Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, madhara gani yatawapata wasichana na wavulana wanaojamiiana kwa kutumia sehemu ya haja kubwa?

Tunasema ngono kutumia njia ya haja kubwa pale ambapo uume uliodinda unaingizwa kwenye njia ya haja kubwa (mkunduni).

Tatizo kubwa la kujamii ana sehemu ya haja kubwa, ni kwamba kuna uwezekano wa kueneza magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya VVU na UKIMWI zaidi kuliko kutumia njia ya kawaida ya uke. Kujamii ana sehemu ya haja kubwa ni hatari kwa sababu hakuna yale majimaji kama ukeni na ngozi ni laini sana. Kwa hiyo michubuko i inaweza kutokea kwa urahisi. Michubuko hii i ii inasababisha maumivu na pia i inarahisisha kuambukizana magonjwa ya zinaa.
Kama bado umeamua kujamii ana kwa kutumia njia ya haja kubwa pamoja na usumbufu wote tulioutaja hapo juu, unashauriwa kutumia kondomu i li kuzuia uambukizaji wa magonjwa.

Je, mvulana anaweza akafikia mshindo kwa njia ya kusugua uume na vidole na kuna madhara gani ukisugua uume na vidole?

Ndiyo, mvulana anaweza akafikia mshindo kwa njia ya kusugua uume na vidole. Anaposuguliwa uume na vidole, msisimko wa mwili unaongezeka na damu zinaingia kwenye mishipa ya damu katika uume.

Basi, uume unasimama na mara nyingi ukiendelea kusuguliwa mvulana anamwaga mbegu zake. Kusugua uume ni njia salama ya kumaliza ashiki ya kutaka kujamii ana. Hakuna madhara yoyote ya kiafya wala kiakili kama uume unasuguliwa. Watu wengine wanasema kwamba kupiga punyeto inasababisha shida ya kisaikolojia kutokea na nguvu ya kiume kupungua. Wengine wanasema kwamba mtu anayepiga punyeto atashindwa kujamii ana na mwanamke. Lakini si kweli, ni uvumi potofu tu.

Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)?

Kufanya mapenzi wakati msichana yuko katika hedhi hakuna madhara yoyote kiafya kwa mwanaume wala mwanamke kama kati yao hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa.

Ila kama mmoja wapo ana ugonjwa wa zinaa, huo ni wakati wa hatari sana kwa maambukizi, kwa sababu utando ndani ya mfuko wa uzazi unabomoka na mlango wa mfuko wa uzazi unakuwa wazi. Hivyo ni rahisi sana vijidudu vya magonjwa mbalimbali kuingia mwilini mwa msichana. Vilevile kama msichana tayari ameambukizwa na magonjwa ya zinaa, katika damu yake viko vijidudu vingi vinavyoweza kumwambukiza mvulana.

Kwa sababu mara nyingi ni vigumu kufahamu kama kati ya wapenzi hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa, haishauriwi kujamii ana wakati wa hedhi na kama ndivyo basi kondomu i tumike.

Katika jamii nyingi kujamii ana wakati mwanamke yuko wenye hedhi haikubaliki kwa sababu ya mila au dini.

Shopping Cart