Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, Tanzania kuna Albino wangapi?

Idadi kamili ya Albino Tanzania haijulikani kwani hakuna
aliyewahesabu. Inakisiwa kufuatana na tafiti katika nchi
nyingine kama Nigeria na Afrika Kusini kuwa mtu 1 kati ya
4,000- 5,000 ni Albino hapa Tanzania. Namba hii ni kubwa mara
nne au mara tano ukilinganisha na Ulaya au Marekani ambako
tunapata Albino 1 kati ya watu 15,000-20,000. Hapa Tanzania
inakisiwa kuwa kuna Albino wapatao elfu kumi.

Ualbino unarithiwa vipi?

Watoto wengi wanaozaliwa na ualbino, wazazi wao wana rangi
ya ngozi, nywele na macho inayafanana na watu wa kabila /asili
yao. Mwili wa kila mwanadamu una seti mbili za vinasaba (moja
hutoka kwa mama na moja hutoka kwa baba). Mtu anaweza
kuwa na rangi ya asili ya kawaida, lakini akawa na kinasaba cha
ualbino. Kama mtu ana kinasaba kimoja cha rangi ya asili na
kimoja cha ualbino atakuwa na taarifa za vinasaba vya kutosha
kutengeneza rangi ya asili. Kinasaba cha ualbino ni seli dhoofu
haiwezi peke yake kuonyesha ualbino mpaka mtu awe nazo
mbili kwa pamoja.
Kama wazazi wote wawili wana vinasaba vya ualbino na wote
hawaonyeshi ualbino, kuna uwezekano wa kupata mtoto Albino
kati ya mmoja katika wanne kwa kila mimba.

Ualbino husababishwa na nini?

Watu wenye ualbino hawana uwezo kabisa au wana uwezo mdogo
wa kuwa na rangi kwenye ngozi zao, nywele na macho. Rangi hii
huitwa β€œmelanini”. Rangi ya ngozi itategemeana na kiasi cha
melanini kilichopo. Hali ya kuzalisha melanini imekaa katika
vinasaba vyetu. Kama vinasaba vya kutoa melanini havipo au
vimebadilishwa madhara yake ni ukosefu au upungufu wa rangi.
Kwa hiyo hali ya ualbino ni ya kurithi. Inaweza kurithishwa
kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto.

Nini maana ya Ualbino?

Albino wana ngozi nyeupe, nywele nyeupe au nyekundu na macho
ya kijivu au ya bluu. Ngozi yao ni nyeupe zaidi kuliko ndugu zao
wa familia moja au watu wa jamii yake
ambao hawana hali ya ualbino. Ngozi hii inaonekana zaidi kuwa
nyeupe katika familia za watu weusi, ingawaje, ualbino
hutokea kwa watu wa kila taifa, rangi, kabila na dini. Albino
wako katika mabara yote ulimwenguni.

Shopping Cart