SMS kwa mpenzi anayeishi mbali
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
Unaweza usione kamwe ni kwa kiasi gani ninavyokujali.
Unaweza usisikie ni kwa kiasi gani nilivyokushiba, unaweza
usihisi namna gani ninavyokukumbuka. Sababu ni moyo wangu
tu uliyoyaficha hayo.
Kila mtu anataka kuwa jua linalong’arisha maisha yako,
lakini ni afadhali niwe mwezi, ili nikuangazie wakati wa
giza ambapo jua limechwea na haliangazi tena.
Penzi, maisha yangu yote nimesoma juu ya neno hili,
nimeota juu yake, nimelilia, nimelihitaji. Sasa pamoja
nawe nimelipata.