Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madhara yatakayokutokea kwenye sehemu zako za siri au katika sehemu nyingine ya mwili wako. Mwanaume au mwanamke akianza kujamii ana baada ya kukaa muda mrefu, atapata raha na starehe.
Watu wengine wanasema kwamba kutofanya mapenzi kunasababisha kuwa na chunusi usoni au sehemu za siri, au hata kuchanganyikiwa kiakili. Siyo kweli kwamba hali hizi zinasababishwa kwa kutojamii ana, vyanzo vya hali hizi ni tofauti.
Uwe na uhakika kwamba kutojamii ana ni salama kabisa kwako na huwezi kupata madhara yoyote. Lakini kama tulivyosema awali, kujamii ana kunaweza kukaleta matatizo mengi kama mimba i isiyotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizo ya VVU na UKIMWI.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments