SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Jumamosi
Cheki kilichotokea baada ya kufumaniwa
Nimefumaniwa hapa na jamaa ameniambia nitulie tuyamalize kishikaji, yaani nisijali sasa ametoka nje nasikia ananoa kisu nadhani anataka anichinjie kuku!
WATU WENGINE WANA ROHO NZURI!ππππ
Hakuna siku mbaya maishani kama hii
Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu we umeninginia kwenye daladala,,, tena ulikua unamzid akili πππhapo Ndo utajua kwann gunia na dunia vinatofautiana neno moja
KICHEKESHO: Ukiona masikini Kachinja kuku
Ukiona masikin kachinja kuku basi kat ya kuku au yeye kuna mmoja atakua mgonjwaΒ ππππ
Eti wanadamu walikuja vipi duniani
Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo waoπππΆπΌπΆπΌπΆπΌ