Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula
Updated at: 2024-05-25 10:35:16 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyakula kama ugali,wali,mkate mweupe,bia na pombe za kienyeji zinazotokana na wanga (kimea) huchangia kuongezeka kwa uzito. Matumizi ya aina hii ya chakula ni muhimu kupunguzwa katika mlo wako.
Sukari inayozidi mwilini toka katika vyakula hubadilishwa na kuwa mafuta. Vyakula kama chokuleti,biskuti,keki na vinyaji kama soda vina kiwango kikubwa cha sukari. Pia usitumie sukari nyingi katika chai na juisi.
Mboga mboga ni nzuri kwa afya kwa ujumla lakini pia haina mafuta hivyo itakufanya kuingiza mafuta kidogo mwilini.
Umesikia kuhusu chai ya kijani (Green Tea), ni chai ambayo ni ya kijani na inasaidia kuondoa sumu za mwili (antioxadation). Hii inasaidia katika kusaidia mwili kuunguza mafuta katika njia inayoitwa thermogenesis.
Tangawizi kama ilivyo chai ya kijani inafahamika kuongeza mmengâenyo wa chakula tumboni hivyo kupunguza mrundikano wa mafuta yasiyotumika
Maji yanachangia kuharakisha mfumo wa uvunjaji chakula tumboni na hivyo kupunguza mafuta yanayohifadhiwa.
Matunda halikadharika hayapunguzi uzito moja kwa moja bali yatakufanya ushibe na usitamani kula kila mara kwani yanakata hamu ya chakula. Hivyo utaokoka na tabia ya kula kila mara ambayo huchangia sana kuongezeka uzito.
Uzito na kula kula hovyo ni marafiki wakubwa. Ukiona mtu ni mnene ujue anapenda kula. Ile kweli anakulakula ikimaanisha anakula kila mara na kila wakati chakula kinapokuwepo.
Anza leo kujenga tabia ya kula kidogo na katika milo muhimu mitatu.
Ndiyo,chumvi inaongeza uzito. Sodiamu iliyomo katika chumvi inachangia katika mchakato wa kikemikali unaopelekea kuongezeka uzito. Tumia chumvi katika kiwango kidogo.
Updated at: 2024-05-25 10:37:50 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana na kuamka ghafla usiku ambapo ubongo hukisa damu ya kutosha.
Unapoamka katikati ya usiku kwenda kujisaidia haja ndogo mfumo wa damu unakuwa umebadilika. Kwa sababu kuamka ghafla,kinakuwa hakuna mzunguko wa kutisha wa damu kwenye ubongo unaosababisha moyo kushindwa kufanya kazi kutokana na ukosefu wa damu.
Ushauri:tumia dakika 3 na nusu kufanya yafuatayo":
1. Unapoamka usingizini lala kitandani kwa nusu dakika ;
2. Kaa kitandani kwa takribani nusu dakika;
3. Shusha miguu,kaa pembeni ya kitanda takribani nusu dakika.
Baada ya dakika 3 na nusu hutakuwa na tatizo la ukosedu wa damu kwenye ubongo na moyo kushindwa kufanya kazi inapunguza uwezekano wa vifo vya ghafla na kuanguka ghafla.
Shirikisha marafiki na jamaa.
Inatokea bila kujali umri.
Kushare ni kujali.Kama tayari ulikuwa unajua hili lichukulie kama kumbukumbu.
Updated at: 2024-05-25 10:37:31 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mbalimbali.
Hizi ni hatua chache za kutibu chunusi kwa kutumia uwatu
a)Chukua kijiko kidogo cha unga wa mbegu za uwatu
b)Ongeza maji kidogo kupata uji mzito (paste)
c)Pakaa mchanganyiko huu sehemu yenye chunusi
d)Acha kwa dakika 20 au kwa usiku mzima
e)Kisha jisafishe a maji safi
f)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 kwa wiki
Updated at: 2024-05-25 10:35:10 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua uzito ni jambo tu la kula kalori chache na kufanya mazoezi zaidi. Hata hivyo, si mara zote zoezi hili linakuwa rahisi. Kama ni lengo lako kupunguza uzito, kuchagua chakula gani ule ni muhimu kama kuchagua kiasi gani cha chakula ule. Ukweli ni kwamba , baadhi ya vyakula vinauwezo wakusaidia kupunguza uzito kutokana na tabia zake za kuunguza mafuta mwilini.
Updated at: 2024-05-25 10:37:30 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi.
a)Kijiko kimoja cha asali
b)Kijiko kimoja cha mtindi
a)Changanya hayo mahitaji yako mawili vizuri
b)Pakaa ple pole mchanganyiko huu kwenye uso wako
c)Ikikauka unapaka tena, hivyo hivyo mpaka umepaka mchanganyiko wote
d)Acha dakika 10 mpaka 15 hivi
e)Mwishoni jisafishe na maji ya uvuguvugu
Updated at: 2024-05-25 10:35:29 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tatizo la Mtindio wa Ubongo au Kupooza ubongo kitaalamu ni Cerebral plasy (CP), ni hali ya kupooza ya moja kwa moja ya viungo vya mwili inayotokana na sehemu ya ubongo (seli) inayotawala viungo hivyo kufa katika kipindi cha mwanzo cha maisha (Utototni).
Mtindio wa Ubongo ni aina ya tatizo la mishipa ya fahamu inayoathiri misuli ya mwili inayotokana na selli za ubongo wa mtoto kufa au kutengenezeka vibaya katika kipindi cha mwisho wa ujauzito (3rd trimester), kipindi cha kuzaliwa au kipindi cha miaka miwili ya mwanzo wa mtoto.
Hii inatoka na sehemu ya ubongo kukosa oksijeni na virutubisho vya kutosha inayopelekea celli hizo kufa. Tunajua kuwa ubongo una kazi mbalimbali mfano kufikilia,kufanya maamuzi(decion making) pia inatawala sehemu mbalimbali ya viungo vya mwanadamu,mfano ubungo wa nyuma unahusika na kuona kama wakati mtoto akichelewa kulia cell za ubongo wa nyuma (occipital) zikafa mtoto huyu baadae atakuwa na matatizo ya kuona.
Vitu vingi vinaweza kusababisha ubongo kupooza, navyo ni katika kipindi cha ujauzito (mtoto akiwa tumboni), wakati wa kujifungua(80%) na kuugua mtoto kipindi cha mwanzo kabla ya miaka miwili.
Zaidi ya 67% ya watoto wote wenye tatizo la ubongo kupooza(CP) Tanzania inatokana na kuchelewa kulia baada ya kuzaliwa(birth asphyxia) ambayo inatokana na mama mjamzito kukaa na uchungu kwa muda mrefu(prolonged labour).
Ikifatiwa na manjano (severe neonatal jaundice) na degedege baada ya kuzaliwa inayopelekea celli za ubongo kufa.
Kabla ya miaka 2, mtoto akipata homa ya uti wa mgongo(meningitis) mtoto kuanguka(head trauma), malaria kali, matatizo haya yanaweza kuathiri seli za ubongo za mtoto ambazo haujakomaa.
Katika kipindi cha awali ujauzito(1st trimester) mama akipata mashambulizi ya magonjwa na kipindi cha miezi ya mwisho ya ujauzito (3rd trimester) shinikizo la damu kuwa juu (Pregnancy Induced Hypertension) na kifafa cha mimba/eclampsia kinaweza sababisha usafirishaji wa damu yenye oksijeni na virutubisho kupitia kondo la nyuma kushindikana vizuri hii inaweza pelekea baadhi ya cell kwenye mwili wa mtoto aliye tumboni kufa.
Kwa utafiti uliofanyika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mwaka 2013 kuhusiana na sababu za watoto waliopooza ubongo, inaonesha zaidi ya 80% ya watoto wenye tatizo hilo linatokana na matatizo katika kipindi cha kujifungua.
Madhala ya ubongo kupooza huwa yanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwasababu inategemeana na sehemu ipi ya ubongo iliyoathiriwa zaidi.
Kupooza ubongo(CP) kunaleta matokeo mabaya ya moja kwa moja(permanent) katika mwili wa mtoto, Kila mfumo katika mwili wa mtoto unaweza athiriwa mfano mfumo wa chakula, wa hewa, mkojo,fahamu, na wa misuli ,athari zenyewe ni kupata degedege, Kifafa, mtoto kuwa na kichwa kikubwa(macrocephaly), mtoto kuwa na kichwa kidogo sana(microcephaly), tatizo la kusikia, kuona, kuongea,kumeza pia kushindwa kutembea na kupata choo ngumu (constipation) , Pia utahila (mental retardation).
Tatizo la ubongo kupooza hakuna matibabu yake, kinachotibiwa ni matokeo ya tatizo hili yanayosaidia kubolesha maisha yao na kuwa na hali ya kujitegemea.
Katika matibabu kuna aina mbili nayo ni medical (dawa) na mazoezi(therapy).
Dawa zinazotumika mfano phenobarbitone na Carbamazepine kwa degedege na kifafa na kukakamaa (contracture,spasticity) hupewa BOTOX inayosaidia kupunguza tatizo.
Kuna therapy mbalimbali kwa watoto wenye CP, nazo ni Physiotherapy, Occupational therapy, Speech therapy n.k.
Kwa tatizo la kutoweza kutembea, watoto hawa wanaweza pata faida katika kitengo cha mazoezi(physiotherapy) mzazi anaweza kufundishwa ili kumsaidia , misuli ya mwili kupata nguvu,hupunguza kukakamaa na pia inasaidia kupata ujuzi wa kutembea n.k. Pia kuna Occupational therapy inamsaidia mtoto apate uwezo wa kula mwenyewe na kukaa.Speech therapy/kuongea, watoto wengi wenye CP huwa na tatizo la kuongea hii inatikana na misuli inayosaidia katika kuongea kuathiriwa, kuna vifaa vinavyotumika kumsaidia mtoto mwenye tatizo hili ili aweze kuongea vizuri.
Sio watoto wote wenye kupooza ubongo wana utahila (mental retardation), 36% ya watoto wenye ubongo kupooza wana utahila(mental retardation). Mtoto anaweza kuwa na tatizo la viungo ila ana uwezo mkubwa wa kufikilia.
Jamii:Kwa utafiti uliofanyika katika hospitali ya Muhimbili, inaonesha zaidi ya asilimia 30 ya wazazi wanahusisha tatizo hili na mambo ya kishirikina(superstition) Wazazi wengi wenye watoto hawa wanafanya maamuzi ya kuwaficha watoto wao vyumbani kutokana na mtazamo wa jamii husika .
Familia:Pia imegundulika kuwa ndoa nyingi huvunjika mara baada ya kuzaliwa watoto wenye CP, kati ya wanawake 100 wenye watoto hawa waliohojiwa katika hospitali ya Muhimbili 16 wanaishi peke yao baada ya kupata watoto hao, wengi wao wanadai kuwa waume zao wanawalahumu kuwa wenyewe ndio chanzo cha hao watoto.
Pia wanawake wengi hupata changamoto katika malezi ya watoto hawa, wengi wao huwatekeleza katika vyumba inayopelekea kuharibika kisaikolojia.Hii inatokana na hali ya uchumi wa familia, mama na wanafamilia wote kuondoka nyumbani kwenda kufanya ujasiliamari ili kujikimu na maisha.
Familia :upendo unahitajika wa hali ya juu kwa watoto hawa, ili wasiharibike kisaikolojia. Kuna watoto wameweza kufanya vizuri katika masomo ambao wana tatizo hili, sio wote wanapata utahila, mtoto anaweza kushindwa kutembea lakini akawa na IQ kubwa, katika watoto waliokuwa wanahudhulia clinic ya watoto wa CP na kifafa Muhimbili, alikuwepo mmoja aliyekuwa anaongoza katika darasa analosoma na pia anamipango wa kusoma ili kuwasaidia watoto wenye tatizo hili, pia kuna madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu kwa watoto walioko marekani(Paediatric neurologist) ambao wana matatizo hayo.
Wazazi wasikate tama kwa watoto hawa kwa sababu kwa therapi mbalimbali watoto wanaweza rudi katika hali kama watoto wengine, pia wakiendelea kutumia dawa na kuhuzulia clinic kama watu wenye sukari na presha.
Uongozi: Kupitia vyombo vya Habari na vipeperushi , jamii ya Tanzania katika miji na vijiji, elimu itolewe kuhusiana na sababu ya tatizo ili kuweza ziepuka. Pia kuna vituo vichache sana vya mazoezi (physiotherapy na occupational therapy) wazazi wanapata changamoto nyingi, katika jiji la Dar, wengi wao huenda katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya mazoezi, kutokana na hali ya uchumi, nauli inakuwa changamoto wanaamua kuacha kuhudhulia kliniki.
Fursa ya kufungua vituo vya mazoezi(physiotherapy) na shule katika kila wilaya kwa sekta binafsi na serikali itasaidia watoto wenye CP. Pia shule za watoto wenye CP katika nchi ya Tanzania hazipo, kuna shule chache za watoto wenye utahila, watoto wenye CP sio wote wenye utahila.
Updated at: 2024-05-25 10:37:33 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Updated at: 2024-05-25 10:35:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes.
Ugonjwa huu huenea zaidi msimu wa nvua. Huchukua siku 3-14 kwa mgonjwa kuonyesha dalili za dengue. Dalili kuu za dengue huwa ni maumivu makali ya kichwa, mgongo pia kutokwa na damu maeneo ya wazi kama puani maskioni (Hasa watoto) .
Siku zote kinga ni bora kuliko tiba hivyo huna budi kufanya yafuatayo kujikinga na ugonjwa hatari wa dengue:
1. Epuka Kuvaa nguo fupi kama kaptura, shati au tisheti kata mikono. Vaa suruali na shati/sweta la mikono mirefu
2. Usiweke Makopo chini ya Viyoyozi kwani hudondosha maji yanayoweza kuwavutia mbu.
3. Maji ya kwenye makopo ya maua yabadilishwe mara kwa mara.
4. Epuka Kuanika nguo Mbichi ndani ya nyumba. Hii huwavuta mbu kuzaliana
5. Osha vyombo visivyotumika angalau mara moja kwa wiki.
6. ondoa madimbwi yoyote yanayotuwamisha maji.
7. Tumia chandarua unapolala nyakati za mchana.
8. Funika makopo ya taka ili kutowavutia mbu.
9. Kunywa maji mengi na jenga mazoea ya kunywa juice za matunda.
10. Usiache milango wala madirisha wazi bila sababu ya msingi.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wapendwa, napenda kushirikiana na nyinyi kujuzana hili nililolisikia kupitia channel ten leo asubuhi kuhusu ugonjwa wa kisukari.
Wataalam waliokua wakitoa mada walikua Prof Endrew Swai na Dr Mohamed Juma.
Kwa ufupi wamesisitiza sana kufanya mazoezi kwa takriban nusu saa kwa siku na ambayo mtu anatoa jasho na moyo kumwenda mbio. Hiyo ni kwa ajili ya kusaidia misuli ya miguu,tumbo kifua, mgongo na mikono kutumia kiasi cha sukari kinachozalishwa mwilini.
Kadhalika wamesisitiza sana kula vyakula visivyokobolewa,ikiwamo kula dona badala ya sembe,ulezi,mtama na matunda.
Watu wapunguze na ikiwezekana kuacha kunywa vimiminika vyenye sukari,ikiwamo juice,soda pombe na vinginevyo. Na hiyo nikwasababu vinywaji hivyo havikai tumboni na badala yake huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida.
Vyakula visivyokobolewa vinafaida sana kwani vinachukua muda wa kutosha kutoka kwenye tumbo na kwenda kwenye utumbo mwembamba na hatimaye kuvunjwavunjwa kwa ajili ya kutumika mwilini. Kadhalika makapi yatokanayo na hivyo vyakula hutuzuia kupata kansa ya utumbo. La ajabu wametoa takwimu za kutisha kwani ulaya kwasababu wanakula vyakula vilivyokobolewa wanapata kansa ya utumbo kuliko nchi au bara la afrika,
na kansa hiyo ni ya nne kwa kusababisha vifo barani ulaya na amerika.
Tafadhalini tujihadharini kwani mada ilikua ndefu na nzuri sana kwa mustakabali wetu na afya zetu.
1.Mazoezi ni muhimu
2.Vyakula viwe na uasilia wake
3.Mtu aliye na mwenza wake afanye tendo la ndoa kwa kadiri inavyowezekana kwani ni sehemu ya mazoezi
4. Tubadili mifumo ya maisha yetu,kukaa tu bila kuishughulisha miili yetu.
Atakayeona anataka kupata elimu zaidi hao madaktari niliowataja wapo hospitali ya muhimbili kitengo cha tiba ya kisukari.
Ufahamu juu ya afya yako binafsi âŚnimeikuta sehemu đđđđđđ
Updated at: 2024-05-25 10:35:30 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemengâenywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama âketonesâ.
Ketones zina uwezo wa kusambaza nguvu katika ubongo hata kama insulin itakuwa chini ya kiwango kama matokeo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Insulin kazi yake kubwa ni kuishughulikia sukari (glucose) na hivyo kuzipa nguvu seli za ubongo.
Ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hauwezi kujitengenezea insulin yake kwa usahihi na vya kutosha. Kwa hiyo inashauriwa kutumia mafuta haya.
Mafuta ya nazi yanao uwezo wa kupigana na seli za kansa. Tafiti za karibuni zinasema kitu chochote chenye uwezo wa kuuongezea nguvu ubongo husaidia pia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa katika mwili.
Zaidi ni kuwa mafuta haya yana uwezo wa kumdhibiti bakteria ajulikanaye kama âhelicobacter pyloriâ ambaye husababisha vidonda vya tumbo.
Kuongeza kinga ya mwili ni moja ya faida za mafuta ya nazi sababu ni mafuta ambayo hupigana dhidi ya bakteria, fangasi na virusi mbalimbali.
Paka moja kwa moja juu ya ngozi au kuyanywa pia kuchanganya kwenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili.
Mafuta ya nazi yana asidi mafuta nzuri zenye uwezo wa kusaidia na kuzilinda seli za ubongo na kuziwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
Mafuta ya nazi yanajulikana vizuri kwa uwezo wake wa kukuongezea uvumilivu yaani stamina.
Mafuta ya nazi ni dawa ya mba na mara nyingine hutumika kwa kuchanganywa na mafuta mengine
Ni mazuri kwa ngozi na yanatibu magonjwa mbalimbali ya ngozi.
Mfuta ya nazi yanaweza kuzuia mpaka asilimia 20 ya miale ya jua kushindwa kukufikia moja kwa moja kwenye ngozi yako kama utayafanya kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa.
Wengi mnapenda kufanya scrub hasa usoni (facial). Kwa lugha nyepesi ni kitendo cha kusugua ngozi kwa dawa maalumu ili kuondoa uchafu wote na kuifanya ionekane nyororo na yenye kupendeza.
Sasa huhitaji dawa zenye kemikali kwa ajili hiyo wakati mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia hilo bila madhara yoyote mabaya.
Fanya hivi changanya nusu kikombe (mln125) cha mafuta ya nazi na sukari kikombe kimoja na ufanye dawa ya kusugua na kusafisha uso wako.
Unaweza pia kutumia nazi yenyewe moja kwa moja kabla hujapata mafuta yake.
Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza kutumika kama scrub ya asili ya ngozi yako.
Fuata hatua hizi zifuatazo ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini, nyororo na wenye mvuto.
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini hapa nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.
*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yaani mara moja kwa siku.
Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako na hata vocha utaninunulia kunipongeza.
Unatakiwa kupakaa tu sehemu yenye tatizo moja kwa moja huku ukinywa kijiko kidogo kimoja kila siku na hutakawia kupona hivyo vidonda.
Yanangarisha kucha na kuzikinga na wadudu.
Mafuta ya nazi Yanaweza kutumika kama dawa ya asili ya kufukuza wadudu (insect repellent) wakiwemo mbu. Unachohitaji ni kuchanganya pamoja na kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu au ya mnanaa (mint) na ujipake juu ya ngozi yako na hakuna mdudu yoyote akiwemo mbu atakayekusogelea.
Mafuta ya nazi yana viondoa sumu vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya vijidudu nyemelezi.
Zaidi, matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kurahisisha umengâenywaji wa madini ya kalsiamu tumboni mwako.
Upungufu wa madini ya kalsiamu mwilini husababisha mifupa kuwa hafifu jambo linaloishia kuleta ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
Kuzuia ugonjwa wa mifupa unahitaji kuongeza mafuta ya nazi kuwa sehemu ya chakula chako. Hii ndiyo faida ya mafuta ya nazi ambayo niliona si vema kama sitakuambia.
Watu wenye vitambi au unene uliozidi wanatakiwa kuongeza mafuta ya nazi kwenye milo yao na miili yao itakaa sawa yenyewe.
Matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kusaidia mafuta kuchomwa zaidi mwilini huku kiasi chako cha njaa kikishuka.
Mifadhaiko ni jambo lisiloweza kuepukika katika maisha yetu. Kazi ya mfadhaiko au stress ni kukufanya uwe imara zaidi, mpole na unayejiamini zaidi.
Unapofadhaishwa mwili wako huwa unajiongeza na kuwa na shauku ya kufanikiwa zaidi. Hata hivyo mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu unaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika kihisia na hata kimwili pia.
Mfadhaiko wa muda mrefu unaweza kupelekea huzuni mbaya na hatimaye kuathiri muonekano wako.
Watu wenye mifadhaiko (stress) ya muda mrefu huonekana ni wenye umri mkubwa hata kama umri wao bado ni mdogo.
Tafiti za karibuni zimeonyesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kupungua kwa mfadhaiko wa akili.
Tunaweza kusema kuwa, kitendo hiki cha kuondoa mfadhaiko au stress ni moja ya kazi ya kustajaabisha kabisa ya mafuta ya nazi. Asidi mafuta zilizomo ndani ya mafuta haya ndizo zinazohusika na kazi hii mhimu.
Ili mwili wako ubaki ni wenye afya na kuzuia usipatwe na magonjwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula na wakati huo huo mfumo imara wa uchukuwaji wa viinilishe, madini na vitamini mbalimbali kutoka kwenye chakula unachokula.
Kwa bahati nzuri, kuuongezea nguvu mfumo wa mmengâenyo wa chakula ni kazi nyingine ambayo mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia bila madhara mengine mabaya.
Matumizi ya mafuta ya nazi yatakuwezesha kuongeza uchukuwaji wa viinilishe mhimu kutoka kwenye chakula sababu mafuta haya yana madini ambayo huweza kuyeyuka kwenye mafuta kama kalsiamu na magnesiamu.
Zaidi, mafuta haya yanaweza kusaidia umengâenywaji wa mafuta mengine magumu ndani ya mwili kama matokeo ya kuimarishwa kwa vimengâenya vinavyohusiana na mmengâenyo wa chakula.
Kama unapata maumivu au matatizo yoyote katika kongosho au kibofu cha mkojo unahitaji kuongeza matumizi ya mafuta ya nazi.
Ukiendelea kutumia mafuta ya nazi kila mara utaweza kujitibu pia tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo na kuondoa hali ya kutojisikia vizuri kutokana na magonjwa katika kongosho au kibofu cha mkojo.
Faida kubwa ya mafuta ya nazi haiishii katika uwezo wake wa kuchoma mafuta, bali yana kazi nyingine ya kushangaza zaidi nayo ni kutengeneza misuli ya mwili.
Kwenye bidhaa nyingi zinazouzwa zaidi duniani za kutengeneza virutubishi vya kutengeneza misuli ya mwili mafuta ya nazi lazima yawemo.
Kama unataka kuongeza misuli mingi mwilini kirahisi zaidi changanya tui zito la nazi kikombe kimoja (robo lita), ongeza vanilla vijiko vikubwa vitatu, ongeza maji maji ya chungwa vijiko vikuwa viwili na ndizi zilizoiva mbili.
Saga na mashine ya kusagia matunda jikoni (blender) mchanganyiko huu kwa pamoja na ule wote kutwa mara 1 kila siku.
Kuzuia kuoza kwa jino na magonjwa ya fizi ni moja ya kazi nyingine nzuri ya kushangaza ya mafuta ya nazi ambayo nimependa kukufahamisha kupitia makala hii.
Mafuta ya nazi ni dawa inayoweza kudhibiti bakteria wabaya na hivyo kuzuia kuoza kwa jino na maumivu mengine katika fizi. Ili kuzuia haya unahitaji tu kutumia mafuta yako ya nazi kama dawa yako ya mswaki kila siku.
Unaweza pia kuongeza kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto ili kutengeneza dawa ya kusafisha mdomo (mouthwash).
Kwa mjibu wa madaktari wengi, kuna uhusiano wa karibu kati ya madhara ya figo na kushindwa kufanya kazi kwa ogani hii mhimu.
Kama tatizo la kufeli kwa figo halitapatiwa ufumbuzi linaweza kupelekea kifo. Figo na Ini ni ogani mhimu zaidi katika mwili ambazo zinatakiwa kupewa uangalizi wa karibu kila mara zisipatwe na madhara yoyote.
Kwa bahati nzuri, mafuta ya nazi yanayo uwezo wa kulinda figo na Ini visipatwe na madhara yoyote mabaya moja ya kazi ya mafuta ya nazi mwilini ulikuwa huijuwi bado.
Wanasayansi wameviona viinilishe katika mafuta ya nazi ambavyo ni mhimu sana kwa afya ya Ini na figo katika mwili wa binadamu.
Nazi pamoja na mafuta ya nazi huwa na asidi mafuta mhimu sana ambazo huhamasisha uundwaji wa âMonooctanoinâ ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mawe katika kibofu cha mkojo na figo.
Wagonjwa ambao hawawezi kumudu gharama za upasuwaji kuondoa mawe katika figo na katika kibofu cha mkojo wanaweza kujitibu hilo kwa kutumia mafuta ya nazi kama dawa mbadala.
Unachohitaji kufanya ni kunywa tu kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kila siku kutwa mara 1 mpaka utakapokuwa umepona.
Mafuta ya nazi hudhibiti uvimbe na kuondoa sumu mwilini, kazi hizi mbili zinayafanya kuwa dawa bora ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi.
Unahitaji kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila siku ili kujitibu na ugonjwa wa baridi yabisi.
Faida za mafuta ya nazi zinahusu pia kurekebisha kazi za ogani za mwili kama kuweka sawa mapigo ya moyo, kupumua na kuzalisha homoni mhimu.
Tezi koromeo huzalisha homoni mbili ambazo huwa na msaada mkubwa katika kuongeza nguvu katika mfumo wa mmengâenyo wa chakula.
Ufanisi mzuri wa tezi hii huweza kuhakikisha mapigo ya moyo ni sawa, uzito sawa wa mwili, na usawa ulio sawa wa homoni.
Kutibu kisukari aina ya kwanza ni moja ya kazi nyingine nzuri za mafuta ya nazi sababu mafuta haya yanao uwezo wa kuiweka sawa damu sukari (blood glucose) ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yamethibitika siyo katika kushusha kisukari aina ya kwanza tu bali pia katika kuweka sawa aina mbalimbali za homoni mwilini.
Kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kwa siku kinatosha kwa kazi hii.
Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nyingine nzuri kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi kwa sababu moja kuu kwamba ni mafuta yanayoweza kuua bakteria na virusi mbalimbali.
Hii ni kazi ya mafuta haya ambayo isingekuwa vema kama nisingekujulisha kupitia makala hii. Hii ni matokeo ya kuwa na âlauric acidâ na âcapric acidâ.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha uhusiano uliopo baina ya matumizi ya mafuta yenye afya na kushuka kwa maambukizi ya fangasi.
Kwa fangasi yoyote juu ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kama mafuta yako ya kupakaa kila siku pia unaweza kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kuongeza kinga zaidi ya mwili.
Maradhi mengi mwilini huja kama sababu ya homoni zako kutokuwa sawa. Ni bahati kufahamu kuwa mafuta ya nazi ni moja ya dawa za asili nzuri katika kuziweka sawa homoni zako.
Hii ni kwa sababu mafuta ya nazi yana mafuta mazuri yajulikanayo kama âlauric acidâ. Mafuta ya nazi huiweka sawa homoni mhimu sana kwa upande wa uzazi kwa mwanamke homoni ijulikanayo kama âestrogenâ. Chanzo kingine kizuri cha homoni hii ni pamoja na tunda la parachichi.
Kuzeeka mapema ni jambo lisilopendwa karibu na watu wote. Kuzeeka mapema hakuathiri muonekano wako tu bali huathiri pia afya yako.
Tunapozungumzia juu ya faida za kushangaza zilizomo katika mafuta ya nazi lazima ujuwe kuwa mojawapo ni hili la kukufanya usizeeke mapema.
Viuajivijasumu vilivyomo kwenye mafuta ya nazi hufanya kazi mhimu katika kupunguza vijidudu nyemelezi na matatizo mengine katika ini.
Kuzuia magonjwa ya ubongo ni faida nyingine ya mafuta ya nazi ambayo unapaswa kuijua.
Asidi mafuta zilizomo kwenye mafuta ya nazi hubadilishwa na kuwa âketonesâ ambazo huzuia kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Kupoteza kumbukumbu ni matokeo ya kuongezeka kwa kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama âamyloid beta peptidesâ.
Kwenye mafuta ya nazi kuna kitu mhimu sana kijulikanacho kama âPhenolic compoundsâ ambacho hudhibiti ile kemikali ya âamyloid beta peptidesâ na hivyo kukuondolea tatizo la kupoteza kumbukumbu kirahisi zaidi.
Mafuta ya nazi yanaweza kukupunguzia hitaji lako la kutaka kula chakula kila mara kwa kuwa hufanya kazi ya kupunguza njaa ndani ya mwili.
Kutumia mafuta ya nazi kutakufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na kama matokeo yake kutakusaidia kupunguza kiasi cha nishati unaingiza ndani ya mwili wako kila siku.
Kuna uhusiano wa karibu kati ya mafuta safi kwa afya na kuwa na njaa ya wastani.
Tafiti mbalimbali Zimeonyesha kwamba Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto (high-density lipoproteins -HDL) unao uwezo wa kulinda moyo wako.
Hivyo mafuta ya nazi yanaweza kupunguza hatari kwako ya kupatwa na ugonjwa wa moyo moja ya kazi nyingine mhimu sana ya mafuta haya.
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo âlauric acidâ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.
Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
Tafiti zimeendelea kuonyesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kuimarika kwa mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula.
Mafuta ya nazi yanapokuwa yamemengâenywa ndani ya mwili wako hutumika kama nguvu yako moja kwa moja.
Watu wanaotumia mara kwa mara mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku wanakuwa na mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula jambo ambalo ni mhimu katika kuchoma mafuta na nishati ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yanasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kwani mafuta ya nazi yana kiasi cha kutosha cha viuajivijasumu (antioxidants) dhidi ya vijidudu mbalimbali nyemelezi.
Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuotesha na kukuza nywele.
Mafuta ya nazi ni mazuri kwa kupaka mdomoni. Vilevile kama una tatizo la midomo kukauka basi uwe unapakaa mafuta ya asili ya nazi kila mara.
Mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto.
Mafuta ya nazi hubaki katika hali yake hata katika joto la kawaida tofauti na mafuta mengine.
Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri kwa ajili ya masaji na kukupatia hali ya utulivu unaouhitaji kupitia masaji.
Pakaa mafuta ya nazi katika uke kulainisha. Faida nyingine unapopaka mafuta haya ukeni ni kutibu fangasi na bakteria tena bila madhara.
Mafuta ya nazi yanaweza kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji. Kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na hauta piga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.