Baini Siri za Kuwa na Afya Bora na Utimamu

Sababu, dalili na matibabu ya tatizo la kuziba kwa mrija wa mkojo

Mrija wa mkojo (urethra) ni kiungo muhimu kinachotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu. Mrija huu unaposinyaa au kuziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa
mashaka na maumivu makubwa. Kusinyaa/ Kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa pia
urethral stricture.

Visababishi na vihatarishi vya tatizo hili

Kusinyaa kwa mrija wa mkojo husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya
mrija baada ya mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa.

Inaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu na eneo la kinena unaokandamiza mrija.
Vihatarishi vya tatizo hili ni pamoja na

Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya zinaa

kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya namna hiyo (catheter au
cystoscope)

  • Kuvimba tezi dume (BPH) kwa wanaume
  • Kuwa na historia ya kuumia au kupata majeraha maeneo ya kinena. Hii hutokea

sana kwa wale wanaopata ajali wakiendesha baiskeli

  • Kupata maambukizi ya mara kwa mara ya mrija wa mkojo (urethritis)
  • Ni nadra sana kwa tatizo hili kutokea kwa wanawake. Aidha ni nadra pia kwa

mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo hili (congenital urethral stricture).

Dalili za tatizo hilo.

Mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo,

  • Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu.
  • Kukojoa mkojo mweusi au uliochanganyika na damu.
  • Kupungua kwa kiasi cha mkojo kinachotolewa.
  • Kukojoa kwa shida.
  • kutoa uchafu katika mrija wa mkojo.
  • kukojoa mara kwa mara.
  • Kushindwa kumaliza mkojo wote.
  • Kushindwa kuhimili kutoka kwa mkojo (mkojo kujitokea wenyewe/kujikojolea).
  • Maumivu wakati wa kukojoa.
  • Maumivu chini ya tumbo.
  • Maumivu ya kinena
  • Mtiririko dhaifu wa mkojo (hutokea taratibu au ghafla)
  • Mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa
  • Kuvimba uume

Uchunguzi

Daktari atakufanyia uchunguzi wa mwili na namna unavyokojoa. Uchunguzi wa mwili
unaweza kuonesha:

  • Kupungua kwa mkondo wa mkojo
  • Uchafu kutoka katika mrija wa mkojo
  • Kibofu kilichojaa/kuvimba
  • Kuvimba kwa mitoki ya maeneo ya kinena
  • Tezi dume iliyovimba au yenye maumivu
  • Kuhisi kitu kigumu chini ya uume
  • Uume kuvimba au kuwa mwekundu
  • Hata hivyo, wakati mwingine uchunguzi unaweza usioneshe tatizo lolote lile.

Vipimo

Vipimo ni pamoja na

  • Kipimo cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy)
  • Kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya kukojo (Post-void

residual (PVR) volume)

  • X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram)
  • Vipimo vya magonjwa ya zinaa

Matibabu

Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo
mojawapo ya tiba. Iwapo njia ya kutanua mrija haioneshi mafanikio sana, upasuaji
unaweza kuhitajika. Upasuaji unategemea eneo lilipo tatizo na ukubwa wa tatizo.

Kama tatizo ni dogo/fupi na lipo mbali na bawabu inayotenganisha mrija na kibofu cha mkojo,
linaweza kutatuliwa kwa kukata kasehemu kalikoziba wakati wa kufanya cystoscopy au
kwa kuweka kifaa maalum cha kuzibua na kutanua mrija.

Kama tatizo ni kubwa zaidi, upasuaji wa wazi wa eneo husika unaweza kufanyika.
Upasuaji huu unajumisha kukata sehemu iliyoziba na kisha kukarabati sehemu hiyo.

Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa kutoa mkojo (acute
retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea catheter kupitia juu ya kinena
(suprapubic catherization) hufanyika. Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye
bomba lililowekwa chini ya tumbo.

Ifahamike kuwa mpaka sasa hakuna dawa ya tatizo hili zaidi ya njia za upasuaji na
nyingine zilizoelezwa hapo juu.

Matarajio

Mara nyingi matibabu huleta matokeo mazuri na mgonjwa anaweza kuishi maisha yake
kama kawaida. Hata hivyo wakati mwingine, mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu ya
mara kwa mara ili kuondoa sehemu ya kovu iliyopo katika mrija wa mkojo.

Madhara ya tatizo hili

Tatizo hili halina budi kutibiwa haraka maana kama likiachwa linaweza kusababisha
kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali
ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo
kushindwa kufanya kazi (ARF).
Kinga

Ni muhimu kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kwa kufanya ngono salama au kuacha
kabisa kufanya ngono. Aidha kuwa makini na kazi au mambo ambayo yanaweza
kukusababishia kuumia maeneo ya kinena.

Tikiti maji kama dawa ya kutibu nguvu za kiume

Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’, ‘Magnesium’ na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction).

Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.

Tikitimaji lina kirutubisho aina ya ‘arginine’, ambacho huchochea uzalishaji wa ‘nitric oxide’ kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa ya Viagra.

Kazi nyingine zinazofanywa na tikiti maji katika mwili wa mwanadamu;

Huimarisha mishipa ya damu.

Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya ‘Potassium’ kama vile Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.

Husaidia kupunguza uzito wa mwili.

Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji.

Huimarisha kinga za mwili.

Kirutubisho cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili.

Huondoa sumu mwilini.

Kuondoa ‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.

Tunda hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.

Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo

Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika dunia, watu wamekuwa wakiteseka bila kujua nini chanzo cha tatizo hili na vipi kuliondoa tatizo hili na wengine wamekuwa wakilipuuzia bila kujua madhara ambayo wanaweza kuyapata kutokana na tatizo hili.

Tatizo hili hutokea pale mtu anakula vizuri lakini unakata siku tatu hadi nne bila kupata choo. Ukiona unakula kutwa mara tatu na unakaa siku mbili hadi tatu huendi chooni au unatoa choo kigumu kama mbuzi hilo ni tatizo kwako.

Tafiti zinaonyesha mtu anaweza kupoteza maisha kama atakosa choo kwa siku tano hadi saba mfululizo.Watu wengi hulidharau tatizo hili lakini linamadhara makubwa tofauti na wanavyofikiria.

Zifuatazo ndizo sababu za kukosa choo;

  • Kupenda kula saana vyakula vilivyokobolewa (mfano ugali wa sembe,mikate n.k)
  • Ukosefu wa mbogamboga za majani na matunda ya faiba kama machungwa,ukosefu wa kula mboga za majani na matunda hasa ya faiba kama machungwa huongeza tatizo hili.kila mtu anatakiwa kula matunda aina mbili na mboga za majani aina mbili kila siku.
  • Matumizi makubwa ya pombe na sigara
  • Unywaji mdogo wa maji. Kila mtu anapaswa kunywa maji kwa kiwango cha chini lita 3 kila siku na usinywe maji wakati unakula, kunywa maji nusu saa kabla au baada ya kula.
  • Matumizi mabaya ya madawa. Mfano dawa za presha, aleji n,k.
  • Kuugua kisukari au ugonjwa wa misuli.
  • Kansa ya utumbo mpana

Yafuatayo ndiyo madhara yatokanayo na kokosa choo;

  1. Unaweza kuugua saratani ya utumbo mpana.
  2. Unaweza kupata tatizo la tumbo kujaa gesi.
  3. Figo yako inaweza isifanye kazi vizuri.
  4. Unawezasababisha magonjwa ya moyo.
  5. Unaweza pata tatizo la kukakamaa mishipa ya damu ambapo utasababisha miguu kuwaka moto na ganzi miguuni au mikononi.
  6. Unawezasababisha magonjwa ya ini
  7. Unawezapata kisukari

Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita 9 hadi 18 na huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka 6 na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50.

Lakini pia tunda la shelisheli ni zao kuu maeneo ya Pasifiki na lina kiwango kikubwa cha wanga na huweza kuliwa likiwa bichi au baada ya kupikwa.

Tunda hili lina faida mbalimbali zikiwemo za kiafya na za kiuchumi, lakini moja ya sifa kuu ya tunda hili ni kuwa na kiwango kizuri cha wanga.

Kutokana na kiwango kikubwa cha wanga kwenye shelisheli kunalifanya tunda hilo kutumika badala ya unga wa ngano kwenye baadhi ya nchi na hivyo hutengenezewa chapati.

Aidha, utomvu wake unaelezwa kutumika kama njia asili ya kupunguza matatizo ya kuhara na magonjwa ya ngozi.

Hivyo basi kwa kuzingatia na kujali afya yako unashauriwa kuweza kutumia tunda hili ili uweze kuifanya ngozi yako iwe nyororo lakini pia uweze kujitibu matatizo yote yatokanayo na kuhara.

Sababu, dalili, matibabu na kinga ya fangasi sehemu za siri kwa mwanamke

Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.

Maambukizi

Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya;
Vyoo vichafu.
Kuchangia nguo za ndani na taulo.

Sababu

Uwezekano wa kupata fangasi ya uke au fangasi ya uke kujirudia rudia unaongezeka pale ambapo mwanamke ana;
Kisukari.
Ujauzito.
Anatumia antibiotics kwa muda mrefu
Ukimwi.
Joto, unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu haumbukizwi kwa njia ya ngono.

Dalili

Fangasi ya ukeni inaweza kuleta dalili zifuatazo kwa wagonjwa wenye maambukizi;
Kuwashwa sehemu za siri hasa wenye uke na mashavu ya uke.

Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya.
Maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisabaishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.

Matibabu

Matibabu ya fangasi ya uke hutumia dawa za kuua fangasi (antifungals). Mara nyingi dawa za kuingiza kwenye uke (vaginal pessaries) hutumika kwa muda wa siku 3 mpaka 6. Wakati mwingine dawa za kunywa zinaweza kutumika kutibu fangasi hii.

Muone daktari kwa ajili ya uchunguzi, dawa na dozi sahihi.Cotrimazole na ketoconazole ni kati ya dawa zinazotumika mara kwa mara.

Kinga

Pamoja na matibabu kuna hatari ya maambukizi ya fangasi hawa kujirudia, hivyo ni muhimu kupata tiba hospitali na kurudi unapoona inajirudia. Vitu vingine muhimu kuzingatia ni;
Usafi wa nguo za ndani; kuvaa safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).

Vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.

Vaa nguo za ndani zilizotengezwa kwa pamba (hupunguza joto na hivyo hatari ya fangasi kuzaliana)

Usafi wa sehemu za siri na kujikausha viruzi baada ya kuoga.

Usafi wa choo ni muhimu sana.

Shopping Cart