Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku

Featured Image

Viambaupishi

Mchele wa basmati - 3 vikombe

Kuku - ½

Bilingani - 2 ya kiasi

Viazi - 4

Vitunguu - 2

Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 2

Chumvi - kiasi

Garama masala (mchanganyiko wa bizari) - 1 kijiko cha chai

Hiliki ya unga - ¼ kijiko cha chai

Mafuta ya kupikia wali - ¼ kikombe

Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
Kata kuku vipande upendavyo safisha
Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala).
Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
Menya na kata viazi kaanga weka kando.
Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando.
Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo.
Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa.
Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive.
Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mapishi ya wali wa mboga

Mapishi ya wali wa mboga

Mahitaji

Wali uliopikwa (cooked rice) kiasi
Hoho la kijani (green pepper) 1/2
H... Read More

Upishi na Karanga na Mbegu: Vyakula vya Virutubishi

Upishi na Karanga na Mbegu: Vyakula vya Virutubishi

Upishi wa vyakula vya virutubishi kama vile karanga na mbegu ni muhimu sana kwa afya yetu. Kwa ba... Read More

Jinsi ya kupika Donati

Jinsi ya kupika Donati

Viamba upishi

Unga
2 Magi (kikombe kibuwa cha chai)

Sukari
1/3 Kikombe ch... Read More

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu Lishe

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu Lishe

Nini maana ya lishe?

• Lishe yahusu mafunzo ya chakula na jinsi miili ... Read More

Mapishi ya Mandazi ya nazi

Mapishi ya Mandazi ya nazi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour) vikombe 2 na1/2
Sukari (sugar) 1/2 kikombe... Read More

Mapishi ya Ndizi Mbichi Za Nyama Ng'ombe

Mapishi ya Ndizi Mbichi Za Nyama Ng'ombe

Vipimo

Ndizi mbichi - 10

Nyama - kilo 1

Nazi ya kopo - 1

Chumvi - 1 Kij... Read More

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unak... Read More

Mapishi ya Viazi vitamu na kachumbari

Mapishi ya Viazi vitamu na kachumbari

Mahitaji

Viazi utamu 3
Nyanya 2 kubwa
Kitunguu
Tango
Limao
Chumv... Read More

Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe

Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe

Vipimo - Mahitaji Ya Nyama

Nyama ya n’gombe ya mifupa - 3 lb

Tangawizi mbichi il... Read More

Jinsi ya kupika Wali Wa Karoti Na Nyama

Jinsi ya kupika Wali Wa Karoti Na Nyama

Viambaupishi: Wali

Mchele 3 Magi

Mafuta 1/4 kikombe

Karoti unakata refu refu ... Read More

Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

Viambaupishi

Mchele (Basmati) 3 vikombe Nyama ya ngo’mbe 1 kg Pilipili boga 1 kubw... Read More
Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Viambaupishi

  1. Mchele (Basmati) - 3 vikombe
  2. Mbogamboga za barafu (karot, njege... Read More