Katoliki: Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa

Mafundisho kuhusu Toharani

Toharani ni mahali gani?

Toharani ni mahali pa mateso zinakosafishwa roho ambazo hazikutimiza kitubio vizuri baada ya kuungama dhambi. (1Kor 3:15, 1Pet 1:7).

 


 

Je, hatuwezi kupunguza mateso ya roho za marehemu waliokwenda toharani?

Ndiyo: twaweza kupunguza hata kuyamaliza kwa kuwasalia na kuwapatia rehema na hasa kwa kuadhimisha Misa kwa ajili yao. (2Mik 12:38-46)

 


 

Toharani maana yake nini?

Toharani maana yake kuna hali ya muda ambayo huruma ya Mungu inawatakasa marehemu waliofariki dunia katika urafiki naye lakini bila ya usafi kamili unaotakiwa kwa kuingia mbinguni. Sisi tunaweza kuharakisha utakaso wao kwa kumtolea Mungu sala na sadaka, hasa ekaristi. Yuda Mmakabayo โ€œalichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi.
Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zaoโ€ (2Mak 12:43-46). Imani hiyohiyo iliongoza Wakristo wa kwanza kuwafanyia marehemu ibada ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na Mtume Paulo: โ€œKama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?โ€ (1Kor 15:29).
Read and Write Comments

Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;
  1. Kifo
  2. Hukumu
  3. Mbinguni
  4. Motoni
Mambo haya yote yanaweza kutokea wakati wowote bila kujua wala kutarajia

Kifo

Kifo ni kitu ambacho kinaweza kumpata mtu yeyote wa umri wowote awe mtoto kijana au mzee na kwa wakati wowote.
Maranyingi watu hawapendi kuongelea kuhusu kifo kwakua ni kitu ambacho kinampata kila mtu na hakipingiki wala hakina mjadala.

Hukumu

Baada ya kifo, inafuata hukumu, kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake kama ulitenda mema utaenda mbinguni, na kama umetenda mabaya utaenda motoni.

Mbingu

Kama mtu akifa akiwa katika hali usafi wa moyo anaelekea mbinguni. Haijalishi ni kwa kipindi gani aliishi hivyo. Ila ni kwa hali gani kifo kilimkuta. Kwa sababu hii kila mtu anatakiwa aishi katika hali ya usafi wa moyo kwani hajui ni wakati gani atakutwa na kifo.

Motoni

Kama mtu akifa katika hali ya dhambi anaenda motoni. Kwa hiyo inatupasa tutumie vyema msamaa na huruma ya Mungu katika maisha yetu ili mwishi wetu uwe mzuri wakati bado tukiwa na muda.
Kila unapoishi ni lazima ufikirie mambo haya ukizingatia hujui wakati yanaweza kukupata. Kwa hiyo, nilazima uishi ukiwa unatafakari haya
ili uwe na mwisho mzuri.

Read and Write Comments

Maswali na majibu kuhusu Mpako wa wagonjwa au Mpako wa Mwisho

Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu gani?
Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu alijua udhaifu wa binadamu hauishi mara anapopokea uzima wa Mungu kwa sakramenti tatu za kuingizwa katika Ukristo. Hivyo alipanga kusaidia mpaka mwisho wa dunia waamini wake watakaopatwa na dhambi na ugonjwa, kama alivyowasaidia wengi aliokutana nao katika maisha yake.
โ€œYesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, โ€˜Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zakoโ€™โ€ฆ โ€˜Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambiโ€™ โ€“ amwambia yule mwenye kupooza โ€“ โ€˜Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwakoโ€™. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hiiโ€ (Math 9:2,6-8).


Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na nani?
Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na Yesu, kama sakramenti zote. Maandiko yanasimulia huruma yake iliyomfanya awaponye wengi kwa namna mbalimbali na kuwapa Mitume uwezo wa kufanya vilevile kwa โ€œkupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila ainaโ€ (Math 10:1). Nao
โ€œwakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapozaโ€ (Mk 6:13).
โ€œMtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewaโ€ (Yak 5:14-15).


Mafuta ya mpako wa wagonjwa yanamaanisha nini?
Mafuta ya wagonjwa yanamaanisha lengo la kuwaponya na kuwarudishia nguvu na uzuri.
Kama kawaida, maneno yanaweka wazi zaidi kuwa lengo si kuponya mwili tu, bali hasa roho kwa kuitia msamaha na faraja katika mateso ambayo huenda yakaendelea. Kwa kuwa Mungu haponyi mwili kila mara, isipokuwa kwa faida na wokovu wa mgonjwa na wa wengine. Kama ndiyo mapenzi yake, kila mmoja ajifunze kufaidika vilevile na ugonjwa:
โ€œMakusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, โ€˜Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifuโ€™. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yanguโ€ (2Kor 12:7-9).
โ€œSasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lakeโ€ (Kol 1:24).


Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ni nini?
Ni Sakramenti ambayo Padri humuombea neema ya Mungu na kumpaka Mafuta Matakatifu mgonjwa aliye katika hatari ya kifo kwa ajili ya neema ya roho na mwili. (Yak 5:14-15, Mk 6:13)
Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ilianza lini? Je, wakati wa Yesu kulikuwa na sakramenti hii?
Sakramenti ya mpako wa wagonjwa ilikuwepo tangu wakati Yesu akiwa hai. Tunaweza kuiona Kwenye Biblia tunaposoma Yesu alivyowatuma wanafunzi wake waliwapaka watu mafuta. “Waliwatoa pepo wengi Wabaya, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta wakawaponya. (Marko 6:13)


Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa inaadhimishwaje?
Inaadhimishwa kwa Padre kumuombea mgonjwa, kumuwekea mikono na kumpaka mafuta katika panda la uso na viganja vya mikono; kwa kutumia mafuta aliyobariki Askofu siku ya Alhamisi kuu.


Sakramenti ya Mpako Wa Wagonjwa inamanufaa gani rohoni mwa mtu?
Manufaa ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni
1. Nguvu ya kuvumilia mateso na kuyaunganisha na mateso ya Yesu Kristo
2. Maondoleo ya dhambi zote asizoweza kuziungama
3. Nafuu ya mwili, hata uzima ikifaa kwa wokovu wa roho yake
4. Neema ya kujiandaa kuaga dunia na kuingia katika uzima wa milele


Ni nani anayetoa Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?
Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa hutolewa na kuhani tuu yaani Askofu au Padri


Padri aitwe kwa mgonjwa lini?
Padri aitwe kwa mgonjwa mara inapoonekana Hatari ya Kifo na kamwe isisubiriwe mpaka mgonjwa apoteze fahamu.


Ni nani aweza kupokea Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?
Ni kila Mkatoliki aliyefikia umri wa kufikiri na aliye katika hatari ya kufa kwa ugonjwa au uzee aweza kupokea Sakramenti hii.


Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa yaweza kupokelewa mara ngapi?
Sakramenti hii yaweza kupokelewa mara nyingi ugonjwa ukizidi au akipatwa na ugonjwa mwingine mkubwa


Alama wazi ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni tendo la kupaka Mafuta Matakatifu wagonjwa na kutamka maneno
“Kwa mpako huu Mtakatifu na kwa pendo lake kuu, Bwana Akujaze na nguvu ya Roho Mtakatifu. Amina Akuondoe katika enzi ya dhambi, akuweke huru. Kwa wema wake akupe nafuu katika mateso yako na kukujalia neema. Amina”


Kama padri hatapatika na mgonjwa afanye nini?
Kama padri hatapatikana mgonjwa aweke nia ya kuungama na afanye majuto kamili


Komunyo pamba ndio nini?
Komunyo pamba ndio Ekaristi inayopokelewa na wale wanaokaribia kuaga maisha ya duniani na wanaojiandaa kuvukia uzima wa milele

Read and Write Comments

Shopping Cart