SMS kwa mpenzi kumwambia unampenda kwa moyo
unaweza ukafunga macho kwa usilolitaka kuliona lakini
hauwez kufunga moyo wako kwa Unalo Lipenda. Nakupenda
Mpenzi
unaweza ukafunga macho kwa usilolitaka kuliona lakini
hauwez kufunga moyo wako kwa Unalo Lipenda. Nakupenda
Mpenzi
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa
penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi
kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye
kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye
mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako
Safarini nitajenga hekalu la pendo letu
Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako
Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Naomba niwe CHOZI ndani ya JICHO lako,
Nikitoka tu NIDONDOKE kwenye SHAVU lako,
Ukinipangusa NIGANDE kwenye KIGANJA chako,
Kwa sababu NAKUPENDA sana