Kwa nini vijana wengine Albino wanaanza kujamiiana katika umri mdogo?

Kuna sababu nyingi ambazo zinamfanya kijana kuanza kujamiiana
katika umri mdogo. Baadhi ya sababu hizi ni kama vile:
• Ushindani kati ya vijana wa kuwa na vitu vya anasa kama
vile simu ya mkononi, saa na vitu vya kuchezea. Ama kutaka
mahitaji ya pesa kwa ajili ya kulipa ada ya shule.
• Shinikizo kutoka kwa rika wa kumfanya mtu ajiingize kwenye
kujamiiana. Shinikizo rika unakuwa na nguvu zaidi kwa
kijana Albino kwani yeye tayari anajiona ametengwa na
hivyo kushawishika zaidi katika mambo wanayofanya wengine
ili akubalike na wanarika hao.
• Kwa kuamini kwamba njia halisi ya kuonyesha mapenzi ni kujamiiana
na pia kulazimika kujamiiana hata kama ni kinyume
na matakwa yake kwa mtazamo kuwa haya ndio mapenzi ya
kweli.

Je, kuna madhara yoyote yanayompata kijana Albino wa kike au wa kiume anayeamua kutoanza kujamiiana hadi afikie umri uliokubalika?

Ukweli ni kwamba hakuna athari zinazojulikana kwakusubiri au
kuacha kujamiiana hadi mtu afikie umri unaokubalika / utu uzima
au hata muda mrefu zaidi. Pia via vya uzazi havitaathirika kwa
njia moja au nyingine (havisinyai wala kutoweka.) Kuna uvumi
potofu unaodai kuwa watu wanaoacha kujamiiana kwa muda
mrefu wanaota chunusi na upele usoni au pia kwenye sehemu
zao za siri na wengine kuchanganyikiwa. Hakuna ukweli wowote
kuhusu uvumi huu. Kuwa na chunusi usoni ni mojawapo ya hali
inayowakabili vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 19. Hali ya
kuota chunusi inasababishwa na kuwepo mafuta mengi kwenye
ngozi. Hali hii hubadilika kadri umri unavyosogea mbele. Mara
nyingi inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili ili kuwezesha
vitundu vilivyopo kwenye ngozi kufunguka na kuwezesha ngozi
kupumua.
Hakuna madhara ya kiafya ambayo yanatokana na kuacha
kujamiiana, bali kinyume ni kuwa, kuna madhara mengi ya
kiafya, hisia na ya kimwili yanayotokana na kujamiiana katika
umri mdogo kama vile mimba zisizotarajiwa, uambukizo wa
magonjwa yatokanayo na kujamiiana pamoja na Virusi vya
UKIMWI.

Hatua gani zichukuliwe dhidi ya wanaowakeketa au kuwachezea unyago Albino juani?

Swali hili linaonyesha mambo mawili ambayo ni mabaya. Jambo
la kwanza ni ukeketaji ambao ni kinyume dhidi ya haki ya afya
ya uzazi kwa mwanamke na ni uvunjaji sheria ya kukeketa mtoto
wa kike. Jambo la pili ni kuwacheza Albino unyago juani. Kitendo
hiki ni kuwaumiza Albino kwa sababu ya ulemavu walionao wa
ngozi watapata madhara wakikaa sana juani. Pia hii ni aina ya
unyanyapaa kwa nini weusi wachezeshwe ndani na Albino juani?

Hii ni imani potofu. Ushauri unaotolewa hapa ni kutoa taarifa
kwenye serikali na jamii husika ili wachukue hatua. Kwa sababu
ni vitendo labda vilivyokubalika na jamii kama mila, ni muhimu
kuhusishwa watu wenye umaarufu katika hiyo jamii ili waweze
kushawishi jamii kubadilika. Watu hawa ni kama viongozi wa
dini na wazee mashuhuri katika jamii.

Ni hatua gani zinazochukuliwa na serikali ili kukomesha vitendo vya kuwinda Albino?

Kufuatia vitendo vibaya vya mauaji ya Albino, vilivyozuka
Tanzania tangu mwaka 2007 hadi sasa, Serikali imechukua
hatua kadhaa kurekebisha hali hiyo. Hatua hizo ni pamoja
na:
• Kuliagiza jeshi la polisi kuwatafyta na kuwakamata wauaji
wa aalbino.
• Kumteua Albino kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Wanawake.
• Kutangaza hadharani kuwa mauaji haya siyo utamaduni
• bali ni uhalifu mbaya ambao lazima uchukuliwe hatua za
kisheria.
• Kutaka mikoa yote watangaze majina ya watu wote wanahusika
na mauaji haya.
• Kuliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwakamata
wauaji wa Albino.
• Kuanzishwa kamati maalumu ya mahakimu ili kuharakisha
hukumu za wauaji.
• Viongozi wa juu wote wanalaani vitendo hivi katika mikutano
ya hadhara na matukio maalumu kama wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2009.

Shopping Cart