1000+ Vichekesho vipya: Vichekesho vya AckySHINE
Jinsi mzunguko wa elimu ulivyo
01.π Wale wanafunzi walioongoza
Mashuleni, wanaenda kwenye
Engineering na Medical school.
02.π Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa
wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.π Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia
Siasa na kuwaongoza wote hapo juu.
Yaani wa kwanza na wa pili.
04.π Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu
wote hawana raha.
05.π Wale waliopata Zero na waliokataa
shule wanakuwa waganga wa kienyeji,
wote hapo juu watamtafuta huyu, pale
mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake.
ππππππππππΏππΏπππππ
Chezea kufulia!
Huu Mwezi jinsi nilivyofulia yaani hata nikikuta mende wamesimama wawili najua wananisema
πππ
Angalia nilichomfanyia huyu dereva sasa
Tulikua kwa basi tunaelekea arusha,ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari, nikaenda kumziba macho nkamuulizaΒ otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana
NA SASA HIVI NIMEZINDUKA NIMEONA ABIRIA WOTE TUPO WODI NAMBA 3 HAPA KCMC MOSHI. π€π€π€π€
SODA ZA WAGONJWA PLIIIZ!!! πππππ
Kuwa na Binti aliyeacha shule
Kuwa na binti aliyeacha shule ni BALAA.
Anaweza kukuacha kwa staili ileile alotumia kuacha SHULE
π π π π π