Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Featured Image

Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi
na njia za uzazi wa mpango. Unatakiwa kuanza kutumia huduma
za afya ya uzazi pale unapoona unazihitaji. Na hasa iwapo
umeamua kujamiiana, unatakiwa uende kwanza kwenye huduma
za afya ya uzazi, na kupata ushauri juu ya ujinsia na masuala
ya afya ya uzazi pamoja na njia mbalimbali za uzazi wa mpango.
Vijana kisheria wamepewa haki ya kutumia njia za uzazi wa
mpango.
Nchini Tanzania kuna sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992.2
ambapo kati ya mambo mengine inalenga katika kuandaa
vijana, kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa wawe wazazi
wanaowajibika kwa kuinua kiwango cha elimu ya familia.
Sera hii inazungumzia uanzishwaji wa huduma za afya ya uzazi
ambayo itakidhi mahitaji ya vijana na inawahakikishia vijana
kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi bila pingamizi
katika umri wowote.
Baadhi ya watu wanafikiri kuwa huduma za uzazi wa mpango ni
kwa watu walio kwenye ndoa. Hii si kweli, mtu yoyote anaruhusiwa
kutumia huduma za uzazi wa mpango na kupata njia mbalimbali
za uzazi wa mpango. Vijana3 wanafaidika na kuwa na haki sawa
kama watu wazima walio kwenye ndoa. Huduma za kinga kama
vile ushauri juu ya mafunzo ya afya ya uzazi na vilevile kondomu
ni njia za kuzuia mimba zinapatikana bure katika vituo vya afya
vya serikali hapa Tanzania.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Nifanyeje Kukabiliana na Mawazo yasiyofaa kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Mawazo yasiyofaa kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Mawazo yasiyofaa kuhusu Ngono? πŸ€”βœ‹

  1. Jua vipaumbele v... Read More

Nitafanya nini kuzuia dawa za kulevya na jinsi gani nitaepukana na marafiki wabaya?

Nitafanya nini kuzuia dawa za kulevya na jinsi gani nitaepukana na marafiki wabaya?

Wakati mwingine ni vigumu kusema hapana ukiwa na
maana ya hapana. Jaribu kuwa mpole na usiwe... Read More

Kwa nini watu wanaotumia dawa za kulevya mara nyingi hudanganya?

Kwa nini watu wanaotumia dawa za kulevya mara nyingi hudanganya?

Wengi wa waathirika wa dawa za kulevya hukataa matatizo yao. Hudanganya kwa sababu hawataki kukub... Read More

Uhusiano wa ubakaji na uvaaji wa nguo fupi?

Uhusiano wa ubakaji na uvaaji wa nguo fupi?

Ubakaji kamwe siyo kosa linalomhusu yeye aliyebakwa; ni kosa
linalomuhusu yeye aliyebaka. Un... Read More

Je, ni muhimu kwa washiriki wote kufikia kilele wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni muhimu kwa washiriki wote kufikia kilele wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni muhimu kwa washiriki wote kufikia kilele wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Wakati wa... Read More

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa ni ile ambayo mwanamume au mwanamke
anaozwa bila yeye mwenyewe kukubali... Read More

Je, mama anayenyonyesha mtoto anaweza kupata mimba?

Je, mama anayenyonyesha mtoto anaweza kupata mimba?

Katika miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua, mwanamke anayenyonyesha mtoto anapata kinga ya m... Read More

Jinsi mimba inavyopatikana

Jinsi mimba inavyopatikana

Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baada ... Read More

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kujihusisha na mambo ya kujamiiana?

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kujihusisha na mambo ya kujamiiana?

Kujamiiana ni uamuzi wa mtu binafsi. Ni uamuzi wako na hakuna
mtu yeyote mwenye haki ya kuku... Read More

Jinsi ya Kumvutia Msichana kwa Njia ya Kipekee

Jinsi ya Kumvutia Msichana kwa Njia ya Kipekee

Mtoto wa kike anapenda mambo mazuri na ya kipekee, kwa hivyo ikiwa unataka kumvutia msichana kwa ... Read More

Lengo na sababu ya kujamiiana

Lengo na sababu ya kujamiiana

Lengo kuu la kujamiiana ni kutafuta watoto. Lakini si sababu pekee. Sababu hizo ni pamoja na;

... Read More
Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kuna sababu kuu mbili i kwa wana ndoa kupata maambukizi i ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kw... Read More