Kizinda ni kiwambo laini kinachokuwepo ndani ya uke. Kiwambo hiki kina tundu katikati i i ili kuwezesha damu ya hedhi kupita kiurahisi. Ukubwa na unene wa kiwambo hiki hutofautiana kati ya msichana na msichana. Wakati wa tendo la kwanza la ngono, huchanika na kwa wengi i i inasababisha kutokwa damu. Lakini pia inawezekana kutokuwepo na tendo la kutokwa damu. Hii ni kwa sababu kiwambo hiki kina asili ya kunyumbuka sana na wakati mwingine tundu lake ni kubwa. Inawezekana pia kuwa kiwambo hiki tayari kilikuwa kimeharibiwa na sababu nyingine.
Read and Write Comments
Recent Comments