudinda haimaanishi kwamba ni lazima ujamii ane. Kujamii ana ni njia mojawapo tu ya kuonyesha mapenzi. Kuna njia nyingine ambazo hutumika, kwa mfano kubusu, kuongea, kushikana mikono, kukumbatiana na kushikanashikana.
Njia nyingine ya kutumia kumaliza hamu ni kupiga punyeto. Kupiga punyeto ni kitendo cha msichana kushikashika na kusugua taratibu kinembe chake mpaka anafikia mshindo au kitendo cha mvulana kusuguasugua uume wake mpaka akojoe manii . Watu wengi wanaopiga punyeto hufanya hivyo wakiwa peke yao. Kupiga punyeto hakuna madhara yoyote ya kiafya wala kiakili.
Kwa vyovyote vile, kama huwezi kabisa kuacha kujamii ana, hakikisha mapenzi yawe salama. Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizo ya VVU na UKIMWI. Kwa upande mwingine, mapenzi salama yanaweza kuwa ni vitendo vya kumaliza hamu bila kuhusisha sehemu za siri za mwanamke na mwanaume kukutana. Kwa upande mwingine mapenzi ya uume kuingizwa ukeni yanakuwa pia salama i iwapo tahadhari imechukuliwa kwa maana kwamba kondomu i litumika.

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madhara yatakayokutokea kwenye sehemu zako za siri au katika sehemu nyingine ya mwili wako. Mwanaume au mwanamke akianza kujamii ana baada ya kukaa muda mrefu, atapata raha na starehe.

Watu wengine wanasema kwamba kutofanya mapenzi kunasababisha kuwa na chunusi usoni au sehemu za siri, au hata kuchanganyikiwa kiakili. Siyo kweli kwamba hali hizi zinasababishwa kwa kutojamii ana, vyanzo vya hali hizi ni tofauti.
Uwe na uhakika kwamba kutojamii ana ni salama kabisa kwako na huwezi kupata madhara yoyote. Lakini kama tulivyosema awali, kujamii ana kunaweza kukaleta matatizo mengi kama mimba i isiyotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizo ya VVU na UKIMWI.

Shopping Cart