Updated at: 2024-05-25 18:11:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hii ndio Bongo
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.
MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi….kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .
BINTI: Mi naitaka hii
MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako…
Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.
MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.
Updated at: 2024-05-25 17:03:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallah…!! sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!! Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu.. Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza
Zuzu: Mambo Anna! Anna: Poa! Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyeshe… Anna: Kitu gan? Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda) Anna: Haya nionyeshe…
Updated at: 2024-05-25 18:07:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Zuzu: Mambo Anna! Anna: Poa! Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyeshe… Anna: Kitu gan? Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda) Anna: Haya nionyeshe…
Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga) Anna: Haya nionyeshe sasa!.. Zuzu: Zima taa kwanza (akazima) Anna: Mhm…nionyeshe sasa! Zuzu: Haya njoo hapa kitandani… Anna: Ok, nionyeshe! Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizani… Acha mawazo mabaya ww???
Mke anamwambia mme wake kuwa angetamani mme wake awe tajiri cheki alichojibiwa
Updated at: 2024-05-25 17:03:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mke; mme wangu ungekuwa tajiri ningefurahi Mimi; kwa nini? Mke; ungekuta na sisi tuna gari nzuri hatutembeu kwa mguu Mimi; ah wap,unadhani ningekuwa tajiri ningekuwa na wewe?ungekuta natoka na kina wema,zari… 😁😁😁 naona anakusanya nguo zake itakuwa anaenda kufua