Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisaβ¦. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeyeβ¦β¦
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatokaβ¦ sorry bae sitaweza kuja kwa leoβ¦ sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kituβ¦..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”
#dada wa watu mashavu yakamshukaβ¦ hakuamini kilichotokeaβ¦. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwaβ¦β¦
Recent Comments