Watu wawili👬 walikuwa wanakunywa pombe🍺🍻 baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana🙅🏾♂ na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi.
Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga. Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena.
Kumbe amemwua mwenzie.😰
Ndipo alipoanza kukimbia🏃🏾 huku shati laki likiwa limechafuka sana na damu. Wale waliyokuwa wanauangalia ule ugomvi wakaanza kumfukuza.
🏃🏾 🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾
Huyu mwuaji akakimbilia kwenye 🏡🏃🏾nyumba ya mtu mmoja mcha Mungu na akamwomba yule mtu amfiche maana ameua mtu na watu walikuwa wanamfukuza.
Yule mcha Mungu akasema nitakuficha wapi wakati mimi nina chumba kimoja tu?😨
Yule mwuaji akamjibu akamwambia acha kuendelea kupoteza wakati fikiria tu mahali pa kunificha. Yule mcha Mungu akavua shati👔 lake safi akampa yule mwuaji alafu yeye akachukua lile shati la muaji lililojaa damu akalivaa.
Akampa sharti yule mwuaji na kumwambia tunza shati langu usilichafue. Yule mcha Mungu alipofungua mlango wa chumba chake wale watu wakamvamia🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾 na kumpiga sana wakijua yeye ndo mwuaji huku mwuaji akiondoka salama na kurudi kwake.
Baada ya kumpiga sana yule ndugu akapelekwa polisi👮🏾👮🏽♀ na baadaye akapelekwa mahakamani na akahukumiwa kunyongwa👴🏼 kwa kumwua mtu mwingine.
Yule mwuaji halisi akiwa kule nyumbani alijisikia vibaya sana😞 akaenda mahakamani akajisalimisha akasema yeye ndiye aliyeua, yule ndugu aachiwe huru.
Hakimu⚖ akamwambia umechelewa, yule ndugu kesha nyongwa.
Alilia😭😩 sana na kujiambia kuwa yule mtu amekufa kwa kosa ambalo sio lake.😰
Akakumbuka maneno ya mwisho ya yule ndugu _*”LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE.”*_
Wapendwa,
YESU alikufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu. Alichukua vazi letu lililochafuliwa na uchafu wa dhambi zetu akatupa vazi Lake takatifu la haki. YESU aliuawa kwa kosa lako na langu. Akatupa haki Yake na kutuambia tusichafue tena maisha yetu.
Kuendelea kutenda dhambi baada ya yale ambayo Yesu ametufanyia ni kuidharau sana kazi ya msalaba na kuikanyagia chini Damu Yake ambayo tumesafishwa kwayo.
Ni kushindwa kuthamini kuwa kuna mtu alishakufa kwa ajili yetu. Ni kushindwa kutambua uthamani wa wokovu ambao tumeupokea.
Wapendwa,
*Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii?*
T A F A K A R I
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Dumu katika Bwana.
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Rehema hushinda hukumu
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Neema ya Mungu inatosha kwako
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Nguvu hutoka kwa Bwana
Tumaini ni nanga ya roho
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Endelea kuwa na imani!
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Imani inaweza kusogeza milima
Baraka kwako na familia yako.
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Mwamini katika mpango wake.
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Mungu akubariki!
Neema na amani iwe nawe.
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Nakuombea 🙏
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Katika imani, yote yanawezekana
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Mwamini Bwana; anajua njia
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Sifa kwa Bwana!
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Rehema zake hudumu milele
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Mungu ni mwema, wakati wote!
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi