Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Katika miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua, mwanamke anayenyonyesha mtoto anapata kinga ya m...
Read More
Jinsi ya Kuepuka Kujihusisha na Ngono Kwa Shinikizo la Wenzako
Habari kijana! Leo tunajadi...
Read More
Wataalamu wanashauri kwamba msichana anastahili kuanza kubeba mimba kuanzia umri wa miaka 18 hadi...
Read More
Imani hiyo si kweli kabisa. Inawezekana ni kupotoshwa kwa
makusudi wa ukweli kuhusu jambo hi...
Read More
Ndiyo. Hapa Tanzania kuna kitengo maalumu kinachojishughulisha
na masuala ya akili. Wataalam...
Read More
Rafiki yako wa kike ana haki ya kukataa kujamiiana na wewe.
Labda hayuko tayari kujamiiana a...
Read More
Si kweli.
Pombe haiongezi damu, vitamini wala nguvu. Ukweli ni kwamba unywaji po...
Read More
Leo, tutazungumzia kuhusu mbinu za kuleta msisimko wa kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Ni...
Read More
Jinsi ya Kujenga Uaminifu katika Uhusiano wako na Msichana
Katika uhusiano wowote, uaminif...
Read More
Je, katika kujaribu fantasia za ngono/kufanya mapenzi pamoja na mwenza wako? Hii ni mada ambayo i...
Read More
Ndiyo, Kama nikotini, pombe huweza kukufanya mwenye busara
iwapo utakunywa, na ujiwekee kiwa...
Read More
Kuna i imani potofu kwamba wote wenye matatizo ya akili wamekuwa hivyo kutokana na matumizi ya da...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!