Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ujasiri na kujiamini

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ujasiri na kujiamini

Kuwa na ujasiri na kujiamini ni muhimu katika mahusiano, lakini mara nyingine tunaweza kukosa uja... Read More

Kusisimua Hisia katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuchochea Hamu na Ushirikiano

Kusisimua Hisia katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuchochea Hamu na Ushirikiano

Kusisimua Hisia katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuchochea Hamu na Ushirikiano

Mapenzi ni h... Read More

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Ushirikiano katika Familia

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Ushirikiano katika Familia

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Ushirikiano katika Familia

Familia ni kiini cha jamii,... Read More

Kuishi na Tofauti za Kijinsia katika Uhusiano: Kuelewa na Kuheshimu

Kuishi na Tofauti za Kijinsia katika Uhusiano: Kuelewa na Kuheshimu

Kuishi na Tofauti za Kijinsia katika Uhusiano: Kuelewa na Kuheshimu

  1. Kuelewa Tofa... Read More

Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?

Jambo la faragha kabisa ni ngono au kufanya mapenzi. Kila mtu ana hisia tofauti kuhusu suala hili... Read More

WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI

WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI

1.Hachezi mbali na simu yake kila wakati.
2.Inbox na sending items hufutwa kila wakati.
Read More

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Kwa wengi, kufanya ma... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kiroho katika Mahusiano: Kuungana kwa Kiimani

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kiroho katika Mahusiano: Kuungana kwa Kiimani

  1. Kutafuta jambo la pamoja: Uhusiano wa kiroho unahitaji kuwa na jambo la pamoja ambalo linaw... Read More
Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu kwenye blogi hii ambapo tutazungumzia kuhusu mbinu za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufa... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu aina mbalimbali za ngono/kufanya mapenzi kama vile BDSM?

Je, watu wanapendelea kujaribu aina mbalimbali za ngono/kufanya mapenzi kama vile BDSM?

Leo tutazungumzia kuhusu kwa nini watu wanapendelea kujaribu aina mbalimbali za ngono/kufanya map... Read More

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu katika Mahusiano ya Kimapenzi

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu katika Mahusiano ya Kimapenzi

Mahusiano ya kimapenzi yanaweza kuwa na changamoto nyingi, lakini jambo moja muhimu ni kuwa na us... Read More

Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

1. Ukija kijiweni au pub au kwenye nyama choma acha zile stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, s... Read More