Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kujenga Familia Bora: Njia za Kuifanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee

Jinsi ya Kujenga Familia Bora: Njia za Kuifanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee

Jinsi ya Kujenga Familia Bora: Njia za Kuifanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee

Familia ni se... Read More

Njia za Kujenga Ushirikiano na Kupata Amani na Furaha katika Familia Yako

Njia za Kujenga Ushirikiano na Kupata Amani na Furaha katika Familia Yako

Karibu katika makala hii ambapo tutajadili njia za kujenga ushirikiano, amani, na furaha katika f... Read More

Je, kuna umuhimu wa ngono/kufanya mapenzi unabadilika wakati wa mzunguko wa maisha?

Je, kuna umuhimu wa ngono/kufanya mapenzi unabadilika wakati wa mzunguko wa maisha?

Habari za leo wapenzi wangu! Nami nina furaha sana kuwa hapa leo kuongelea kuhusu swala la ngono ... Read More

Njia za Kukuza Shukrani na Kutambua Maana ya Ndoa

Njia za Kukuza Shukrani na Kutambua Maana ya Ndoa

Ndoa ni moja ya hatua kubwa na ya kipekee katika maisha ya kila mtu. Ni wakati wa kujitolea kwa m... Read More

Jinsi ya Kufanya Familia kuwa Kitovu cha Upendo na Ukarimu

Jinsi ya Kufanya Familia kuwa Kitovu cha Upendo na Ukarimu

Kufanya familia kuwa kitovu cha upendo na ukarimu ni jambo la muhimu sana katika jamii yetu. Fami... Read More

Jinsi ya Kusimamia tofauti za maoni na migogoro katika uhusiano wa mapenzi

Jinsi ya Kusimamia tofauti za maoni na migogoro katika uhusiano wa mapenzi

Kusimamia tofauti za maoni na migogoro ni sehemu muhimu ya kujenga uhusiano wa mapenzi wenye afya. H... Read More
Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Familia

Kuendeleza ushirikiano katika familia ni muhimu sana kwa ustawi wa kila mwanafamilia. Kwa kufanya... Read More

Jinsi ya kuimarisha furaha na ustawi wa kihisia na mke wako

Jinsi ya kuimarisha furaha na ustawi wa kihisia na mke wako

Kuimarisha furaha na ustawi wa kihisia katika ndoa ni muhimu sana kwa uhusiano mzuri na wenye afya n... Read More
Jinsi ya Kujenga Mazingira ya Kujifurahisha na Burudani katika Familia Yako

Jinsi ya Kujenga Mazingira ya Kujifurahisha na Burudani katika Familia Yako

Hakuna jambo muhimu kama familia. Familia ni mahali pa kujifunza, kujifurahisha, na kupata upendo... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuunga Mkono Ndoto za Mwenzi wako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuunga Mkono Ndoto za Mwenzi wako

Mwenzi wako ni rafiki yako wa karibu na mtu anayekuaminu sana. Kwa hivyo, ni muhimu kuwa na ushir... Read More

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Kwa wengi, ngo... Read More

Jinsi ya Kupenda na Kuwaunga Mkono Watoto wa Kambo: Kuleta Umoja katika Familia

Jinsi ya Kupenda na Kuwaunga Mkono Watoto wa Kambo: Kuleta Umoja katika Familia

Kupenda na kuwaunga mkono watoto wa kambo ni muhimu sana kwa ustawi wa familia. Watoto wa kambo w... Read More