Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, watu wote wenye virusi vya UKIMWI watapata UKIMWI? Na kama ndiyo, itachukua muda gani?

Ndiyo, baada ya muda fulani karibia watu wote wenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI wataanza kuugua UKIMWI. Lakini muda kati ya kuambukizwa na kuanza kuugua UKIMWI unatofautiana. Wengine wanaishi muda mrefu. Kwa wastani watu wazee wazima wanaendelea kuishi miaka kumi kabla ya kupata dalili za awali. Watoto wanaopata virusi kabla ya umri wa miaka mitano kwa wastani wanendelea kuishi mwaka moja hadi mitatu.
Hakuna jibu la ujumla ni miaka mingapi ataishi tena mtu aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI. Idadi ya miaka ya kuishi baada ya kuambukizwa i inategemea vitu vingi, kinga asilia i inayomkinga mtu, hali ya lishe ya mtu, wakati muafaka na usahihi katika kutibu magonjwa nyemelezi na wakati muafaka na usahihi wa kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kwa Kiingereza Anti-Retro-Viral drugs (ARVS )

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Virusi hivi vinakaa katika chembechembe nyeupe zilizopo kwenye majimaji ya mwili i wa binadamu hasa kwenye damu, shahawa na maji maji ya ukeni na maziwa ya mama anayenyonyesha. Ndani ya chembechembe nyeupe ndiyo mahali virusi vinakaa na kuendelea kuzaliana. Vikiwa ndani ya chembechembe nyeupe hizi, virusi huendelea kuzaliana hadi kusababisha chembechembe nyeupe hizi kupasuka.

Virusi hivi hupata nafasi ya kuendelea kushambulia chembechembe nyingine nyeupe za damu. Kwa kadri chembechembe nyeupe zilizoshambuliwa zinavyoendelea kupasuka ni kwa kiwango hicho hicho chembechembe nyeupe zinaendelea kuharibiwa na kupungua. Matokeo yake ni kupungua kwa kinga mwilini na mtu kuendelea kudhoofika.

Kinga ya mwili ni nini?

Kinga ya mwili ni mpangilio wa mwili kujikinga na maradhi. Chembechembe nyeupe zilizopo katika damu ya mwili mzima wa binadamu zina kazi maalum katika kuhakikisha kinga ya mwili i i ipo. Kama askari jeshi wanaolinda nchi yao, chembechembe hizo kwa pamoja zinalinda mwili dhidi ya magonjwa. Hivyo, kama chembeche-mbe hizo zikishambuliwa, mwili hauwezi kujikinga na maradhi au magonjwa.

Nitafanya nini kuzuia dawa za kulevya na jinsi gani nitaepukana na marafiki wabaya?

Wakati mwingine ni vigumu kusema hapana ukiwa na
maana ya hapana. Jaribu kuwa mpole na usiwe mgomvi.
Jaribu kueleza sababu zako kwa upole na uwaeleze rafiki zako kile unachokijua na nini unachofanya. Hivyo utapata heshima kutoka kwa wanarika wenzako na rafiki zako. Kama vijana wenzako watakushawishi utumie dawa za kulevya wakati wewe hutaki, wanaweza kuwa marafiki wabaya. Kumbuka kwamba rafiki ni mtu ambaye anajali, analinda na kuthamini maisha ya rafiki yake. Kwa maana hiyo, kwa nini mtu anayekushawishi kwa makusudi kufanya kitu chenye madhara kwa afya yako awe rafiki wa kweli?!

Shopping Cart