Utani kwa wadada wembamba
πππππππππππ
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii β¦β¦β¦mnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
π€£π€£π€£π€£
πππππππππππ
π€£π€£π€£π€£
Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.
Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.
Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.
Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:
Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution) . Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu?
Hivyo wito wetu kwako kuendelea kunywa maji mengi ya kutosha kadri uwezavyo hii itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwa na afya bora
Kuna wakati mwanaume huweza kupata maumivu ya korodani, ambapo inawezekana ikawa ni maumivu kwa korodani moja au zote mbili.
Maumivu hayo yanaweza kutokea endapo korodani zitakuwa zimeumizwa au kupata maambukizi.
Aidha, maambukizi hayo huweza kuwa makali na ya muda mfupi au makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe, lakini pia huweza kuwa ni maumivu ambayo siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayomnyima raha mhusika.
Mbali na hayo, pia maumivu ya korodani huweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa βFournierβs gangreneβ.
Kuna wakati mhusika anaweza kupata maumivu ya korodani mara inapotokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha mhusika kupata maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni.
Kimsingi maumivu ya korodani huchangiwa na vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takribani zaidi ya miezi mitatu.
Vilevile maumivu hayo yanaweza kusababishwa na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha ugumba.
Pia korodani inaweza kuwa na vivimbe kwa ndani, pembeni au juu ya kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi vinaweza kuwa na mishipa ya damu iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo kawaida, hivyo kuchangia mbegu za kiume kujikusanya na kushindwa kutoka na mengine ya kitaalam ambayo pia tutakuja kuyaona.
Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupindu. Inaripotiwa kuwa Kipingupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri jamii maskini zaidi kwa kiasi kikubwa hasa hasa kwenye nchi zinazoendelea, kiasi kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeuweka ugonjwa huu kama mojawapo ya viashiria vya maendeleo ya jamii husika.
Moja wapo ya changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea ni jamii kutokuwa na uhakika wa kupata Maji safi na salama, pamoja na kutokuwa na mazingira safi kwa ujumla. Ndio maana mpaka leo nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na mlipuko wa kipundupindu au huwa katika hatari ya mlipuko wa ugonjwa huo.
Ugonjwa huu hutokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu uletwao na vimelea vya bacteria vijulikanavyo kitaalamu kama Vibrio cholerae.
Kwa kawaida vimelea hawa hupendelea kuishi katika kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kunywa maji ama chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea hivi vya kipindupindu.
Mara baada kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa, baadhi ya vimelea hivi huuwawa kwa tindikali iliyopo kwenye tumbo (stomach) pindi chakula au maji haya yanapoingia tumboni. Hata hivyo baadhi ya vimelea hawa hufanikiwa kukwepa ukali wa hii tindikali na hivyo kuendelea kuishi.
Vimelea waliofanikiwa kuepukali tindikali ya tumbo la binadamu, hujongea kwenda kwenye ukuta wa utumbo mdogo kwa kutumia βmaumboβ maalum yaliyo kwenye miili ya ambayo huwawezesha kusafiri ama kwa kitaalamu huitwa flagella. Wawapo kwenye ukuta wa utumbo mdogo Vibrio cholerae hutoa sumu iitwayo CTX au CT (cholera Toxin) ambayo husababisha mtu kuharisha choo chenye majimaji, papo hapo kuendelea kutoa kizazi kingine cha vimelea hao nje kwa njia ya haja kubwa.
Iwapo choo hicho cha mtu aliyeambukizwa kipindupindu kitachanganyika na chanzo cha maji au chakula, watu wengine huambikzwa kirahisi. Hali kadhalika iwapo ni kwenye choo ambacho hakipo kwenye mazingira ya usafi kuna hatari ya choo cha mwambukizwa kuchanganyika na chanzo cha maji au chakula na hivyo kupelekea watu wengi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu.
β’ Kuanza Kuharisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho rangi yake ni kama maji ya mchele) na chenye harufu mbaya kama shombo ya samaki.
β’ Kutapika
β’ ngozi huwa kavu,
β’ midomo kukauka,
β’ mgonjwa kuhisi kiu kikali,
β’ machozi kutoweza kutoka,
β’ kupata mkojo kidogo sana,
β’ Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana.
β’ Macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto.
Kwa kawaida kipindupindu huweza kugunduliwa na kutambuliwa kwa kutumia dalili. Hata hivyo ili kuthibitisha kuwa mlipuko uliotokea ni kweli kipindupindu, vipimo vifuatavyo huweza kufanyika;
Kupima damu kwa ajili ya kuotesha vimelea vya kipindupindu maabara.
Kuchunguza choo kwa kutumia darubini (dark field microscope) ambapo vimelea hivi vya V. cholerae huweza kuonekana. Vile vile choo hiki hutumika kuotesha vimelea vya v. cholerae kwa ajili ya utambuzi zaidi.
Lengo kuu katika kutibu kipindupindu ni kurejesha maji na madini ambayo mgonjwa wa kipindupindu hupoteza kwa wingi baada ya kuharisha na kutapika.
Njia kuu zitumikazo katika kumrejeshea mgonjwa wa kipindupindu maji na madini aliyopoteza ni kwa kumpatia maji maalum yenye madini hayo kwa njia ya mdomo, yaani kwa kumpa anywe au kwa njia ya mshipa wa damu ambayo kitaalamu huitwa intravenously (i.v).
ORS
Pamoja na ORS hiyo ambayo imetengenezwa na kuwekwa kwenye paketi tayari kwa matumizi, Shirika la afya duniani (WHO) limetoa pia mwongozo wa kutengeneza maji yenye madini yanayohitajika mwilini (oral rehydration fluid) ambao ni rahisi na usio na gharama.
ORS ya kutengeneza nyumbani kwa kadiri ya muongozo huo huitaji kuchanganya na
β’ Lita moja ya maji safi na salama,
β’ Changanya na vijiko vidogo vinane vya sukari, kisha
β’ Ongeza na kijiko kidogo kimoja cha chumvi
β’ Aidha, unaweza kuongeza nusu glasi ya juice ya machungwa au nusu ya ndizi (tunda) lilipondwapondwa kwa kila lita, ili kuongeza madini ya potassium na pia kuboresha ladha.
Kwa wagonjwa wenye hali mbaya na wale wasioweza kunywa wenyewe, hupewa maji yenye madini mbambali kwa njia ya mshipa wa damu. Maji haya huitwa kitaalamu kama Ringerβs Lactate.
Baada wa mgonjwa kuwasili katika kituo cha afya, hupimwa kiwango cha upungufu wa maji kilichopo mwilini.
Kisha muhudumu wa afya husahihisha upungufu wowote wa maji utakaonekana kwa awamu mbili. Kwanza kwa kati ya masaa 4-6 ya kwanza tangu kuwasili kituoni na kuendelea mpaka hali ya kuishiwa kwa maji mwilini itakapoonekana imekwisha.
Mhudumu wa afya hutakiwa kurekodi kwenye cheti maalum kiasi cha maji anayokunywa mgonjwa na kiasi cha mojo anachokojoa.
Njia ya mshipa hutumika pale tu, hali ya mgonjwa inapokuwa mbaya sana au pale ambapo mgonjwa hawezi kunywa chochote mwenyewe. Aidha kiasi cha maji kitolewacho kwa njia hii ya mshipa wa damu hwa ni kati ya 50-100 mL kwa kilo za uzito wa mgonjwa kwa saa.
Baada ya hapo, mgonjwa huendelea kupewa ORS anywe kwa kiwango cha 800 mpaka lita moja kwa saa.
Ieleweke kuwa tiba sahihi na makini ya ugonjwa huu wa kipindupindu ni kumrejeshea mgonjwa maji na madini aliyopoteza wakati wa kuharisha na kutapika kwa njia ambazo zimeelezwa hapo juu. Matumizi ya dawa (antibayotiki) husaidia tu kufupisha muda wa kuwatoa wadudu na wala yasitumike kama tiba kuu ya ugonjwa huu.
Baadhi ya dawa ambazo hutumika katika matibabu ya ugonjwa huu ni Azithromycin na Tetracycline.
Mara kwa mara serikali na taasisi zake zimekuwa zikihimiza watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu wa kupindupindu. Miongoni mwa njia zinazofaa katika kuzuia milipuko ya ugonjwa huu ni
Upatikanaji wa maji safi na salama, watu hawana budi kuhakikisha kuwa maji ya kunywa yanachemshwa vyema kabla ya kuyanywa. Vile vile wanaweza kutumia chlorine katika maji ambayo huua vimelea hawa wa V. cholerae.
Ni muhimu kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula
Tunashauriwa kufunika chakula kikiwa mezani ili nzi wasitue juu yake
Inashauriwa kujenga choo umbali wa angalau mita 30 kutoka chanzo cha maji
Inashauriwa kwa wasafiri watokao nchi zilizoendelea kupata chanjo iitwayo Dukoral, pindi wanaposafiri kwenda nchi zinazoendelea.
Watu wengi hasa vijana watakuwa wanafahamu dawa ambazo hutumiwa sana kuzuia ujauzito pale ambapo wapenzi wamejamiiana ndani ya siku za hatari. Ninazungumzia dawa za kuzuia mimba sio dawa za kupanga uzazi. Dawa hizi zipo za aina nyingi ambazo zitozitaja hapa siku ya leo. Endapo wawili hawa wanakuwa hawapo tayari kupata mtoto, na wanaona kwamba siku walizojamiiana zitapelekea mwanamke huyo kutunga mimba, basi anaweza kutumia dawa hizi ambazo zinaharibu mazingira au uwezekano wa mimba kutungwa.
Dawa hizi zinaweza kutumika ndani ya saa 72 tangu mwanamke alipojamiina, lakini ikumbukwe kuwa, kadiri unavyozitumia mapema, ndivyo uwezekano wake wa kuzuia mimba unavyozidi kuwa mkubwa.
Licha ya kuwa watu wengi hutumia dawa hizi, ni wachache sana huchukua muda na kutaka kujua madhara yatokanayo na dawa hizo. Kwa ufupi tutaangalia madhara yanayoweza kutokana na dawa hizo. Hii haina maana kwamba, ukiitumia, basi ni lazima madhara haya yote yatakayojadiliwa hapa yakutokee, bali yanaweza kutokea baadhi au yasitokee kabisa.
Dawa hizi husababisha madhara kwa baadhi ya watumiaji. Miongoni mwa madhara ya kawaida ambayo husababisha ni pamoja na kupata maumivu ya tumbo, kuvurugika kwa mfumo wa hedhi, kutapika.
Unapotumia dawa hizi, mfumo wa hedhi katika mwezi unaofuata, hedhi inaweza kuanza mapema zaidi au kwa kuchelewa na damu inayotoka inaweza kuwa nzito ama nyepesi kuliko ilivyo kawaida.
Madhara haya ni ya muda mfupi tu, yanapita. Unapotapika ndani ya saa 3 baada ya kumeza dawa hizi, unashauriwa kuonana na mtaalamu wa afya au umeze tena dawa hizo.
Madhara mengine yanayoweza kutokana na dawa hizi ni maumivu ya kichwa, kuumwa na nyonga, maumivu ya mgongo na misuli.
Unapotumia dawa hizi na kuhisi maumivu makali, unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu. Pia unaweza kula chakula au kitu kingine ili kupunguza maumivu ya tumbo.
Bado hakuna ushahidi wa kitaalamu kuwa matumizi ya dawa hizi yanaweza kusababisha madhara ya muda mrefu kwenye afya ya uzazi ya mtumiaji. Aidha, unashauriwa kutozitumia mara kwa mara.
NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya namna mihogo mibichi na nazi kavu maarufu kama mbata vinavyoweza kuwasaidia watu kiafya, na hasa wanaume.
Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa ukihusisha mahojiano na baadhi ya madaktari na pia maandiko yatokanayo na tafiti mbalimbali, umebaini kuwa mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na kina mama jijini Dar es Salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha heshima kwa kina baba mbele ya wenzi wao kwa kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zinc na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambata cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.
βVyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya kina babaβ¦ vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarisha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenzi wao,β mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es Salam aliiambia Nipashe.
Ofisa Utafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni, alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitika kitaalamu kuwa husaidia kuiamrisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayopatikana, na hasa Zinc.
Alisema ni kwa sababu hiyo, anaamini ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa ni kina mama.
βKuna uvumi mwingi kuhusu faida za mihogo mibichi na nazi kavu kwa wanaume. Wengi huhusisha na masuala ya tendo la ndoaβ¦ukweli ni kwamba wanaozungumzia suala hilo wako sahihi ingawa wanaweza kuwa siyo wataalamu.
Vitu hivyo vina madini mengi yakiwamo ya Zinki ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume kwa mtu anayekula kwa usahihi na kwa muda mrefu,β alisema Mgeni.
Alisema zaidi ya kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume, mihogo mibichi na mbata vina faida nyingine nyingi mwilini mwa walaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha milango ya fahamu, kusaidia uponaji wa vidonda vya ndani na nje ya mwili, kutunza ngozi na kuilinda, nywele na pia kusaidia uponaji wa matatizo mengi ya macho.
MUUJIZA ZAIDI
Dokta John Kimai wa Kituo cha Afya cha Arafa kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam alisema ni kweli mihogo mibichi na nazi mbata husaidia kuiamrisha afya za walaji katika maeneo mengi ikiwamo via vya uzazi.
Aidha, alisema faida nyingine kiafya, hasa kwenye nazi mbata ni kuepusha matatizo ya moyo yatokanayo na wingi wa lehemu kwa kuwa nazi aina hiyo huwa na kiwango kikubwa cha kiambata kiitwacho βlauric acidβ.
Alisema faida nyingine ya nazi mbata ni kusaidia mlaji kuepukana na athari za kuvimbiwa, kuongeza nguvu za mwili kutokana na mafuta yake kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu (medium chain triglycerides β MCT) na hivyo huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu.
Aidha, kwa mujibu wa Dk. Kimai, mbata husaidia pia kuimarisha kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kutokana na uthibitisho wa tafiti mbalimbali kuthibitisha kuwa βlauric acidβ hubadilishwa kuwa acid inayojulikana kama βmonolaurinβ. Aidha, nazi kavu husaidia pia kuzisisimua seli na shughuli za ubongo na kwa kufanya hivyo husaidia kuzuia matatizo ya akili (dementia) na upotezaji wa kumbukumbu (Alzheimer).
Akielezea kuhusu faida za mihogo mibichi, daktari mwingine alisema kuwa ina madini mengi pia yakiwamo ya calcium, phosphorus, chuma na potassium ambayo kwa pamoja husaidia ukuaji wa tishu za mwili wa binadamu.
βKwa mfano, calcium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno kwa mwanadamu na hivyo mtu anayekula kwa wingi mihogo mibichi huimarisha meno yake na kuyafanya kuwa na nguvu,βalisema.
Katika mbata, baadhi ya virutubisho vingine vilivyomo ni Folates, Niacin, Pantothenic acid,
Pyridoxine, Riboflavin, Thiamin, Sodium na Copper
Vyakula vinavyofaa kuliwa wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaanza kuchambua kimoja baada ya kingine, Mbali na Waislamu, uchambuzi huu unawafaa pia wale ambao siyo Waislamu. Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Baada ya kushinda kutwa nzima na Swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena. Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi.
Mshuko wa sukari walioupata wale ambao hawakula au kunywa kwa kipindi kirefu, unaweza kusababisha ulegevu wa mwili.
Pindi sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha vyenyewe na kumfanya mtu aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho.
Ingawaje tende, mara nyingi, si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari.
Nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwa ajili ya glukosi pekee. Usambazaji wa haraka-haraka wa glukosi itokayo kwenye tende huusaidia mwili kuodokana upesi na hali ya ulegevu kiasi kwamba mtu aliyefunga huweza kujimudu sawasawa katika ibada.
Mbali ya glukosi, tende pia ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi ambazo huwezesha michakato ya umengβenyaji mwilini kuendelea, na huzuia tatizo la kushindikana kwa michakato hiyo ya uyeyushaji wa chakula mwilini.
Vilevile tende ni chanzo kizuri cha potasiamu, madini ambayo ni muhimu kwa usawazishaji wa maji mwilini. Hivyo, wale ambao hawapendelei ladha ya tende wanaweza kupata manufaa ya chakula hiki kwa kula angalau tende moja, na wale wanaopendelea tende, basi wanaweza kula tatu, tano, na kadhalika.
Mwili wa binadamu, kwa kiasi kikubwa, unajengwa na maji. Faida za maji ni kubwa. Kama unavyohijati sukari kujirudishia nishati upesi, ndivyo unavyohitaji maji kujijazilizia ili uweze kufanya kazi vizuri.
Siyo tu maji huurudishia mwili maji upesi na kukata kiu, bali pia ni kisafishio asilia cha uchafu na sumu ambazo zimejilimbikiza kwa muda fulani.Kwa kutwa nzima, mtu mzima mwenye afya nzuri, hushauriwa kunywa jumla ya vikombe vinane vya maji.
Hii haijumuishi yale maji yatokanayo na vyakula kama vile matunda na mbogamboga.
Kwa vile mtu aliyefunga huwa hanywi maji muda wote wa swaumu yake, basi naye anahitajika kufikisha kiwango hicho cha unywaji wa maji kabla ya daku na baada ya futari.
Inapendekezwa hivi, kwamba mwanzoni mwa kufuturu, mtu anywe kiasi kidogo cha maji (nusu kikombe au kikombe kimoja), na baada ya kufuturu, anywe maji kwa viwango vidogo muda baada ya muda (mathalani nusu kikombe au kikombe kimoja kila baada ya saa moja).
Hii itaepusha ujazo mkubwa wa maji tumboni kwa wakati mmoja na itarejesha maji mwilini kidogokidogo kabla ya swaumu inayofuata
Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (mishipa ya fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi kutokana na mifupa (vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.
Mgongo wazi(spinal bifida) inaweza pata watoto 3 kati ya watoto 10000 wanaozaliwa.
Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa, ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.
Kuna sababu mbalimbali zinapelekea uti wa mgongo kutoziba, ambazo zinaweza zuhilika, nazo ni Upungufu wa folic acid(vit B9) na vitamin B12 katika kipindi cha ujauzito, katika kipindi cha miezi ya awali.
Mama mjamzito kupiga X-ray, mattumizi ya dawa za kifafa katika kipindi cha ujauzito .
Pamoja na maambukizi ya baadhi ya virusi kwa mama mjamzito.
Zipo aina mbiliza tatizo la tundu katika mgongo ama mgongo wazi
Aina ya kwanza ni occultaΒ ambapo huwa na aina mbili pia, aina ya kwanza ni ile ambapo panakuwa na vinyweleo tu vinavyoonekana nyuma chini ya mgongo bila kuwa na dalili zozote zile, ama kunaweza kujitokeza kwa kuta zinazofunika mishipa ya fahamu tu.
Aina ya pili ni ni cysticaΒ ambapo panakuwa na vifuko vinavyofunika mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya kuchomoza katika tundu la mgongoni.
Aina hii ni mbaya zaidi kwani linaweza kusababisha mtoto asitembee ama asiweze kuzuia haja kubwa na ndogo.
Dalili huwa kama zifuatazo
Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo.
Kuwa na vinyweleo sehemu za chini za mgongo bila kuwa na tatizo la mishipa ya fahamu
Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu
Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa ama ndogo endapo mishipa yote ya fahamu imepita katika tundu hilo.
Na dalili zingine zinazoambatana kuharibika kwa mishipa.
Upasuaji
Upasuaji ni tiba pekee ya uti wa mgongo ulio wazi(spinal bifida) inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu(neurosurgeons) wanachofanya ni kuziba lile tundu lililowazi.
Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B na folic acid inavyopaswa, vyakula hivyo ni matunda,mboga za majani, mbaazi na choroko.
Mwanamke mjamzito akipata lishe yenye virutubisho hivyo pamoja na kunywa vidonge vya folic acid, kwa asilimia 30% inaweza kupunguza hatarishi ya kupata watoto wenye uti wa mgongo ulio wazi.
Pia kwa wanawake wajawazito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanashauriwa kutokupiga X-ray.Inawezekana mwanamke akawa hatambui kama ni mjamzito,kipimo cha mkojo cha ujauzito(UPT-urinary pregnancy test) kifanyike kwa haraka kama mwanamke haelewi vizuri mzunguko wake wa hedhi kabla hajapiga X-ray ikiwa ana tatizo lingine la kiafya,
Mwanamke mwenye kifafa akiwa mjamzoto pia yupo kwenye matibabu, awahi haraka kwa daktari kushauriana ni nini zaidi cha kufanya ili kumsaidia.
Wanawake wajawazito wanashauriwa kuhudhulia kliniki mapema zaidi ili wapate elimu ya lishe na kuweza kuanza mapema kutumia folic acid kama kinga ya Mgongo wazi.
Jamii inapaswa kujua kuwa Mgongo wazi(Spinal bifida) haitokani na mambo ya kishirikina bali ni hali ambayo inaweza kuzuilika. Mzazi yeyote mwenye mtoto mwenye Mgongo wazi anashauriwa ampeleke mtoto wake hospitali ili apate maelekezo ni wapi mtoto anaweza kupata matibabu ya upasuaji.)
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Β· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
Β· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
Β· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
Β· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
Β· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
Β· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
Β· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
Β· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
Β· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzito ila mara nyingi hutokea katika umri wa mimba kuanzia miezi mitatu.
Kiungulia ni maumivu mithili ya moto yanayotokea kifuani sehemu ya katikat ya kifua. Maumivu haya hayana uhusiano na moyo.Yanatokea pale asidi ya kwenye tumbo inapopanda na kurudi kwenye koo la chakula.
Asidi hii ikiwa tumboni haisababishi madhara wala maumivu kwani inazalishwa muda wote na kuta za tumbo kumeng’enya chakula. Seli za kuta za tumbo haziathiriki na asidi hii ndio maana inapokuwa tumboni haileti shida yoyote.
Ila seli za kuta za koo la chakula haziwez kustahimili asidi hii ndiyo maana inapopanda kwenye koo la chakula unapata maumivu ya kiungulia.
Kiungulia mara nyingi hutokea wakati unakula au baada ya kula na kinaweza kuzidi makali wakati umelala.
Dalili ni kama, Kuhisi maumivu kama ya kuungua kwenye kifua au chembe moyopamoja na kujisikia radha ya uchachu mdomoni.
Sehemu mbali mbali za mwili hupata mabadiliko wakati wa ujauzito. Wakati wa ujauzito mwili hutengeneza kwa wingi hormone ya progesterone na relaxin ambazo huathiri mfumo wa chakula.
Progesterone hormone hii hufanya chakula kutembea na kufyonzwa kwa taratibu sana.
Relaxin hormone hufanya misuli laini ya mwili kulegea ikiwemo misuli inayobana sehemu ya juu ya tumbo (sphincter) inayozuia chakula au vitu vya tumboni visirudi kwenye koo la chakula .
Mabadiliko haya hufanya kuwa rahisi asidi na chakula vilivyomo tumboni kurudi kwenye koo la chakula na kusababisha kiungulia.
Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Tatizo hili limewakumba wanaume wengi walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta utatuzi kwani tatizo hili huwafanya kuwa na wasiwasi wa maisha. Ndoa nyingi zimevunjika na mahusiano kuharibika kwa sababu ya tatizo hili.
Kwa wanaume wenye umri mkubwa, upungufu wa nguvu za kiume unaweza usiwe ni tatizo kwani miili yao inakuwa tayari imechoka.
Hizi hapa ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kurudisha nguvu za kiume zilizokuwa zimepotea, au kuimarisha uwezo wako wa tendo la ndoa.
Tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini inakunyima uwezo wa kufanya tendo hilo, kwani hupunguza kiwango cha maji mwilini.
Watu wengi wameelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupatishi damu ya kutosha kwenda sehemu mbali mbali kama vile ubongo, ini na figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake. Uume ili usimame kwa uimara, unatakiwa upate damu ya kutosha.
Kufanya mazoezi hupunguza kiwango cha mafuta katika mishipa ya damu na kuiwezesha kupeleka damu ya kutosha katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo uume.
Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi kwani ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. Kula vyakula asili na nafaka ambayo haijakobolewa, kula matunda kwa wingi pamoja na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utakuwa imara katika tendo la ndoa.
Ufanyaji wa tendo la ndoa huwa unahusisha mambo mengi. Unaweza ukawa umekamilika kiafya lakini ukashindwa kufanya mapenzi kwa kuwa una msongo wa mawazo. Hakikisha kabla ya kwenda faragha na mpenzi wako, unauituliza akili na usiwaze mambo mengine nje ya tendo linaloenda kufanyika. Hii itakupa muda mzuri wa ubongo wako kupeleka damu ya kutosha katika uume.
Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki, chuma, selenium, manganese na vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki. Madni haya huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako. Madini haya hupatikana katika mboga, samaki na matunda ya aina mbalimbali.
Kunywa maji ya kutosha kila siku, usingoje mpaka kiu ikupate. Mtu mzima anapaswa kunywa maji glass 8 mpaka 10 kwa siku. Maji husaidia kuongeza kiwango cha damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini.
Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti.
Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.
Watu wengi hufikiri kuwa kula mboga za majani ni umaskini; lakini ukweli ni kuwa mboga za majani zina manufaa makubwa kwenye miili yetu. Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri.
Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).
Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.
Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.
Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.
Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.
Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.
Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.
Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.
Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki tendo, Maumivu haya yaweza kuwa;- Wakati tu uume unaingia,
Unapoingiza kitu chochote hata kidole, Wakati uume ukiwa ndani na Maumivu ya kupita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.
Sababu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.
Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango.
Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.
Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano βvaginal agenesis na imperforate hymen.β
Msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.
Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba. Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.
Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume.
Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini.
Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya βprolactineβ.
Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.
Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni βProlactinβ, Estrogenβ na Progesterone.
Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.
Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu na wasiwasi au shauku fβlani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.
Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya βpituitary au pituitary adenomaβ.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile βCimetidineβ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili.
Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.
Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo.
Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu.
Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary.
Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa.
Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi.
Hypotension ndio jina linalotumika kuelezea presha ya kushuka ambayo mpaka sasa chanzo chake hakijawa wazi. Kipimo cha presha huwa na namba mbili. Namba moja huwa juu na nyengine huwa chini. Hivyo basi namba ya juu kikawaida kwa mtu mzima inapaswa kuwa 100 hadi 139 na ya chini inapaswa kuwa 60 hadi 90. Hivyo basi pressure yako ikiwa chini ya 100/60 Ndio inajulikana kama Hyptension yaani pressure iko chini.
Hypotension (haipo juu). Kwa watu wengi presha hii huwatia kizunguzungu na kuwaangusha. Presha hii ikiwa ya muda mrefu husababisha mtu kupata maradhi ya mshtuko.Watu wenye afya nzuri, hasa wakimbiaji, presha ya kushuka huwa ni dalili ya uzima kwao.
Si rahisi kuziona dalili kwa mtu mwenye presha ya kushuka hata kama imedumu kwa muda mrefu. Mara nyingi matatizo ya kiafya huonekana pale mtu presha yake inaposhuka ghafla. Wakati huo wa matatizo ya kiafya, damu kidogo hufika katika ubongo. Hali hii humfanya mtu awe na kizunguzungu au kuumwa na kichwa.
Kushuka ghafla kwa presha mara nyingi humtokezea mtu pale anapofanya jambo la haraka kama mtu aliyekaa na kutaka kusimama mara moja. Kitaalamu presha hii inajulikana kama postural hypotension, orthostatic hypotension, au neurally mediated orthostatic hypotension.
Postural hypotension inachukuliwa ni hali ile ya kushindwa kwa mfumo wa mawasilianao unaojiendesha wenyewe mwilini kufanya kazi yake kikamilifu (autonomic nervous system). Mfumo huu huendesha na kuongoza vitendo visivyo vya hiari (involuntary vital actions), kama vile mapigo ya moyo kubadilika kutokana na jambo lililotokea kwa wakati uleopo.
Kwa kawaida unapoinuka, kiwango fulani cha damu yako kinakuwa kimebaki sehemu ya chini (miguuni). Kukiwa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na mwili wako, hali hii itasababisha presha yako kushuka. Katika hali hii mwili wako unafanya nini ?
Mwili wako unapeleka taarifa kwenye moyo na kuamuru uongeze usukumaji wa damu ambao utaizidi mishipa yako na kuifanya kuwa membamba hali itakayopelekea kuifanya presha yako kubakia ileile. Ikiwa jambo hili halikufanyika au limaefanyika polepole sana, presha yako itashuka ghafla. Hapa ndipo mtu unapomuona anaguka ghafla.
Kwa ufupi athari ya maradhi ya presha ya kushuka na ya juu huongezeka kadri mtu anapokuwa na umri mkubwa na pia kubadilikabadilika kadri umri unavyoongezeka. Jambo jingine la kufahamu ni kuwa, ufikaji wa damu kikawaida kwenye ubungo unapungua kadri umri unavyoongezeka. Inakisiwa kiasi cha asilimia 10 mpaka 20 ya watu wenye umri unaozidi miaka 65, wanapata tatizo la presha yao kushuka.
Hakuna kiwango maalum kinachojulikana ambacho ni sawasawa kwa watu wote kikifika ndio kinaitwa maradhi. Kiwango ambacho kwako ndio uzima, basi huenda kwa mwenzako ikawa ni maradhi. Katika presha ya kushuka, madaktari wengi huchukulia kuwa tayari mtu ana maradhi pale aambapo kiwango chake cha presha kinafuatana na dali za maradhi yenyewe.
Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wanachukulia tayari mtu ana maradhi ya presha ya kushika pale vipimo vinapoonyesha kiwango hichi 90/60 mm Hg. Tufahamu kuwa kiwango cha namba inayosomwa chini katika kipimo cha presha (β¦ /60 mm Hg ), hichi huonyesha tayari mtu huyu anapresha ya chini hata kama kile cha juu ( 90/β¦mm Hg) kina namba iliyozidi 100.
Mfano ikiwa umepimwa presha na ukapata kipimo hichi 115/60 mm Hg, presha yako itakuwa ipo chini. Na kama umepata kipimo hichi 115/50 mm Hg, sio kwamba presha yako itakuwa ipo chini tu, bali presha hii itakuwa si ya kawaida.
Kama nilivyokwisha tangulia kusema, presha inaweza kuwa sawa kati ya watu wawili lakini ikawa na matokeo tofauti. Presha hiyo inayoweza kuwa sawa na ikawa na matokeo tofauti si yenye kipimo hichi 120/80 mm Hg. Presha yenye kipimo hichi 120/80 mm Hg, ndiyo nzuri na watu wenye presha hii wanakuwa na afya nzuri. Kitu muhimu ni kujua, mabadiliko gani yanaleta tatizo katika presha hata inapelekea kuwa si ya kawaida.
Presha nyingi za watu wanapopimwa huwa zinakuwa kati ya 90/60 mm Hg (presha iliyo chini) mpaka 130/80 mm Hg (presha iliyo juu). Mabadiliko ya kushuka presha upande wa chini, hata kama kidogo kiasi cha 20 mm Hg, hupelekea matatizo kwa baadhi ya watu ( hasa watu wasiofanya mazoezi kila siku).
Mtu mwenye mazoezi ambaye presha yake nzuri (120/80 mm Hg) akapimwa presha na kupata kipimo hichi, 110/60 mm au 120/70 mm Hg, mtu huyu hatakuwa na tatizo lolote la presha
Kuna aina tatu za presha ya kushuka :
Orthostatic sambamba na postprandial orthostatic (Orthostatic hypotension, including postprandial orthostatic hypotension)
Orthostatic, hii ni aina ya kwanza ya presha inayosababishwa na kubadili mazingira uliyonayo kwa ghafla, maranyingi hutokea kwa mtu anayesimama kutoka alipolala. Presha hii haidumu muda mrefu, kiasi cha sekunde chache mpaka dakika moja. Ikiwa presha hii itatokeze. baada ya kula, basi itakuwa ni hatua ya pili (postprandial orthostatic) .
Hatua hii ya pili huwapata zaidi wazee na wenye presha ya juu.
Neurally mediated hypotension (NMH)
NMH kama ilivyo kifupisho cha presha aina ya pili, huwapata zaidi vijana na watoto. Presha hii hutokea pale mtu anaposimama kwa muda mrefu. Maranyingi huwapata sana watoto.
Mambo mengine yanayosababisha presha kushuka ni pamoja na :
Severe hypotension hii ni aina ya tatu ya presha ya kushuka ambayo hutokana na kupoteza damu
Kwa muhtasari, dalili za presha ya kushuka ni pamoja na :
Kinachosababisha presha ya chini bado hakijatambulika hasa. Chanzo chake hakiko wazi. Hata hivyo mambo yafuatayo yanaweza kuhusiswa nayo :
Presha ya kushuka ghafla inayompata mtu anapoinuka ghafla, inaweza kumpata mtu yeyote kwa sababu tofauti zikiwemo,
Pia Presha ya kushuka mara nyingi huwapata watu wanaotumia dawa kwa kutibu presha ya juu (hypertension). Pia huwapata wajawazito au wagonjwa wa kisukari. Mara nyingi wazee nao hupata maradhi haya hasa wale walio na presha ya juu wakiwa wanaendelea kutumia dawa zao za presha.
Baadhi ya maradhi ambayo yanasababisha presha kushuka kuendelea ni pamoja na;
Matibabu huanza na hatua zako wewe mwenyewe. Wakati utakapojiona presha yako inashuka, kaa chini au lala chali na unyanyue miguu yako juu. Wakati yanafanyika haya, ufanyike utaratibu wa kuonana na daktari haraka.
Pia ufanyike utaratibu wa kuonana na daktari yanapoonekana mambo yafuatayo yamemkuta mtu :
Pia afuatwe daktari haraka ikiwa baada ya hayo yaliyotokea, kuongezeka na haya yafuatayo :
Presha ya kushuka ambayo haijulikani chanzo chake wala haileti dalili au inampa mtu kizunguzungu anaposimama, mara chache inaweza kutafutiwa matibabu. Ikiwa zipo dalili, matibabu yataendana na chanzo chenyewe na daktari atashughulikia hicho chanzo. ( kuharisha,maradhi ya moyo, kisukari). Ikiwa presha ya chini imesababishwa na matumizi ya dawa kwa matibabu, basi matibabu yake huwa kubadili dawa nyingine ua kuacha kutumia dawa kabisa.
Ikiwa hakuna uhakika wa sababu za presha ya kushuka au hayapatikani matibabu yaliyo sahihi, matibabu sahihi yatakuwa ni kuifanya presha yako ipande na kuondoa zile dalili zanazokupata inapokujia.
Kwa kutegemea umri wako, hali yako ya kiafya na aina ya presha uliyonayo, mambo haya yanaweza kukusaidia :
Kuongeza matumizi ya chumvi. Matumizi ya chumvi lazima yawe kwa kipimo, kwani chumvi nyingi hupandisha presha. Kabla hujaanza kuongeza matumizi ya chumvi, ni vizuri uwasiliane na daktari ili akupe kiwango cha matumizi.
Kunywa maji mengi. Kunywa maji mengi kunamsaidia kila mtu sio mtu mwenye presha ya chini tu. Tunapozungumzia maji tunalenga zaidi vinywaji na sio maji peke yake, lakini vinywaji vyenyewe viwe ni maji, maji ya matunda maziwa na hata kahawa au chai. Tahadhari ichukuliwe kwa vinywaji vya viwandani kwani huwaletea matatizo baadhi ya watu.
Kuvaa mavazi yenye kubana. Haya ni mavazi ya mpira ambayo yanavaliwa sehemu za miguuni. Mavazi haya yanasaidia kufanya damu yako isikae miguuni na iendelee kwenye mzonguko wake kikawaida.
Matumizi ya dawa. Zipo dawa mbalimbali ambazo zinatumika kufuatana na hali ya presha uliyonayo.
Presha ya kushuka inayomtokezea mtu mwenye afya nzuri ambayo haina dalili zozote na haimletei matatizo yeyote, hatahitajika kutumia dawa. Ikiwa zipo dalili, atahitaji matibabu kutokana na hizo dalili zilizoonekana. Ikiwa presha ulokuwa nayo inatokana na matumizi ya dawa, daktari atakubadilishia dawa nyengine au utaacha matumizi ya dawa. Wale wenye NMH pamoja na matumizi ya dawa, inabidi waache tabia ya kusimama muda mrefu. Kimtazamo presha ya chini inatibika hata kufikia mtu kuwa na presha ya kawaida.
Napenda nichukue nafasi hii kuwafahamisha kuwa, bila kubadili mfumo wa maisha ulionao, hata ukikusanyiwa dawa nzuri za dunia nzima kwa kutibu maradhi yako hutopata uzima wowote. Kubadili mfumo wa maisha si katika kuishughulikia presha tu, bali kwa maradhi yote ndio
Tiba sahihi. Nini dawa zinafanya?. Dawa zinalazimisha kuurudisha mfumo katika hali yake ya kawaida tu. Baada ya dawa kutoa msaada wake huu, kinachotakiwa kwako wewe kuendeleza mfumo huo unaofaa ambao dawa zimekurudishia tena.
Kwa kutegemea sababu za kupata presha uliyonayo, unaweza kuchukua hatua zifuatazo :
Kunywa maji mengi, kuacha kunywa pombe, Kula vyakula kiafya (kula nafaka, matunda, mbogamboga, kula mifupa ya samaki na hata ya ndege[kuku,njiwa nk]) Tupendelee kuku wa kienyeji zaidi. Ikiwa kuongeza chumvi katika chakula, basi usizidishe vijiko viwili vya chai kwa siku na ni vizuri sana upate ushauri kwa daktari.
Kujenga utamaduni wa kuinuka taratibu ulipo kaa ua kulala. kulalia mto, ikiwa unapenda kunalalia ubavu, pendelea kulalia upande wa kulia (kila unapozungumzia presha, basi jambo la kwanza la kukumbuka ni moyo, moyo wako uko upande wa kushoto, kitendo cha kulalia upande wa kushoto kinaweza kuupa tabu moyo katika utendaji wake wa kazi).
Kuwa na tabia ya kula chakula kidogo katika mlo wako. Kufanya hivyo kunasaidia presha yako kutoshuka baada ya kumaliza kula. Jipangie utaratibu wa kula mara kwa mara ili uweze kula chakula cha kutosha. Punguza kula vyakula vyenye uwanga kwa wingi kama vile, mbatata, wali na mikate. Kula chakula pamoja na chai au kahawa. Ni vizuri haya yote utakayoyafanya ukawasiliana na daktari kabla.
Ikiwa wewe ni mzima au tayari una presha ya kushuka, Daktari atakushauri hatua za kuzuia isitokee au isiendelee au kuipunguza. Hatua hizo ni pamoja na :
1. Kuacha unywaji wa pombe.
2. Kuepuka kusimama muda mrefu ( hasa ikiwa tayari una NMH)
3. Kunywa maji kwa wingi
4. Kuinuka taratibu kutoka ulipokaa ua kulala
5. Kuvaa mavazi ya kubana miguuni (ikiwa tayari unayo)
Mrija wa mkojo (urethra) ni kiungo muhimu kinachotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu. Mrija huu unaposinyaa au kuziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa
mashaka na maumivu makubwa. Kusinyaa/ Kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa pia
urethral stricture.
Kusinyaa kwa mrija wa mkojo husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya
mrija baada ya mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa.
Inaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu na eneo la kinena unaokandamiza mrija.
Vihatarishi vya tatizo hili ni pamoja na
Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya zinaa
kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya namna hiyo (catheter au
cystoscope)
sana kwa wale wanaopata ajali wakiendesha baiskeli
mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo hili (congenital urethral stricture).
Daktari atakufanyia uchunguzi wa mwili na namna unavyokojoa. Uchunguzi wa mwili
unaweza kuonesha:
residual (PVR) volume)
Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo
mojawapo ya tiba. Iwapo njia ya kutanua mrija haioneshi mafanikio sana, upasuaji
unaweza kuhitajika. Upasuaji unategemea eneo lilipo tatizo na ukubwa wa tatizo.
Kama tatizo ni dogo/fupi na lipo mbali na bawabu inayotenganisha mrija na kibofu cha mkojo,
linaweza kutatuliwa kwa kukata kasehemu kalikoziba wakati wa kufanya cystoscopy au
kwa kuweka kifaa maalum cha kuzibua na kutanua mrija.
Kama tatizo ni kubwa zaidi, upasuaji wa wazi wa eneo husika unaweza kufanyika.
Upasuaji huu unajumisha kukata sehemu iliyoziba na kisha kukarabati sehemu hiyo.
Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa kutoa mkojo (acute
retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea catheter kupitia juu ya kinena
(suprapubic catherization) hufanyika. Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye
bomba lililowekwa chini ya tumbo.
Ifahamike kuwa mpaka sasa hakuna dawa ya tatizo hili zaidi ya njia za upasuaji na
nyingine zilizoelezwa hapo juu.
Mara nyingi matibabu huleta matokeo mazuri na mgonjwa anaweza kuishi maisha yake
kama kawaida. Hata hivyo wakati mwingine, mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu ya
mara kwa mara ili kuondoa sehemu ya kovu iliyopo katika mrija wa mkojo.
Tatizo hili halina budi kutibiwa haraka maana kama likiachwa linaweza kusababisha
kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali
ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo
kushindwa kufanya kazi (ARF).
Kinga
Ni muhimu kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kwa kufanya ngono salama au kuacha
kabisa kufanya ngono. Aidha kuwa makini na kazi au mambo ambayo yanaweza
kukusababishia kuumia maeneo ya kinena.
Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, βPotassiumβ, βMagnesiumβ na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction).
Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
Tikitimaji lina kirutubisho aina ya βarginineβ, ambacho huchochea uzalishaji wa βnitric oxideβ kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa ya Viagra.
Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya βPotassiumβ kama vile Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.
Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji.
Kirutubisho cha βarginineβ kilichomo kwenye Tikitimaji mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili.
Kuondoa βammoniaβ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
Tunda hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.
Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika dunia, watu wamekuwa wakiteseka bila kujua nini chanzo cha tatizo hili na vipi kuliondoa tatizo hili na wengine wamekuwa wakilipuuzia bila kujua madhara ambayo wanaweza kuyapata kutokana na tatizo hili.
Tatizo hili hutokea pale mtu anakula vizuri lakini unakata siku tatu hadi nne bila kupata choo. Ukiona unakula kutwa mara tatu na unakaa siku mbili hadi tatu huendi chooni au unatoa choo kigumu kama mbuzi hilo ni tatizo kwako.
Tafiti zinaonyesha mtu anaweza kupoteza maisha kama atakosa choo kwa siku tano hadi saba mfululizo.Watu wengi hulidharau tatizo hili lakini linamadhara makubwa tofauti na wanavyofikiria.
Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita 9 hadi 18 na huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka 6 na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50.
Lakini pia tunda la shelisheli ni zao kuu maeneo ya Pasifiki na lina kiwango kikubwa cha wanga na huweza kuliwa likiwa bichi au baada ya kupikwa.
Tunda hili lina faida mbalimbali zikiwemo za kiafya na za kiuchumi, lakini moja ya sifa kuu ya tunda hili ni kuwa na kiwango kizuri cha wanga.
Kutokana na kiwango kikubwa cha wanga kwenye shelisheli kunalifanya tunda hilo kutumika badala ya unga wa ngano kwenye baadhi ya nchi na hivyo hutengenezewa chapati.
Aidha, utomvu wake unaelezwa kutumika kama njia asili ya kupunguza matatizo ya kuhara na magonjwa ya ngozi.
Hivyo basi kwa kuzingatia na kujali afya yako unashauriwa kuweza kutumia tunda hili ili uweze kuifanya ngozi yako iwe nyororo lakini pia uweze kujitibu matatizo yote yatokanayo na kuhara.
Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.
Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya;
Vyoo vichafu.
Kuchangia nguo za ndani na taulo.
Uwezekano wa kupata fangasi ya uke au fangasi ya uke kujirudia rudia unaongezeka pale ambapo mwanamke ana;
Kisukari.
Ujauzito.
Anatumia antibiotics kwa muda mrefu
Ukimwi.
Joto, unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu haumbukizwi kwa njia ya ngono.
Fangasi ya ukeni inaweza kuleta dalili zifuatazo kwa wagonjwa wenye maambukizi;
Kuwashwa sehemu za siri hasa wenye uke na mashavu ya uke.
Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya.
Maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisabaishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.
Matibabu ya fangasi ya uke hutumia dawa za kuua fangasi (antifungals). Mara nyingi dawa za kuingiza kwenye uke (vaginal pessaries) hutumika kwa muda wa siku 3 mpaka 6. Wakati mwingine dawa za kunywa zinaweza kutumika kutibu fangasi hii.
Muone daktari kwa ajili ya uchunguzi, dawa na dozi sahihi.Cotrimazole na ketoconazole ni kati ya dawa zinazotumika mara kwa mara.
Pamoja na matibabu kuna hatari ya maambukizi ya fangasi hawa kujirudia, hivyo ni muhimu kupata tiba hospitali na kurudi unapoona inajirudia. Vitu vingine muhimu kuzingatia ni;
Usafi wa nguo za ndani; kuvaa safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).
Vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.
Vaa nguo za ndani zilizotengezwa kwa pamba (hupunguza joto na hivyo hatari ya fangasi kuzaliana)
Usafi wa sehemu za siri na kujikausha viruzi baada ya kuoga.
Usafi wa choo ni muhimu sana.
Recent Comments