Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Madhara ya sigara na pombe kwa mtoto

Watoto hawatakiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara!

Watoto hasa ndio wapo katika hatari zaidi ya kupata madhara
yatokanayo na uvutaji sigara na unywaji pombe, kwa sababu
bado wanaendelea kukua. Wanaweza wakaathiri miili yao na ubongo
kwa maisha yao yote. Wana hatari zaidi ya kuathirika katika
maendeleo yao ya kijamii na kisaikolojia. Matumizi mabaya ya pombe
na sigara yanaweza yakaleta madhara katika makuzi ya mtoto.

Wanawake wanaweza kulewa haraka kuliko wanaume?

Wasichana na wanawake wanaweza kulewa kwa ujumla.
Mara nyingi, hulewa pombe haraka kuliko wanaume. Hii
inatokana na uzito mdogo wa miili yao, na kiasi cha mafuta na
maji katika miili yao. Kilevi husambaa kiasi kikubwa katika miili
ya wanawake. Maini yao huharibika kirahisi zaidi kuliko maini
ya wanaume.

Kutokana na kilevi, wanawake au wasichana huwa wepesi
kufanya vitu ambavyo wasingefanya kama wasingelewa.
Wanaume hutumia nafasi hii kuwashawishi kufanya mapenzi
bila kuchukua tahadhari yoyote kama vile kutumia kondomu ili
kupunguza maambukizo ya VVU.

Madhara ya pombe kwa mwili na akili

Pombe huingia kwenye damu na kuzunguka mwili mzima pamoja
na kwenye ubongo wako. Ina madhara kwa viungo vya mwili
wako na ubongo wako na hivyo huathiri tabia na hisia zako.

Unywaji wa pombe kupita kiasi unaweza kuathiri viungo vingi
kwa mfano, ini ambalo ndilo huathirika zaidi. Ini hilo linafanya
kazi ya kufyonza kilevi katika mwili wako. Kama ukinywa zaidi
utaathiri ini kiasi kwamba halitaweza kufanya kazi kikamilifu au
litashindwa kabisa hatimaye utakufa. Kilevi kingi husababisha
kansa ya ini na tumbo.

Hatari kubwa siku hizi ni kupata na kusambaza virusi vya
UKIMWI. Mlevi mara nyingi huwa mzembe na husahau kinga
muhimu kama vile kutumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi.
Anaweza pia kufanya mapenzi na watu ambao hafahamu afya
zao, kama ni wagonjwa au la. Zaidi ya hayo mlevi mara nyingi
huwa dhaifu, hivyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa
mbalimbali pamoja na VVU.

Pombe inaathiri pia uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Huwa ni
vigumu kwa uume kusimama. Pia huathiri ubongo hasa sehemu
zile zinazomiliki ufahamu na mihemko.

Kwanza unaweza kujisikia mchangamfu na huru, lakini mara
tu unaanza kujisikia taabu na kushindwa kutembea vizuri.
Utakuwa na matatizo ya kutoona vizuri na matatizo ya kutoa
uamuzi sahihi. Watu huanza kuwa na vijitabia vya ajabu na
vipya baada ya kulewa. Kugombana na watu wengine na kufanya
mambo yasiyokubalika kama vile kujikojolea mbele za watu.
Kama utaendelea kunywa kuna uwezekano mkubwa wa kupata
madhara. Kila dhara huharibu mamilioni ya seli za ubongo wa
binadamu.

Kwanza hutakuwa na kumbukumbu ya nini kimetokea, lakini
unaweza pia kupoteza kabisa kumbukumbu zako. Kama ukinywa
pombe kupita kiasi kwa muda mrefu unaweza kupungukiwa
akili na mwisho kuharibu kabisa akili. Pombe pia ni dawa ya
kulevya kwani huweza kukutawala. Watu waliotawaliwa na
pombe, hutumia pesa nyingi na muda mwingi kwenye pombe,
hali ambayo inaweza kuwa ni mzigo mzito kwa familia na jamii,
na pindi mtu anapotawaliwa, ni vigumu kunywa kidogo au kuacha
kabisa. Kama mtu atajaribu kuacha, hupata matatizo kama
kutetemeka, mapigo ya moyo kuongezeka, kutokwa na jasho
jingi, na kukosa usingizi wakati wa usiku. Hali hiyo husababisha
maumivu na ni hatari kwa watu ambao wametawaliwa na pombe.

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

Ndiyo, lakini ni mwanzo tu na kwa muda mfupi; hii ni kwa
sababu mwanzoni nikotini iliyomo katika sigara inasababisha
damu kumiminika kwa wingi kupita kwenye ubongo wako. Hivyo,
husababisha msisimko na kukufanya ujisikie raha. Nikotini
pia inasababisha misuli mwilini kujichua na hivyo kukufanya
ujisikie mchangamfu.

Baada ya muda utajisikia kinyume na ulivyojisikia mwanzoni.
Kama utavuta zaidi na zaidi damu na oksijeni kidogo vitatiririka
mwilini na kwenye ubongo. Hii itakufanya ujisikie mchovu na
mwenye huzuni.

Kwa bahati mbaya baadhi ya matangazo ya biashara au
marafiki watakushawishi kwamba, uvutaji wa sigara ni safi, poa
na hukufanya kujisikia mkubwa. Lakini hawaongelei madhara
mabaya kiafya yatokanayo na uvutaji wa sigara na ugumu wa
kuacha uvutaji huo pale utakapoizoea.

Nikotini mara nyingi
huitwa kianzisho. Hii inamaanisha kwamba wakati mwingine
vijana wanaanza kuvuta sigara na kisha kuhamia kwenye
utumiaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo uvutaji ni gharama.

Kwa nini watu wanakunywa pombe?

Unywaji wa pombe ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania na nchi
nyinginezo duniani.

Watu hupendelea kunywa pombe katika
sherehe za kidini, kijamii, nyumbani na vilabuni. Wanakunywa
pombe ili kujiburudisha, lakini pia kuongeza ujasiri, kuondoa
aibu au kusahau matatizo yao kwa kipindi fulani au kwa muda
mfupi.

Vijana wengi, hasa wavulana, hudhani kwamba kunywa
pombe ni ishara ya kujionyesha kuwa wamekuwa watu wazima.
Kimsingi, unywaji pombe kidogo hukubalika kijamii na hauna
madhara, lakini ulevi wa kupindukia ni hatari na huweza
kusababisha vifo na haukubaliki katika jamii zetu kwa sababu
hudhoofisha na kufanya watu kusahau majukumu yao, hupunguza
heshima na afya njema.

Shopping Cart