Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Ndiyo, unaweza. Kifo kinaweza kuwa cha ghafla au
kutokana na madhara ya muda mrefu katika viungo vya
ndani ya mwili kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Watu wengi hufa katika ajali pale wanapokuwa wana kiasi kikubwa cha kilevi katika damu, kwani wanashindwa kutambua mazingira ya hatari.
Mtumiaji wa dawa za kulevya anaweza akafa ghafla kwa kile kinachoitwa kuzidisha dawa, pale mtu atakapotumia dawa za kulevya zaidi ya uwezo wa mwili. Kifo cha ghafla kinaweza kutokea au kutokana na matumizi ya kokaini na vifukishi kama petroli bila hata ya kuzidisha kiwango. Watumiaji wa vifukishi kama petroli mara nyingi hutumia mifuko ya plastiki i i ili kuongeza kiwango cha mvuke wanaovuta. Katika mazingira haya ni rahisi kupoteza fahamu kutokana na kukoseshwa hewa na mifuko hiyo. Kuchanganya baadhi ya dawa za kulevya kama vile heroini na dawa zingine hasa dawa za kutuliza maumivu (mfano valium) au pombe pia huweza kusababisha kifo.

Je, kuna madhara yoyote pale utakapojaribu kutumia dawa za kulevya mara moja tu au utakapotumia kwa kiasi kidogo sana?

Kutumia dawa za kulevya kwa kiasi kidogo kunaweza kusilete madhara i ila mpaka tu pale utakapoyazoea. Mara nyingi watu huanza kuhitaji dawa zaidi pale wanapozizoea na kupata madhara. Hii i ii inaweza kusababishia mtu kutawaliwa na dawa za kulevya. Mtumiaji wa dawa za kulevya anaweza kuwa mtegemezi wa dawa hizo bila ya kujijua. Kujaribu dawa za kulevya kunaweza kukawa na madhara kama “utaishia pabaya”. “Kuishia pabaya” ni jambo la kutisha na si la kufurahisha hata kidogo! Hali hiyo inaweza kutokea mara ya kwanza unapoanza kutumia bangi.

Madhara ya dawa za kulevya kwa mwili na ubongo

Moja kati ya vitu vinavyotisha kuhusu dawa za kulevya ni kwamba zinaathiri watu kwa njia mbalimbali na huwezi ukasema kwa uhakika jinsi zitakavyokuathiri. Madhara ya dawa za kulevya yanategemea aina, kiwango na jinsi zitakavyotumika. Vilevile inategemea na umri, afya ya mwili na ukomavu wa akili, na pia mazoea ya matumizi ya dawa hizo.
Madhara ya muda hutokea mara tu baada ya dawa za kulevya kutumika, wakati madhara ya muda mrefu huonekana baada ya muda kupita, na mara nyingi husababisha uharibifu wa kudumu kwenye mapafu na ubongo.

Kwa mfano, bangi, husababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo, matatizo ya kumbukumbu ya muda mfupi, pamoja na umakini, kujifunza, kufikiri na kutatua matatizo. Pia inaweza ikasababisha kasoro kwenye utaratibu wa viungo vya mwili. Mara kwa mara wavuta bangi huwa na macho mekundu. Na vijana wengine hupata mihemuko mbalimbali kama uoga na hofu baada ya matumizi ya bangi.
Dawa za kulevya za vichangamsho, kama mirungi na kokaini, inasemekana kuwa huwafanya watumiaji kuwa macho, kujiona wana nguvu na kujiamini. Vichangamsho vikitumika kwa wingi, humfanya mtumaji kujihisi kuwa na wasiwasi au hofu. Matumizi mabaya ya dawa za kulevya kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo ya akili au hata kifo i iwapo yatatumika kwa kiwango cha juu.
Dawa za kulevya zinazokufanya upooze kama heroini au dawa nyingine zinazoagizwa na daktari, husababisha kujisikia umetulia, una amani na furaha. Ukizidisha vipimo husababisha usingizi, upungufu wa umakini na uwezo wa kuona, kizunguzungu, kutapika na kutokwa jasho. Vilevile kipimo kingi kinaweza kusababisha usingizi wa muda mrefu, kuzimia na hata kifo.

Pombe za kienyeji kama gongo ni hatari kwa afya na zinaweza kusababisha upofu na hata kifo.
Matumizi ya dawa za kulevya hupunguza uwezo wa vijana kuhimili na kutatua matatizo yao ya kijamii na kiakili. Hii husababisha vijana kuwa wepesi kujihusisha na ujambazi na mambo ya ngono na ugomvi, mabadiliko hayo ya tabia husababisha ugomvi katika familia na kuvunjika kwa urafiki. Matumizi ya dawa za kulevya ndiyo sababu kubwa ya ajali za barabarani, kujiua na maambukizo mbalimbali.

Tofauti ya VVU na UKIMWI

Neno VVU ni i virusi au vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI. Neno hili kwa lugha ya Kii ngereza ni HIV yaani “Human Immunodeficiency Virus”. UKIMWI ni kifupi cha maneno matatu ambayo ni Upungufu wa Kinga Mwilini. Kwa Kii ngereza jina la UKIMWI AIDS ambacho kirefu chake ni “Acquired Immune Deficiency Syndrome”. Neno UKIMWI tayari linaonyesha tayari aina ya ugonjwa, i ikii manisha kuwa mwili umepungua uwezo wake wa kinga kwa maradhi mbalimbali mwilini. Dalili za upungufu huu ukianza kujitokeza basi maradhi haya huitwa UKIMWI.

Tofauti kati ya VVU na UKIMWI ni kuwa mtu aliyeambukizwa VVU bado anaweza kuonekana mzima wa afya. Pamoja na kuwa virusi hivyo vitaonenekana katika damu yake, ni kwamba virusi hivyo vitakuwa havijaanza bado kushambulia chembechembe nyeupe za damu. Kwa upande mwingine kinga ya mwili ya mtu anayeumwa UKIMWI i itakuwa tayari i i imepungua. Mwili wake utaanza kuugua magonjwa nyemelezi. Magonjwa nyemelezi hupata nafasi ya kushambulia mwili huu ambao tayari kinga imepungua. Watu wnaoumwa UKIMWI wanaweza kupungua uzito wa mwili, kuharisha au kupata matatizo ya ngozi. Hata hivyo maradhi haya siyo lazima yatokane na kuwa na VVU. Ili kuwa na uhakika, onana na mtaalamu yaani dakatari wako.

Sababu za matumizi ya dawa za kulevya

Zipo sababu nyingi zinazowafanya watu kutumia dawa za kulevya, nazo ni kama zifuatazo:
Watu wengi hutumia dawa wakitumaini kusahau matatizo yanayowakabili, wengine hutumia kama viburudisho na wanataka kujionyesha kwamba ni watu wazima na wenye nguvu. Wengine pia huanza kutumia dawa kiutani na hatimaye hushindwa kujizuia kuzitumia. Wengine hutumia kutokana na msukumo wa rika au kutokana na kushawishiwa na watu wengine kwamba dawa za kulevya huwapa raha. Wengine hutumia kutokana na ukali wa maisha, uchovu pamoja na upweke. Kimsingi, dawa za kulevya hazimpatii mtu ufumbuzi wa matatizo, bali humwongezea matatizo mtumiaji.

Shopping Cart