Ujasiriamali: Matumizi ya Fedha

[caption id="attachment_2939" align="alignnone" width="300"]Mbinu za kutumia na kupata Pesa Mbinu za matumizi na kutafuta fedha[/caption]

Ni vizuri kujua haya

👉🏿Degree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
👉🏿Uzuri ulio nao hauwezi kukupeleka kwenye ndoto zako.
👉🏿Usipobadilisha hao marafiki ulio nao hutofika mahali popote.

👉🏿Usipobadilisha vitendo unavyovifanya kila siku hivyo hivyo mafanikio utayasikia kwa wengine.

👉🏿Kazi au ajira unayoifanya usipojiongeza haiwezi kukupeleka kwenye maisha unayoyataka.

👉🏿Huo mshahara unaolipwa usipoutumia vizuri na kujiwekea akiba au kuwekeza kidogokidogo hutoacha kulalamika kila siku mshahara mdogo au hautoshi.

👉🏿Usipoacha kukopa bila malengo mafanikio ni ngumu kuyapata.

👉🏿Usipowekeza muda kwa ajili ya kujifunza na kuelewa mambo mengi ya biashara na ujasiriamali kwa ujumla na kufahamu dunia imetoka wapi,iko wapi na inaelekea wapi huytoacha kulalamika.

👉🏿Usipolipia gharama za kujifunza na ukajifunza kweli kile unachoelekezwa ikiwa ni pamoja na Pesa na muda haya mambo waachie wengine.

👉🏿Usipobadili fikra na mtazamo wako huwezi kubadilisha chochote katika maisha yako.

👉🏿Ukiacha kusikiliza kila aina ya ushauri unaopewa na ndugu zako,jamaa zako,marafiki zako,familia yako,majirani zako na kujisikiliza wewe mwenyewe utahangaika sana.

👉🏿Usipofanya bidii na juhudi na ukakubaliana na changamoto zozote utakazokutana nazo maisha yatakuwa magumu sana kwako.

Kumbuka mtu pekee Wa kuyabadilisha maisha yako na kukusaidia kufikia malengo na ndoto zako wala sio mwingine ni mmoja tu nae ni WEWE.
Badilisha fikra zako,badilisha mtizamo wako,badilisha maisha yako.

Ujumbe kwako wewe mwajiriwa au uliyejiari

Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-

Kwako muajiriwa

👉🏿Umeshawahi kujiuliza huo mshahara unaolipwa unakutosha kukutimizia Yale yote unayohitaji maishani mwako??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ukifukuzwa au ukipunguzwa kazini utafanya nini?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ofisi au kampuni unayofanyia ikifilisika wewe utafanya nini?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuhama au kuacha kazi hapo unapofanyia uende ofisi nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwanini hupapendi hapo unapoishi lakini bado unaendelea kuishi hapo?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini huo usafiri unaoutumia huupendi lakini kila siku unautumia huo huo??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanao au watoto wako hawapendi shule wanayosoma lakini wewe uwezo wako ndipo ulipoishia??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini hupendi mikopo lakini bado unaendelea tu kukopa??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza unaipenda kwa dhati tena kutoka moyoni kazi unayoifanya??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unaomba kila Mara kuongezewa mshahara kama sio kuandamana??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unatamani ukasome uongeze elimu??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini mkubwa wako kazini hataki uache kazi au ukasome au uhamie ofisi nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini kila siku uko “busy” kazini au ofisini mpaka unakosa muda wa kufurahia na ndugu,jamaa,na marafiki na familia na mifuko yako au akaunti yako benki haiko “busy”??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kufungua kibiashara chako au unataka ufanye kilimo Fulani kwa sababu umesikia kinawatoa watu???

👉🏿Umeshawahi kujiuliza usipokwenda kazini kwa muda Wa wiki au mwezi au mwaka je kipato hicho hicho unachokipata utaendelea kukipata??

Hebu jiulize hayo maswali na mengine mengi yanayofanania na haya ujaribu kuona kama majibu yake unayo na kama majibu yapo ni njia gani unatumia au unategemea kutumia ili kuondokana na hayo??

Kwako wewe uliyejiajiri

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini biashara yako haikui kwa muda wote huo uko pale pale??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka uachane na hiyo biashara ufanye nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini kila kitu unafanya wewe mwenyewe haumruhusu msaidizi kuwepo??

👉🏿Kwa nini huthubutu kumuachia mtu biashara yako kwa muda tu ukiondoka unafunga??

👉🏿Kwa nini unawaumiza wengine au wengine wanaumia ndipo wewe utengeneze faida yako??

👉🏿Kwa nini huwezi kuwasaidia wengine waweze kutengeneza kipato kama chako??

👉🏿Kwa nini akija mwenzako pembeni yako kufungua biashara kama yako unachukia???

👉🏿Kwa nini unachukia kulipa kodi ya pango lakini inakubidi tu ufanye hivyo??

👉🏿Ni watu wangapi wanaichukia au kuipenda biashara yako??

👉🏿Wangapi wanakuongea vizuri au vibaya kutokana na Huduma yako unayotoa??

👉🏿Kwa nini unatamani usiwe unalipa kodi??

👉🏿Kwa nini hupendi kuwaonyesha wengine njia unazotumia katika kuijenga biashara yako??ikiwa ni pamoja na upatikanaji Wa mizigo,unavyouza na unavyopata Wateja??kwa nini?

👉🏿Kwa nini hupendi kuona aliyeanza nyuma yako akifanikiwa kabla yako??

Hayo ni baadhi ya maswali ya kujiuliza wewe kama mjasiriamali au uliyejiajiri ingawa yapo na mengine unaweza kujiuliza tu uone kama utapata majibu yake na yawe ya kueleweka

Shopping Cart