Je, mbegu za kiume zinaweza kupita kwenye kondomu?
Updated at: 2024-05-25 16:23:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapana, mbegu za kiume haziwezi kupita kwenye kondomu. Kondomu zimetengenezwa ili kuzuia mbegu za kiume kufikia ukeni wakati wa kujamiiana. Kwa sababu shahawa haziwezi kupita kwenye kondomu, kondomu ni njia nzuri ya kuzuia mimba pamoja na maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Watu wengine wanasema kwamba kuna mashimo madogo kwenye kondomu yanayorahisisha mbegu pamoja na vijidudu vya magonjwa ya zinaa kupita. Huu ni uongo. Ukitaka kuwa na uhakika kwamba kondomu mpya haina mashimo, chukua kondomu moja na ijaze maji ya kawaida. Utaona kwamba maji hayapiti kwenye kondomu kabisa. Baada ya kujaribisha itupe kondomu ndani ya choo cha shimo au ichome moto, lakini usiitumie wakati wa kujamiiana
Nani wa kulaumiwa kuhusu dawa za kulevya Tanzania, Serikali au wasambazaji na watumiaji?
Updated at: 2024-05-25 16:22:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna mtu wa kulaumiwa, lakini i i inabidi kila mtu awajibike. Kila mtu i inambidi afanye lolote lile lililo katika uwezo wake i ili kupunguza dawa za kulevya. Serikali i i inabidi i i ihakikishe kwamba sheria zilizowekwa zinatekelezwa. Pia i inatakiwa kuwasaidia walio na matatizo ya kimwili na kisaikolojia ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kutoa vifaa na huduma za kiafya kwao. Ni kweli kwamba watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya wanawasababishia watu wengine matatizo. Lakini kusingekuwa na usambazaji wake kama kusingekuwa na wahitaji. Hivyo basi mtumiaji anatakiwa awe na uamuzi wa kujali maisha na afya yake binafsi. Hii ndiyo sababu, watu hasa vijana wanatakiwa kuelimishwa kuhusu athari za dawa za kulevya.
Je, ni muhimu kujadili mipaka na dhibitisho wakati wa ngono/kufanya mapenzi?
Mambo ya mipaka na dhibitisho ni muhimu sana wakati wa ngono/kufanya mapenzi, lakini haimaanishi tunapaswa kuwa wakali na waoga. Hebu tuifanye hii safari ya kimapenzi kuwa yenye furaha na kujenga imani kwa kila mmoja wetu!
Updated at: 2024-05-25 16:16:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Je, ni muhimu kujadili mipaka na dhibitisho wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Ndio, ni muhimu sana kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Nimepokea maoni mengi kutoka kwa wateja wangu na wengi wao wanaamini kwamba kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho ni muhimu sana katika kuzuia matatizo ya kimapenzi. Hapa ni baadhi ya sababu kwa nini ni muhimu kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho wakati wa ngono/kufanya mapenzi:
Inasaidia kuzuia magonjwa ya zinaa: Kujadili mipaka na dhibitisho kunasaidia katika kuzuia magonjwa ya zinaa. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kujua kama mpenzi wako ana magonjwa ya zinaa au la.
Inaboresha uhusiano wako: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kuimarisha uhusiano wako na mpenzi wako. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kuelewa kila mmoja vizuri na hivyo kuimarisha uhusiano wenu.
Inaongeza usalama: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kuongeza usalama wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kuhakikisha kwamba unafanya mambo kwa usalama.
Inasaidia katika kuzuia unyanyasaji wa kingono: Kujadili mipaka na dhibitisho kunaweza kusaidia katika kuzuia unyanyasaji wa kingono. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kumwambia mpenzi wako kwamba hapendi mambo fulani na hivyo kuzuia unyanyasaji.
Inasaidia katika kuepuka matatizo ya kimapenzi: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kusaidia katika kuepuka matatizo ya kimapenzi. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kuepuka matatizo ya kimapenzi kwa sababu utakuwa umeweka mipaka na utaheshimu mipaka ya mpenzi wako.
Inasaidia katika kuboresha mawasiliano: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kusaidia katika kuboresha mawasiliano. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kuelewa vizuri mawazo na hisia za mpenzi wako.
Inasaidia katika kupunguza wasiwasi: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kusaidia katika kupunguza wasiwasi. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kujua kama mpenzi wako anajali mipaka yako na hivyo kupunguza wasiwasi wako.
Inasaidia katika kujenga imani: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kusaidia katika kujenga imani. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kumwambia mpenzi wako mambo ambayo yanakufanya uhisi vizuri na hivyo kujenga imani.
Inasaidia katika kujua kama mpenzi wako anakupenda: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kusaidia katika kujua kama mpenzi wako anakupenda. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kujua kama mpenzi wako anajali mipaka yako na hivyo kujua kama anakupenda kweli.
Inasaidia katika kuboresha hali yako ya kihisia: Kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho kunaweza kusaidia katika kuboresha hali yako ya kihisia. Unapojadili kuhusu mipaka yako, unaweza kuondoa hofu yako na hivyo kufurahia ngono/kufanya mapenzi.
Kwa hiyo, ni muhimu sana kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Unapojadili kuhusu mipaka yako na mpenzi wako, unaweza kujua kile ambacho unapenda na kisichopenda. Hivyo, utaweza kufurahia ngono/kufanya mapenzi bila matatizo yoyote na kujenga uhusiano mzuri na mpenzi wako. Je, wewe una maoni gani kuhusu hili? Unaona ni muhimu kuzungumza kuhusu mipaka na dhibitisho wakati wa ngono/kufanya mapenzi?
Updated at: 2024-05-25 16:22:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dawa za kulevya huharibu ufanyaji kaza wa kawaida wa mfumo wa mwili hasa tumbo na utumbo wa watumiaji hushindwa kufyonza virutubisho vidogo kama vile vitamini, madini kutoka kwenye chakula na kwenda kwenye mfumo wa damu. Hiki ndicho kinachowafanya wakonde. Isitoshe, hupunguza uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na hivyo huuweka mwili katika hatari ya kuambukizwa na magonjwa likiwemo gonjwa hatari la UKIMWI.
Ni dawa zipi zilizopigwa marufuku Tanzania na nini hutokea pale mwingizaji anapokamatwa?
Updated at: 2024-05-25 16:22:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapa Tanzania matumizi, umilikaji, usafirishaji na kuhusika katika dawa za kulevya kama vile bangi, hiroini, kokaini na mirungi yamepigwa marufuku. Hii ni pamoja na dawa ambazo zimethibitishwa na daktari kuwa zisitumike kwa matibabu. Kwa Tanzania “gongo”pia ni haramu. Polisi akimkamata mtu anayekwenda kinyume na sheria, humpeleka mtu huyo mbele ya vyombo vya sheria na atahukumiwa ikithibitika kuwa ana hatia. Sheria i inatoa adhabu kali kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya. Faini ya shilingi milioni 10 za Kitanzania au kifungo cha maisha au vyote kwa pamoja.
Je, uume una urefu kiasi gani? Ni kweli kwamba wanaume warefu wana uume mkubwa na wale wafupi wana uume mdogo?
Updated at: 2024-05-25 16:22:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa kawaida urefu wa uume ambao haujasisimuka kwa wastani ni kati ya sentimeta 7 na 10, na uume uliosimama ni sentimeta 13 hadi 18. Si lazima kwamba maumbile ya mtu yawiane na viungo vya uzazi.
Na vile vile katika kujamii ana, jambo la vipimo vya uume si la msingi. Kilicho muhimu ni afya nzuri ya watu wote wawili na kupendana kwao wenye uhusiano. Urefu wa uume si muhimu, kwa sababu sehemu nyingi zinazomridhisha mwanamke haziko ndani ya uke. Kuridhika au kutoridhika wakati wa kujamii ana hakutegemei urefu wa uume!
Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Updated at: 2024-05-25 16:22:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
• Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
• Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
• Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
• Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
• Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
• Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?
Updated at: 2024-05-25 16:22:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuingia utu uzima,0 yaani kuwa mwanamke. Wasichana wanavunja ungo kati ya umri wa miaka 8 na umri wa miaka 18. Lakini, kuvunja ungo haina maana kwamba unahitaji kuanza kujamii ana. Kwa sababu ukijamii ana kuna hatari ya kupata mimba!
Mwanzoni siku za hedhi zinaweza kuwa na mabadiliko sana. Ni baada ya muda ndipo msichana anaanza kwenda mwezini mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo, wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo. Idadi ya siku katika mzunguko wa hedhi ni siku 21 hadi 35.Ukitaka kuelewa kabisa maana ya kutoka damu za mwezi, lazima nieleze kuhusu mzunguko wa hedhi. Siku ya kwanza ya damu huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa.
Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mirija ya kupitishia mayai hadi kwenye mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai likirutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mirija ya kupitisha mayai, i ina maana, kwamba atakuwa amejamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka. Kama yai halikurutubishwa, basi hufa na hutangulia kutoka kama ute, pia utando kwenye mfuko wa uzazi na kuta za uzazi hubomoka na kutoka kama damu. Hii ndiyo hedhi yenyewe.
Endapo msichana amejamiiana na mvulana na yai likarutubushwa, hataona hedhi na aelewe kwamba kuna uwezekano kwamba mimba imetungwa.
Mzunguko wa hedhi kwa baadhi ya wasichana hauna mpangilio mwanzoni, hivyo endapo hupati hedhi inayolingana kila mwezi usijali.
Katika hali ya kawaida usipopata hedhi na hukujamiiana na mvulana, basi inawezekana ni mabadiliko tu ya mwili. Hali hii ikiendelea au ukiwa na wasiwasi unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya
Je, matokeo ya kupima na kukutwa huna virusi vya Ukimwi ni yapi?
Updated at: 2024-05-25 16:22:25 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa kawaida mtu anapoamua kwenda kupima mara nyingi anakuwa na sababu za kumfanya ahisi kuwa au kutokuwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Kwa hiyo mtu akipata jibu kuwa hana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, i itabidi ajiulize huo wasiwasi ulitokea wapi. Pale mtu anapojua ni kitu gani kilimfanya aende kupima, ni vyema mtu huyo kukaa mbali / kuacha kurudia hilo jambo au tabia i iliyomweka katika hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kwa mfano, kama alifanya ngono na mtu zaidi ya mmoja na kwa nyakati zote hakutumia kondomu. Baada ya kupima, mtu huyu anatakiwa aache tabia ya kuwa na wapenzi wengi na pia awe anatumia kondomu kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ni muhimu kuchukua tahadhari zote i ili kujikinga na maambukizi ya Virusi na UKIMWI na UKIMWI.
Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?
Updated at: 2024-05-25 16:24:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango. Unatakiwa kuanza kutumia huduma za afya ya uzazi pale unapoona unazihitaji. Na hasa iwapo umeamua kujamiiana, unatakiwa uende kwanza kwenye huduma za afya ya uzazi, na kupata ushauri juu ya ujinsia na masuala ya afya ya uzazi pamoja na njia mbalimbali za uzazi wa mpango. Vijana kisheria wamepewa haki ya kutumia njia za uzazi wa mpango. Nchini Tanzania kuna sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992.2 ambapo kati ya mambo mengine inalenga katika kuandaa vijana, kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa wawe wazazi wanaowajibika kwa kuinua kiwango cha elimu ya familia. Sera hii inazungumzia uanzishwaji wa huduma za afya ya uzazi ambayo itakidhi mahitaji ya vijana na inawahakikishia vijana kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi bila pingamizi katika umri wowote. Baadhi ya watu wanafikiri kuwa huduma za uzazi wa mpango ni kwa watu walio kwenye ndoa. Hii si kweli, mtu yoyote anaruhusiwa kutumia huduma za uzazi wa mpango na kupata njia mbalimbali za uzazi wa mpango. Vijana3 wanafaidika na kuwa na haki sawa kama watu wazima walio kwenye ndoa. Huduma za kinga kama vile ushauri juu ya mafunzo ya afya ya uzazi na vilevile kondomu ni njia za kuzuia mimba zinapatikana bure katika vituo vya afya vya serikali hapa Tanzania.