Ujumbe wa kimahaba wa kumtumia mkeo mtarajiwa kumsifia alivyoumbika
Kila nikuonapo napata weweseko, yako miondoko si ya kitoto
na zaidi wajua kuweka mikogo, umeumbika si kitoto,
nahitaji uwe wangu mama watoto!
Kila nikuonapo napata weweseko, yako miondoko si ya kitoto
na zaidi wajua kuweka mikogo, umeumbika si kitoto,
nahitaji uwe wangu mama watoto!
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba, nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda,
macho nayaangaza,
taratibu navuta shuka na kujitanda,
mishumaa pembezoni inaniangaza,
mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa
ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako?
Nina huzuni moyoni sijui kwa kuwa siku hizi sikuoni,
naishia kukuota ndotoni,
hivi kweli nipo kwako moyoni? Nakupenda