Mambo ya Muhimu kujua kuhusu dhambi

Dhambi ya asili ndio nini?
Dhambi ya asili ambayo binadamu wote wanazaliwa nayo, ni hali ya kukosa utakatifu na hali ya asili ya urafiki na Mungu


Adhabu gani walipewa Adamu na Eva?
Adamu na Eva kwa ukubwa wa dhambi yao ya kiburi na ya uasi:
1. Walipoteza neema ya utakaso
2. Walifukuzwa paradisini
3. Walipungukiwa akili na kushikwa na tamaa ya kutenda dhambi
4. Walipitia mahangaiko na taabu nyingi
5. Kupaswa kufa. (Mwa 3:16-20: 5:5)


Kisha kosa la Adamu na Eva Mungu aliahidi nini?
Kisha kosa la Adamu na Eva Mungu aliahidi kuwaletea Mkombozi. (Mwa 3:15)


Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili maana yake ni nini?
Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili maana yake hakuzaliwa na dhambi ya asili kama binadamu wengine


Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?
Kwa nini dhambi zipo?
Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani.
β€œMimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu… Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo” (Mwa 45:4-5; 50:20).


Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?
Ndiyo, Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi, lakini aliwaacha watende kwa hiari yao awaonyeshe ukuu wa huruma yake.
β€œMaana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote” (Rom 11:32).


Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?
Hapana, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu kwa kuvutwa na mashetani, yaani malaika waliokataa moja kwa moja kumtumikia; baada ya dhambi ya asili hao wanatutumia sisi pia tuangushane na wenzetu.
Lakini Mungu aliwahi kumuambia Shetani:
β€œNitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako, na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwa 3:15).
β€œHata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4).


Je, dhambi zote zinahusiana?
Ndiyo, dhambi zote zinahusiana kwa sababu dhambi zinazaa dhambi nyingine ndani mwetu na katika mazingira yetu.
β€œHamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya” (1Kor 5:6-7).


Dhambi zimetuathiri vipi tena?
Dhambi zimetuathiri kwa ndani zaidi, zikitutia udhaifu katika mwili, ujinga katika akili na uovu katika utashi; madonda hayo yanatufanya tuzidi kushindwa.
β€œKwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii” (Rom 8:7).


Katika unyonge wetu tutumainie nini?
Katika unyonge wetu tutumainie huruma ya Mungu aliyetutumia Mkombozi hata β€œdhambi ilipozidi, neema ikawa kubwa zaidi” (Rom 5:20).
Ushindi wake juu ya dhambi umetupatia mema makubwa kuliko tuliyoyapoteza kwa dhambi.
β€œMungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu; alituuhisha pamoja na Kristo; yaani, mmeokolewa kwa neema” (Ef 2:4-5).


Yesu ni Mungu au mtu?
Yesu ni Mungu na mtu kwa pamoja, ndiyo sababu ni mshenga pekee kati ya Mungu na watu. β€œKwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu” (1Tim 2:5). β€œKatika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol 2:9). Hivyo ni Mungu kweli na mtu kweli.
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.
6 Mtu mmoja aitwaye Yohana alitumwa na Mungu 7 awaambie watu kuhusu hiyo nuru, ili kwa ushuhuda wake wapate kuamini. 8 Yohana mwenyewe hakuwa ile nuru. Yeye alitumwa kuishuhudia hiyo nuru. 9 Nuru halisi ambayo inawaangazia watu wote ilikuwa inakuja ulim wenguni. 10 Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua! 11 Alikuja nyumbani kwake, lakini watu wake hawakumpokea! 12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: β€œHuyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, β€˜Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.”’ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu. Yohana 1:1-6:37


5 Tomaso akamwuliza, β€œBwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?” 6 Yesu akawaam bia, β€œMimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”
8 Filipo akamwambia Yesu, β€œBwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.” 9 Yesu akamjibu, β€œFilipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, β€˜Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. Yohane 14:5-10


29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, β€œNimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, β€œTunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.” Yohane 10: 29-33


Yesu anapatikana wapi? Yesu anakaa wapi? Yesu Yupo wapi kwa sasa?
Yesu kama Mungu yupo kila mahali, hakuna mahali asipokuwepo. Yesu kama mwanadamu yupo Mbinguni kwa Baba na anakaa nasi duniani katika Maumbo ya Mkate na Divai Katika Ekaristi.


Kwa nini Yesu alishawishiwa/alijaribiwa na Shetani?
Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, β€œhata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Fil 2:8).
β€œKwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” (Rom 5:19).


Kwa nini Yesu aliteswa hadi kuuawa msalabani?
Yesu aliteswa hadi kuuawa msalabani ili abebe kwa upendo na kufidia dhambi za watu wote, alivyotabiriwa:
β€œTulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona” (Isa 53:4-5).
Tangu mwanzo Wakristo wanakiri kwa ufupi kwamba,
β€œKristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko” (1Kor 15:3).
β€œAlijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema” (Tit 2:14).
β€œAlijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote” (1Tim 2:6).
β€œIli kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa” (Eb 2:14-15).


Je, Kanisa linaweza kutuondolea dhambi yoyote?
Ndiyo, Kanisa linaweza kutuondolea dhambi yoyote katika ubatizo na kitubio kwa kutumia mamlaka ambayo Yesu mfufuka aliwashirikisha Mitume wake alipowavuvia akisema:
β€œPokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa” (Yoh 20:22-23).
β€œMlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu” (1Kor 6:11).


Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu gani?
Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu alijua udhaifu wa binadamu hauishi mara anapopokea uzima wa Mungu kwa sakramenti tatu za kuingizwa katika Ukristo. Hivyo alipanga kusaidia mpaka mwisho wa dunia waamini wake watakaopatwa na dhambi na ugonjwa, kama alivyowasaidia wengi aliokutana nao katika maisha yake.
β€œYesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, β€˜Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako’… β€˜Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi’ – amwambia yule mwenye kupooza – β€˜Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako’. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii” (Math 9:2,6-8).


Mungu aliwapa watu (mapadri) amri/uwezo ya kusamehe dhambi kwa njia ya nani? Ni halali kuungama kwa padre?
Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa njia ya Mwanae. Yesu mfufuka aliwaonyesha Mitume alama ya mateso mwilini mwake, β€œakawavuvia, akawaambia, β€˜Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa” (Yoh 20:22-23).
Katika Kanisa tunafurahi kupewa msamaha wa dhambi kila tunapohitaji, mradi tutubu. Kwa njia ya mwandamizi wa Mitume, Yesu anatuambia,
β€œUmesamehewa dhambi zako… Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani” (Lk 7:48,50).
Si dhana wala hisia tu, bali ni neno la hakika tunalolipokea kwa masikio yetu.


Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi zipi?
Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi zote, kwa sababu upendo mtiifu wa Mwanae aliyejitoa kuwa sadaka ya wokovu wetu unampendeza kuliko dhambi zote zinavyomchukiza. Ila hatuwezi kusamehewa dhambi ya kukataa neema ambayo Roho Mtakatifu anatusukuma tuamini na kutubu, kwa sababu pasipo imani na toba hapana msamaha.
β€œKila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa” (Math 12:31).
β€œNasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure” (2Kor 6:1).


Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa sababu gani?
Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa sababu amependa washiriki katika kazi zake. Ametuumba kwa njia ya wazazi na kutulea na kutusaidia kwa njia ya wengine pia. Hasa ametuokoa kwa njia ya Yesu, ambaye yupo nasi sikuzote katika Mwili wake, yaani Kanisa, na katika wale walioshirikishwa mamlaka ya Mitume.
β€œLakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo: mpatanishwe na Mungu” (2Kor 5:18-20).


Je, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi?
Ndiyo, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi tulizotenda baada ya ubatizo, kwa kuwa hatuwezi kupokea msamaha tukikataa masharti yake, na Mungu ametupangia watu ambao watuondolee kwa niaba yake.
β€œWatu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohane. Lakini, Mafarisayo na wanasheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye” (Lk 7:29-30).
Yesu mwenyewe alikubali kubatizwa na Yohane ili atimize mpango wa Baba.
β€œYohane alitaka kumzuia, akisema, β€˜Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?’ Yesu akajibu akamwambia, β€˜Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Math 3:14-15).
Je, sisi tukatae kumkimbilia padri wa Mungu ili kupokea huruma yake tunayoihitaji kuliko hewa?


Tumuungamie padri dhambi zetu kwa lengo gani? Kwa nini Wakatoliki wanaungama kwa padri?
Tumuungamie padri dhambi zetu ili aweze kutushauri na kuamua kama tuko tayari kuondolewa. Tumweleze kwa unyofu makosa yote tuliyoyafanya na nia tuliyonayo ya kuyafidia na kutoyarudia.
β€œTukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo, wala neno lake halimo mwetu” (1Yoh 1:8-10).
Tukumbuke tulivyo viungo vya Mwili mmoja, hivi kwamba dhambi zetu zimewadhuru wenzetu. β€œUngameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana, mpate kuponywa” (Yak 5:16).
Kutokuwa tayari kufanya hivyo walau sirini kwa padri ni dalili ya kiburi na ya kutotubu.


Je, padri akiwa mkosefu, anaweza kutuondolea dhambi?
Ndiyo, padri akiwa mkosefu, anaweza kutuondolea dhambi kwa niaba ya Mungu aliyempa mamlaka hiyo. Hatusamehewi na utakatifu wa padri, bali na huruma ya Baba kwa njia yake.
Yeye anamtumia padri yeyote ili kuturahisishia kazi, tusihitaji kuchunguza kwanza ubora wa maisha yake, wala kwenda mbali tukampate mmoja asiye na dhambi. Tungefanyeje kuhakikisha ni mtakatifu, wakati hatuwezi kusoma moyo wake? Ingekuwa hivi, tusingepata kamwe hakika ya kusamehewa. Kumbe inatutosha kujua ni padri, kwamba Mungu amempa mamlaka ya kusamehe dhambi, kama Yesu alivyowapa Mitume siku tatu baada ya kumkimbia na hata kumkana. Kila padri anaweza kukiri,
β€œNi neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa: ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi, ambao wa kwanza wao ni mimi” (1Tim 1:15).
Amri ya kusamehe dhambi wamepewa watu, si malaika.
β€œTuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu” (2Kor 4:7).


Je, nje ya kitubio tunaweza kuondolewa dhambi tuliyotenda baada ya ubatizo?
Ndiyo, nje ya kitubio tunaweza kuondolewa dhambi tuliyotenda baada ya ubatizo, lakini ni vigumu zaidi, kwa sababu hatupati msaada wa sakramenti hiyo maalumu.
Pamoja na nia ya kumuungamia padri mapema tunahitaji neema ya kutubu kikamilifu, si kwa kuhofia adhabu, bali kwa kumpenda Mungu tuliyemchukiza.
β€œAmesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana” (Lk 7:47).


Dhambi za uchafu huleta hasara gani?
Huleta hasara hizi;
1. Kuharibu usafi wa Moyo na Hekalu la Mungu
2. Huleta Magonjwa duniani na hasara ya baadae. mf UKIMWI. (Efe 5:5)
3. Huvunja amani ya familia
4. Kujijengea mazoea ya uchafu


Mambo yanayomzuia mtu kuishi maisha mema ni yapi?
Mambo hayo ni;
1. Dhambi
2. Vilema
3. Vishawishi


Dhambi ni nini?
Dhambi ni kosa la Mtu mwenye kuvunja Amri ya Mungu au ya Kanisa kwa mawazo (tamaa), kwa maneno au kwa matendo


Je kuna aina tofauti ya dhambi?
Ndiyo, kuna dhambi za mawazo, maneno, matendi na kutotimiza wajibu.


Dhambi zinatofautianaje katika uzito?
Kuna:
1. Dhambi ya Mauti (Dhambi kubwa) na
2. Dhambi nyepesi (Dhambi ndogo)


Dhambi ya mauti ni nini?
Dhambi ya Mauti ni kosa la kuvunja Amri ya Mungu au ya Kanisa, katika jambo kubwa, kwa fahamu na kusudi. (1 Yoh 5:16)


Dhambi ya Mauti hutupotezea nini?
Dhambi ya Mauti hutupotezea;
1. Upendo ndani mwetu
2. Neema ya Utakaso


Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti huenda wapi?
Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti hutupwa motoni milele. (Mt 25:41)


Dhambi nyepesi ni nini?
Dhambi nyepesi ni kosa la kuvunja Amri ya Mungu au ya Kanisa katika jambo dogo, au jambo kubwa kwa makusudi yasiyo kamili. (1 Yoh 5:17)


Dhambi nyepesi hutupotezea nini?
1. Hudhoofisha upendo ndani mwetu
2. Huzuia Maendeleo ya roho zetu kwa kuzuia fadhila na kutenda mema.


Adhabu ya dhambi ndogo ni nini?
Adhabu ya dhambi ndogo ni mateso duniani na Toharani


Je, Tunawajibika kwa dhambi zilizotendwa na wengine?
Ndiyo, Tunawajibika kwa dhambi zilizotendwa na wengine iwapo tunazichangia kwa kutenda kosa husika.
Mfano Utoaji wa Mimba, anayetolewa, anayetoa, anayeshauri na aliyejua lakini hakuzuia wote wanatenda dhambi.


Dhambi zinazomlilia Mungu ni zipi?
Dhambi zinazomlilia Mungu ni;
1. Kuua Binadamu, Mfano Kaini na Abeli
2. Ulawiti na ushoga. (Wag 5:18-21)
3. Kilio cha wanaogandamizwa
4. Kilio cha mgeni, mjane, yatima na walemavu
5. Kukosea haki waajiriwa.


Sakramenti ya Kitubio ni nini?
Sakramenti ya Kitubio ndiyo Sakramenti ya kuwaondolea watu dhambi walizotenda baada ya Ubatizo (Yoh 20:22-23)


Lini na kwa maneno gani Yesu aliweka Sakramenti ya Kitubio?
Yesu aliweka Sakramenti ya Kitubio jioni ya ufufuko wake alipowapulizia mitume na kuwaambia maneno haya “Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi watakua wameondolewa, wowote mtakaowafungia dhambi watakua wamefungiwa” (Yoh 20:22-23)


Mwenye kuwaondolea watu dhambi ni nani?
Mwenyezi Mungu pekee yake aweza kuwaondolea watu dhambi. Ndiye aliyewapa Mitume, Maaskofu na Mapadri uwezo wa kuwaondolea watu dhambi (Yoh 20:21-23)


Nani yampasa kupokea Sakramenti ya Kitubio?
Kila mkristo aliyetenda dhambi yampasa kupokea Sakramenti ya Kitubio


Mkristo akitaka kupokea Sakramenti ya Kitubio yampasa nini?
Mkristo akitaka kupokea Sakramenti ya Kitubio yampasa haya
1. Kutafuta dhambi moyoni (Yoh 3:20-21)
2. Kujuta dhambi
3. Kukusudia kuacha dhambi
4. Kuungama kwa padre
5. Kutimiza malipizi
6. Kumshukuru Mungu aliyemwondolea dhambi


Wakati wa Sakramenti ya Kitubio Utamwomba Roho Mtakatifu kwa sala gani?
Utamuomba Roho Mtakatifu kwa sala hii:
Uje Roho Mtakatifu unisaidie nitambue dhambi zangu, nijute sana, niungame vema, nipate kutubu kweli. Amina


Kutafuta dhambi maana yake ni nini?
Kutafuta dhambi maana yake ni kujiuliza moyoni dhambi nilizotenda Tangu ungamo la mwisho (Ef 4:17-32)


Utafuteje dhambi wakati wa kujiandaa kuungama?
Tafuta dhambi kwa njia hizi
1. Kwa kukumbuka uliyokosa kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo
2. Katika Amri za Mungu na za Kanisa
3. Katika vichwa vya dhambi
4. Katika kutimiza wajibu


Kutubu dhambi maana yake ni nini?
Kutubu dhambi maana yake ni kuona uchungu na chuki moyoni juu ya dhambi tulizotenda na kukusudia kutotenda dhambi tena (Yoh 8:11)


Kwa nini tujute dhambi zetu?
Tunajuta dhambi zetu kwa sababu tumeukosea Utatu Mtakatifu na tunastahili adhabu yake, na pia bila majuto hatuwezi kupata maondoleo ya dhambi.


Kuna majuto ya namna ngapi?
una majuto ya namna mbili,
1. Majuto kamili/Majuto ya mapendo
2. Majuto yasiyokamili/majuto pungufu/majuto ya hofu


Majuto kamili ni nini?
Majuto kamili ni kujuta kwa sababu tumemchukiza Mungu mwenyewe aliye mwema na mpendelevu kabisa


Majuto yasiyo kamili au majuto pungufu ni nini?
Majuto yasiyokamili ni kujuta kwa sababu tumepoteza furaha za Mbinguni na tunahofia adhabu ya Mungu


Asiyejuta aweza kuondolewa dhambi?
Asiyejuta hawezi kuondolewa dhambi kabisa, na anayeungama bila kujuta anatenda dhambi kubwa ya kufuru.


Kabla ya kuungama ni lazima kufanya nini?
Kabla ya kuungama ni lazima kukusudia kuacha dhambi na kuepuka nafasi kubwa ya dhambi bila kusahau kufuata hatua sita za kabla na baada ya kupokea kupokea Sakramenti ya Kutubio ambazo ni,
(1) kuwaza/kutafuta dhambi moyoni,
(2)kutubu/ kujuta,
(3)kukusudia kuacha dhambi,
(4)kuungama kwa padri,
(5)kutimiza kitubio,
(6)kumshukuru Mungu


Anayetaka kweli kuacha dhambi afanye nini?
Anayetaka kuacha dhambi afanye nguvu kuvishinda vishawishi, asali/aombe na apokee Sakramenti Mara nyingi hasa Sakramenti ya Kitubio na Ekaristi Takatifu.


Kuungama ni kufanya nini?
Kuungama ni kumwambia Padri wazi wazi dhambi zako ulizotenda, zipi na ngapi ili upate maondoleo.


Anayeficha kusudi dhambi ya mauti katika ungamo anaondolewa?
Haondolewi, Bali anatenda dhambi kubwa ya kukufuru Sakramenti ya Kitubio. (Mt 7:21-23, Yoh 20:23, Gal 6:7)


Anayekufuru Sakramenti ya Kitubio yampasa nini?
Yampasa kuziungama tena dhambi zake zote alizotenda tangu ondoleo la mwisho


Padri anaondolea dhambi mahali pa nani?
Padri anaondolea dhambi mahali pa Mungu


Padri anaondolea dhambi kwa maneno gani?
Padre anaondolea dhambi kwa maneno haya: Nami “Nakuondolea dhambi zako zote kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu”.


Kitubio tuwezacho kupewa na padre ni nini?
Kitubio tuwezacho kupewa na Padre ni kama sala, kufunga, kutoa sadaka kwa maskini, kusoma maandiko matakatifu, kuwatazama wagonjwa, n.k.


Kitubio tupewacho na padre chatosha?
Ni shida kutosha. Mara nyingi chataka malipizi ya hapa duniani kama kufunga, magonjwa, masumbuko, sala n.k mateso yasipotosha hapa duniani yatakamilishwa toharani


Kutimiza malipizi maana yake ni ni nini?
Kutimiza malipizi maana yake ni kutekeleza kiaminifu sala au matendo aliyotuagiza padre muungamishi ili kulipa adhabu za muda. (Rom 8:17)


Kwa Sakramenti ya Kitubio tunapata neema zipi?
Kwa Sakramenti ya Kitubio tunapata neema hizi;
1. Maondoleo ya dhambi zote kubwa na adhabu ya milele
2. Maondoleo ya dhambi ndogo na adhabu nyingine za muda (Isa 6:5-7, Yoh 8:11)
3. Twarudishiwa na kuongezewa neema ya utakaso
4. Twasaidiwa kuepa dhambi na twapata nguvu ya kutenda mema
5. Twarudishiwa tena mastahili tuliyopoteza kwa dhambi zetu


Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi rohoni anatenda dhambi gani?
Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi anatenda dhambi kubwa yaani kufuru Sakramenti.
26 Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana. (1 Kor 11;26 – 27)
28Basi, kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho; 29 maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana, anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe. 30 Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine kadhaa wamekufa. 31 Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo. 32Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. (1 Kor 11;28 – 32)

Mambo ya Msingi unayotakiwa kufahamu kuhusu Sakramenti ya Daraja

Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu gani?
Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu hazilengi hasa faida ya mtu anayezipokea, bali huduma zake kwa ajili ya Kanisa na jamii. Daraja inatia uwezo wa Kristo kwa ustawi wa Kanisa, Bibi arusi wake. Ndoa inatia upendo wake mwaminifu kwa ustawi wa familia, kanisa dogo la nyumbani.
β€œJitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe” (Mdo 20:28).
β€œHakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa” (Ef 5:29-32).


Je, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa?
Ndiyo, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa kwa sababu kazi ya wokovu haimtegemei binadamu, bali Mungu.
β€œHapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” (Eb 5:4-5),
Yesu alisisitiza alivyopewa na Baba uwezo wa kutuokoa. β€œBaba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake” (Yoh 3:35).
β€œKama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” (Yoh 17:2)
.
Kisha kufufuka alitumia mamlaka hiyo kuwatuma wanafunzi kumi na mmoja waliobaki:
β€œNimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18-20).
Mpaka mwisho wa dunia uwezo huo wa Kimungu utatolewa tu kwa sakramenti ya daraja, inayounganisha mtu na Mitume kupitia mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono ili kushirikishwa mamlaka. Bila yake, kuna upungufu katika ufundishaji, utoaji wa sakramenti na uongozi.


Je, wenye daraja wanastahili heshima?
Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo.
β€œAmin, amin, nawaambieni: Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenipeleka” (Yoh 13:20).
β€œJaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu” (Gal 4:14).
β€œUwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii” (Tito 3:1).
Wenye daraja wanaotimiza kazi zao vizuri wanastahili heshima kwa uaminifu wao pia.
β€œWazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa hao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha” (1Tim 5:17).


Je, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi?
Ndiyo, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi kwa sababu ni binadamu kama sisi sote. Yesu alionja ukosefu wa Mitume hasa wakati wa mateso.
β€œJe, mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?” (Yoh 6:70).
β€œTazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao, na kuniacha mimi peke yangu” (Yoh 16:32).
Paulo alionya mapadri, β€œKatika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao” (Mdo 20:30).


Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa kufanya nini?
Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa hasa kusali.
β€œMwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake” (Math 9:38).
Halafu yanahitajika maandalizi ya muda mrefu, juhudi na ushirikiano wa kidugu.
β€œAsiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi… Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia… Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine” (1Tim 3:6; 4:16; 5:22).


Je, wanawake wanaweza kupewa daraja?, Mwanamke anaweza kuwa padri?
Hapana, wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua wanaume tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa Maria, mtakatifu kuliko wote.
β€œPetro, na Yohane, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake… Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya… kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja” (Mdo 1:13-14,23,26).
β€œWalimchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao” (Mdo 6:5-6).


Je, kutoa daraja kwa wanaume tu ni kuwakosea haki wanawake?
Hapana, kutoa daraja kwa wanaume tu si kuwakosea haki wanawake, kwa kuwa hizo ni huduma zinazofaidisha wote.
β€œMaana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye” (Lk 22:27).
Mwenye daraja anahudumia Kanisa kwa kumwakilisha Yesu; hivyo anatakiwa kuwa mwanamume kama yeye mbele ya Bibiarusi wake. Kukubali mgawanyo wa majukumu maishani ni kusifu hekima ya Mungu aliyetuumba watu wa jinsia mbili tofauti ili kustawisha familia, jamii na Kanisa.
β€œWalakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana… Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1Kor 11:11; 12:27).


Je, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa?
Ndiyo, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa.
β€œHatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?” (1Kor 9:5).
Paulo, akiwa mseja, hakudai kila mmojawao aoe, ila asiwe ameoa mara mbili, bali β€œmume wa mke mmoja” (1Tim 3:2; Tit 1:6), kama alivyoagiza mjane aandikishwe akiwa tu β€œmke wa mume mmoja” (1Tim 5:9).
Polepole mang’amuzi yakaelekeza Kanisa kubana nafasi hiyo kwa Maaskofu, na katika majimbo mengi kwa mapadri pia. Useja mtakatifu unawalinganisha zaidi na Yesu na kuwaachia uhuru wa moyo na wa muda kwa ajili ya huduma.
β€œWako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee” (Math 19:12).


Ni zipi Sakramenti za Huduma ya ushirika na utume?
Ni Sakramenti mbili ambazo ni Sakramenti ya Daraja na Sakramenti ya Ndoa


Sakramenti ya Daraja ndiyo nini?
Sakramenti ya Daraja ndiyo Sakramenti ambayo mwanamme mkatoliki aliyeitwa na Mungu hupata mamlaka na neema ya kuendeleza ndani ya Kanisa Utume Kristo aliowakabidhi Mitume wake


Ni kwa nini inaitwa Sakramenti ya Daraja?
Inaitwa Sakramenti ya Daraja kwa sababu mtu anapata Sakramenti hii kwa kuweka wakfu kwa ibada ya pekee inayomwezesha kwa nguvu ya Roho Mtakatifu atumie uwezo Mtakatifu kwa niaba na mamlaka ya Yesu Kristo ili kuhudumia Taifa la Mungu


Sakramenti ya Daraja ina ngazi ngapi?
Sakramenti ya Daraja inazo ngazi tatu, nazo ni Ushemasi, Upadre, Uaskofu


Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo gani?
Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo yafuatayo;
1. Inampa utimilifu wa SSakramenti ya Daraja Takatifu
2. Askofu anakuwa Mwandamizi rasmi wa Mitume
3. Inampa Askofu ushirika na Papa na maaskofu wengine wa kuwajibikia Makanisa yote
4. Inampa uwezo wa kufundisha, kutakasa na kuongoza


Askofu ni nani?
Askofu ndiye mchungaji mkuu wa kanisa Mahalia au Jimbo lake


Askofu ana kazi gani katika Jimbo lake?
Askofu katika Jimbo lake anamwakilisha Kristo akitimiza kazi ya kichungaji akisaidiwa na mapadri na mashemasi wake.
Askofu ni kiongozi wa kiroho katika jimbo mahalia. Na sio mambo ya kiroho tu ila hata ya kijamii lakini watu/mtu akiitaji ufafanuzi na msaada toka kwake.
Kazi zake ni:-
1. Kuliongoza taifa la Mungu alilopewa yaani wakristo/wengineo pia
2. Kusimamia na kuongoza Litrujia katika eneo husika.
3. Kueneza amani kwa kupitia karama na wadhifa aliopewa na Mungu.
4. Kueneza upendo katika eneo/jimbo mahalia.
5. Mtoa kauli ya mwisho kwa mambo ya kikanisa katika jimbo.
6. Kusimamia miito ya kanisa na kuchochea bila kukata tamaa
7. Kusimamia baraza la walei na kulishauri kwa kutolea kauli ya Mwisho kabla ya kwenda kwingine
8. Kuwashauri watu waliokata tamaa au kushindikana katika ngazi za chini
NB. Hivyo ndani ya kanisa kuna miogozo ili kupata nafasi zisizokinzana


Ni nani ampaye padri Daraja la Uaskofu?
Ni Baba Mtakatifu pekee au humteua Askofu mmoja akisaidiwa na maaskofu wengine wawili humweka wakfu Padri huyo kuwa Askofu (Mt 13:2-3)


Baba Mtakatifu ni nani?
1. Ndiye Askofu Mkuu wa Maaskofu wote
2. Ndiye mchungaji mkuu wa Wakatoliki wote hapa duniani
3. Ni Wakili wa Yesu Kristo hapa duniani. (Mt 16:18-19; Yoh 21:15-17).


Ibada ya Daraja inachapa alama gani nafsini mwa aliyepewa?
1. Ibada ya Daraja inatia rohoni alama isiyofutika
2. Inamlinganisha mpokeaji na Kristo Kuhani
3. Inamwezesha mwenye Daraja kutenda kwa Jina la Yesu aliye Kichwa cha Kanisa


Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka gani?
Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka ya
1. Kuadhimisha sadaka ya Misa Takatifu na kutakasa watu kwa njia ya Sakramenti.
2. Kuhubiri neno la Mungu
3. Kuwaongoza watu (Ebr 5:1-4)


Ni nani wenye uwezo wa kutoa Sakramenti ya Daraja?
Wanaotoa Sakramenti ya Daraja Katika ngazi tatu Uaskofu, Upadre, Ushemasi ni Maaskofu waliopewa Daraja halisi kama waandamizi wa Mitume.


Ni nani aweza kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu?
Mwenye kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu ni Mwanaume peke yake aliyebatizwa, akiwa na wito nasifa zinazotakiwa na kukubaliwa na Mamlaka ya Kanisa. Ndivyo Yesu Kristu alivyotaka mwenyewe


Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni kuweka mikono juu ya yule anayepewa Daraja na kutamka maneneo ya sala ya wakfu.


Anayetaka kuwa padri yampasa nini?
Yampasa;
1. Awe na tabia njema, akili za kutosha na afya nzuri.
2. Apende sana wokovu wa watu na kujitolea kwa huduma ya Mungu
3. Awe tayari kuishi hali ya useja maisha yake yote


Kwa sababu gani cheo cha Padri ni kikubwa sana?
Kwa sababu Padri anashiriki Upadri wa Yesu Kristo na ni mjumbe kati ya Mungu na Mwanadamu


Yatupasa nini kwa wenye Daraja Takatifu?
Yatupasa
1. Kuwaheshimu
2. Kuwasikiliza na kufuata mafundisho yao
4. Kuwasaidia katika utumishi wao kwa Sala na sadaka zetu


Matokeo ya Sakramenti ya Daraja ni yapi?
1. Inaleta mmiminiko wa kipekee wa Roho Mtakatifuambao unamlinganisha mhusika na Kristo
2. Inatia alama ya kiroho isiyofutika. kwa hiyo haiwezi kurudiwa au kutolewa kwa muda tuu.

Maswali yanayoulizwa sana Kumhusu Bikira Maria

Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambia…
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili maana yake ni nini?

Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili maana yake hakuzaliwa na dhambi ya asili kama binadamu wengine


Mama wa Yesu ni nani?

Mama wa Yesu Kristo ni Bikira Maria.
“Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 28Naye malaika akaja kwake akamwambia: β€œSalamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!” 29Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, β€œSalamu hii ni ya namna gani?” 30Ndipo malaika akamwambia, β€œUsiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” 34Maria akamwuliza huyo malaika, β€œMaadam mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” 35Malaika akamjibu, β€œRoho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu Zake Yeye Aliye Juu zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 36Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 37Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”(Lk 1:26-37).
Yesu ni Mungu ndio maana Bikira Maria akaitwa Mama wa Mungu kwa sababu ndiye aliyemzaa Yesu. Yaani Bikira Maria ni Mama wa Mungu tuu kwa sababu ya kumleta Yesu Duniani kama mzazi wa kimwili.
Hii haimaanishi kwamba Bikira Maria ni Mama wa Yesu kabla ya Yesu kuja Duniani kwa maana Yesu Alikuawepo kabla ya kuzaliwa kwake.
“Baba yenu Abrahamu alishangilia kwamba angaliiona siku Yangu, naye akaiona na akafurahi.’’ 57Wayahudi wakamwambia, β€œWewe hujatimiza hata miaka hamsini, Wewe wasema umemwona Abrahamu?’’ 58Yesu akawaambia, β€˜β€˜Amin, amin, nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, β€˜Mimi niko.’’’ (Yohane 8:56-58)
Inamaana kuwa Yesu alikuwepo kabla ya Mama yake mbinguni. Kwa sababu hiyo Umama wa Bikira Maria ni wa Kimwili tuu na sio Umungu. Bikira Maria hajatangulia kuwepo kabla ya Yesu Bali Yesu ndiye alikuwepo kabla na ni Mungu wake pia. Yesu kama Mungu alimuumba Bikira Maria na kumfanya Mama yake wa kimwili.
Bikira maria anamwita Yesu Mwanae wa kumzaa na vilevile anamwita Bwana na Mungu wake kwa kuwa ni Mungu wake pia na hivyo ni mdogo mbele ya Yesu. Sisi tunapomuita Bikira Maria Mama wa Mungu tunaheshimu nafasi yake ya kipekee ya kuizalia Dunia Yesu aliye Mungu. Kwa kuwa Bikira Maria ni Mdogo kuliko Mungu na Hana Umungu wowote hivyo haabudiwi kama Mungu au pamoja na Mungu.
Tunamuheshemu tuu Bikira Maria na Kumuomba atuombee kwa Mungu mwanaye Yesu kwa sababu anayo nafasi ya kipekee mbele ya Mungu mwanaye Yesu kama Mama yake wa kumzaa Duniani na kama mlezi wake akiwa duniani tangu kuzaliwa mpaka kufa Msalabani wakiwa pamoja.


Bikira Maria alimzaa Yesu Kristo kwa uwezo gani?

Bikira Maria alimzaa Yesu Kristo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. (Lk 1:35)


Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu? Na kwa nini aheshimiwe?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu kwa sababu amemzaa Yesu na Yesu ni Mungu.
“Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 28Naye malaika akaja kwake akamwambia: β€œSalamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!” 29Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, β€œSalamu hii ni ya namna gani?” 30Ndipo malaika akamwambia, β€œUsiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” 34Maria akamwuliza huyo malaika, β€œMaadam mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” 35Malaika akamjibu, β€œRoho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu Zake Yeye Aliye Juu zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 36Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 37Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana. 38Maria akasema, β€œTazama, mimi ni mtumisi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka akamwacha.”(Lk 1:26-38).
Yesu ni Mungu ndio maana Bikira Maria akaitwa Mama wa Mungu kwa sababu ndiye aliyemzaa Yesu. Yaani Bikira Maria ni Mama wa Mungu tuu kwa sababu ya kumleta Yesu Duniani kama mzazi wa kimwili.

Je, Bikira Maria kuitwa Mama wa Mungu maana yake ni kwamba yeye ndiye chanzo cha Yesu na Bila yeye Yesu asingekuwepo?

Hapana, haimaanishi kwamba Bikira Maria ni chanzo cha Yesu. Hii haimaanishi kwamba Bikira Maria ni Mama wa Yesu kabla ya Yesu kuja Duniani kwa maana Yesu Alikuawepo kabla ya kuzaliwa kwake.
“Baba yenu Abrahamu alishangilia kwamba angaliiona siku Yangu, naye akaiona na akafurahi.’’ 57Wayahudi wakamwambia, β€œWewe hujatimiza hata miaka hamsini, Wewe wasema umemwona Abrahamu?’’ 58Yesu akawaambia, β€˜β€˜Amin, amin, nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, β€˜Mimi niko.’’’ (Yohane 8:56-58)
Inamaana kuwa Yesu alikuwepo kabla ya Mama yake. Kwa sababu hiyo Umama wa Bikira Maria ni wa Kimwili tuu na sio Umungu. Bikira Maria hajatangulia kuwepo kabla ya Yesu Bali Yesu ndiye alikuwepo kabla na ni Mungu wake pia. Yesu kama Mungu alimuumba Bikira Maria na kumfanya Mama yake wa kimwili.
β€œUsiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” (Luka 1:31-33)
Bikira Maria alipewa nafasi ya kipekee na Mungu kuwa Mama yake na ingewezekana nafasi hii apewe mwanamke mwingine kama Bikira Maria Asingekuwepo au asingekuwa tayari kupokea heshima hii. Ndiyo maana Bikira Maria katika unyonge wake alitambua kuwa ni nafasi ya upendeleo wa Mungu aliyopewa na hivyo alimshukuru na kumtukuza Mungu kwa nafasi hii.
41Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Maria, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42akapaza sauti kwa nguvu akasema, β€œUmebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. 43Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? 44Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha. 45Amebarikiwa yeye aliye amini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.” 46Naye Maria akasema: β€œMoyo wangu wamwadhimisha Bwana, 47nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, 48kwa kuwa ameangalia kwa fadhili unyonge wa mtumishi wake, hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita mbarikiwa, 49kwa maana, Yeye Mwenye Nguvu, amenitendea mambo ya ajabu, Mtakatifu ndilo Jjina Lake.” (Luka 1:41-49)

Je Bikira Maria anamwonaje Yesu? Bikira Maria Anamchukulia Yesu kama nani Kwake?

Bikira maria anamwita Yesu Mwanae wa kumzaa kwa kuwa Bikira Maria ndiye aliyemzaa Yesu Duniani na kumlea kama mtoto wake. Vilevile Bikira Maria anamwita Yesu Bwana na Mungu wake kwa kuwa ni Mungu wake pia. Kwa sababu hivyo Bikira Maria ni mdogo mbele ya (Yesu) Mungu kama kiumbe cha Mungu (Yesu).

Kwa nini Bikira Maria anapewa Heshima kubwa

Tunamuheshimu Bikira Maria kwa sababu ya nafasi yake ya kipekee ya upendeleo aliyopewa na Mungu ya Kuwa Mama wa Mungu. Tunapomuita Bikira Maria Mama wa Mungu tunaheshimu nafasi yake ya kipekee ya kuizalia Dunia Yesu aliye Mungu na Mkombozi wetu.

Je, Bikira Maria anastahili kuabudiwa? Je Tunamwabudu Maria?

Hapana, Bikira Maria hastahili kuabudiwa na wala hatumuabudu Maria. Kwa kuwa Bikira Maria ni kiumbe wa Mungu na ni Mdogo kuliko Mungu kwa hiyo hana Umungu wowote hivyo haabudiwi kama Mungu au pamoja na Mungu.

Kwa nini tunamuheshimu Bikira maria na kusali kwake?

Tunamuheshemu Bikira Maria na Kumuomba atuombee kwa Mungu mwanaye Yesu kwa sababu anayo nafasi ya kipekee mbele ya Mungu mwanaye Yesu kama Mama yake wa kumzaa Duniani na kama mlezi wake akiwa duniani tangu kuzaliwa mpaka kufa Msalabani wakiwa pamoja.
Yesu mwenyewe alimtii na kumsikiliza Mama yake ndio maana muujiza wa kwanza aliofanya aliambiwa na mama yake. Bikira Maria ndiye aliyemwomba Yesu Afanye muujiza wake wa kwanza.
1 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3Hata divai ilipowaishia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni. 6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza mpaka juu. 8Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka. 9Naye mkuu wa sherehe alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa sherehe alimwita bwana arusi, 10akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; na watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. 11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. Yohana 2:1-11


Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa kwa sababu ni yeye aliyemzaa Yesu Kristo ambaye amelianzisha Kanisa.


Bikira Maria anafaida yeyote kwa Kanisa?

Ndiyo. Bikira Maria ni mwombezi Mkuu wa Kanisa.


Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria ni ipi?

Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria inafuata baada ya Heshima kwa Utatu Mtakatifu


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
“BWANA akamwambia Mose, β€œTengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Hapa duniani Yesu alizaliwa na nani?

Hapa duniani Yesu alizaliwa na Bikira Maria kama malaika alivyomuambia:
β€œRoho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo, hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu” (Lk 1:35).


Malaika alimsalimia Maria β€œumejaa neema”: maana yake nini?

Malaika alimsalimia Maria β€œumejaa neema” (Lk 1:28) maana ndiye tunda bora la ukombozi ulioletwa na Yesu.
Kwa stahili za Mwanae alikingiwa asirithi kwa wazazi dhambi ya asili na madonda yanayotokana nayo, wala asitende dhambi maisha yake yote.


Kwa nini Maria anastahili kuitwa β€œMama wa Mungu”?

Maria anastahili kuitwa β€œMama wa Mungu” kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: β€œUmebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
” (Lk 1:42-43).

Je, Bikira Maria ni kama Bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu Duniani au anayo thamani zaidi?

Bikira Maria sio kama bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu duniani. Yesu ametokana na Bikira Maria katika ubinadamu wake. Mwili wa Yesu wa kiubinadamu ni sehemu au uzao wa Bikira Maria. Bikira Maria anayo uhusiano wa damu na Yesu Kristu. Ndiyo maana Mungu alimtakasa Bikira Maria Ili atakayezaliwa kutoka kwake awe na yeye mtakatifu.
Mungu alimtakasa Bikira Maria kabla ya Kuamua kuzaliwa kupitia yeye kwa kuwa Mungu ni Mtakatifu. Ubinadamu wa Yesu (MWILI – Nyama na Damu) asili yake ni Bikira Maria.


Je, Maria amechangia wokovu wetu?

Ndiyo, Maria amechangia wokovu wetu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa.
Msimamo wake ulikuwa mmoja tu:
β€œTazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk 1:38).


Je, Maria ni mama yetu pia?

Ndiyo, Maria ni mama yetu pia: kwa kushiriki kazi yote ya Mwanae, Adamu mpya, amekuwa Eva mpya, mama wa wale wote aliowakomboa msalabani.
β€œYesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, β€˜Mama, tazama mwanao’. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, β€˜Tazama, mama yako’” (Yoh 19:26-27).
Kisha kushirikishwa ufufuko wake, anazidi kutushughulikia kimama tufike salama mbinguni alikotangulia kupalizwa mwili na roho.


Je, ni vizuri kumsifu Maria?

Ndiyo, ni vizuri kumsifu Maria kwa imani yake kama alivyosifiwa na alivyotabiri mwenyewe:
β€œβ€˜Heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana’… β€˜Tazama, tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa’” (Lk 1:45,48).
Ni lazima tulitimize hilo neno la Mungu katika kizazi chetu kama kilivyotimizwa na vizazi vilivyotangulia.


Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote.
β€œKwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Rom 8:38-39).
β€œKwangu mimi kuishi na Kristo, na kufa ni faida… Ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo” (Fil 1:21,23)
.
Kwa kuwa hao wako na Kristo mbinguni, wanatuombea mfululizo pamoja naye.
β€œNiliona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, β€˜Ee Mwenyezi, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini…’” (Ufu 6:9-10).
Tunawaomba wazidi kutuombea kwa Mungu, kama tunavyowaomba wenzetu waliopo duniani.
β€œMkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi” (Ef 6:18-19).


Je, Bikira Maria alikua na watoto wengine Mbali na Yesu?

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.


Wazazi wa Bikira Maria ni nani?

Wazazi wa Bikira Maria ni Yoakimu na Anna

Maswali na Majibu kuhusu Biblia

Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?
Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha “Mungu Mtawala”

Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?
Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa.
β€œNawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vilevile kama nilivyowatolea… Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe” (1Kor 11:2; 15:3).
β€œIlinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu… Mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2Tim 1:14; 2:2).
Tukikata huo mnyororo wa mapokeo, hata kama ni kwa kisingizio cha kushikilia Biblia, tunaachana na asili ya Kanisa.
β€œBasi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu… Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu” (2Thes 2:15; 3:6).

Maandiko Matakatifu ndiyo nini?
Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la β€œBiblia”, yaani β€œVitabu”.
Hao β€œwanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Pet 1:21).

Je, Biblia zote ni sawa?
Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza.
β€œAmin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Math 5:18). β€œNa mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki” (Ufu 22:19).
Je wakristo Wakatoliki wanasoma Biblia kwenye Ibada ya Misa? Biblia inanukuliwa mara ngapi Kwenye Ibada ya misa ya Wakatoliki?
Ndiyo, Wakatoliki wanasoma Biblia kila siku wanapoadhimisha Ibada ya Misa wakati wa Liturujia ya Neno.
Wakatoliki wananukuu Biblia mara Tano kwenye Ibada ya Misa. Wananukuu wanaposoma somo la Kwanzaa, Somo la pili, wimbo wa katikati, Shangilio na Injili.

Tunatambuaje Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu?
Tunatambua Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu kwa njia ya Mapokeo, yaani kwa sababu yametumiwa na Kanisa tangu mwanzo kwa kulisha kwa hakika imani yake.
Tunahitaji Mapokeo kwa kuwa Maandiko yenyewe hayataji orodha ya vitabu vyake vyote, Sanasana Yesu alividokeza baadhi akisema yanamzungumzia na kutimia ndani yake,
β€œNi lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii, na Zaburi” (Lk 24:44).
Halafu Barua ya Pili ya Mtume Petro ikalinganisha β€œna Maandiko mengine” nyaraka zote ambazo Paulo aliziandika β€œkwa hekima aliyopewa” (2Pet 3:15-16).

Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni zipi?
Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni kwamba mambo mengi muhimu hayakuandikwa,
β€œKuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu, ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa” (Yoh 21:25).
Tena barua ni nusu tu ya kuonana; hivyo Yesu hakuandika lolote, nao Mitume hawakupenda kuandika yote.
β€œKwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi mdomo kwa mdomo, ili furaha yetu iwe imetimizwa” (2Yoh 12).
β€œNalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema mdomo kwa mdomo” (3Yoh 13-14).
Hasa ibada haziwezi kufanyika kwa barua; k.mf. kuwekea mikono ili kumshirikisha Roho Mtakatifu. Paji la namna hiyo halipitii Maandiko, bali Mapokeo tu. Hatimaye Biblia ikipotoshwa haipingi, kwa kuwa si mtu hai anayeweza kujitetea.

Biblia iliandikwa kwa kusudi gani?
Biblia iliandikwa kusudi tupate β€œkuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini” tuwe β€œna uzima wa milele” (Yoh 20:31).
β€œTangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki” (2Tim 3:15-16).
Si lengo lake kutufundisha historia, jiografia wala sayansi: kuhusu elimu hizo na kuhusu ufasaha wa lugha Biblia ilitegemea ujuzi na vipawa vya watu walioiandika.

Je, vitabu vya Biblia vinatofautiana?
Ndiyo, vitabu vya Biblia vinatofautiana kwa kuwa Mungu alijifunua hatua kwa hatua; hivyo vitabu 46 vilivyoandikwa kabla ya Yesu vinaitwa Agano la Kale na 27 vilivyomfuata vinaitwa Agano Jipya.
β€œKwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka” (Eb 8:13).
Mungu β€œndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha” (2Kor 3:6).

Je, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana?
Ndiyo, vitabu vyote vya Biblia vinahusiana kwa kuwa vinaangaziana na kuunda kitabu kimoja ambacho ni Neno la Mungu yuleyule, ingawa katika hatua tofauti: Agano la Kale ndiyo maandalizi na Agano Jipya ndio utimilifu wake.
Yesu alisema, β€œMsidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17).
Tunahitaji Agano la Kale ili tuelewe vizuri Agano Jipya katika maandalizi yake, na tunahitaji Agano Jipya ili tuelewe Agano la Kale lilivyotimilizwa na Yesu.

Je, inafaa tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi?
Hapana, haifai tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi wasiozingatia jinsi Yesu alivyolitimiliza kwa maneno na matendo hata wakamshutumu kutenda kinyume:
β€œMtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato” (Yoh 9:16).
Alipofafanua amri 10 za Mungu alikariri:
β€œMmesikia watu wa kale walivyoambiwa… lakini mimi nawaambieni…” (Math 5:21,27,31,33,38,43).
Alipouliziwa unajisi wa vyakula kadhaa, alisisitiza,
β€œβ€™Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni?’ Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote” (Mk 7:18- 19).
β€œBasi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16-17).
Hakika, mwili ni mzito kuliko kivuli chake.
Vile vile katika Warumi 4:16. Tunasoma “Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote:si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali kwa wale waishio kwa Imani kama Abrahamu. Yeye ni Baba yetu sote.”
Wakristo wengine wanachanganywa na wale wasioyajua maandiko na kuwataka washike sheria na Torati,basi tukisema ni lazima kushika sheria tutakua tunakataa kua Abrahamu hakuwa mtu wa Mungu maana kwa Abrahamu hatukuwa na Sheria wala Torati na alipata kibali machoni Pa Mungu tuu kwa Imani. Kumbuka pia Abrahamu alitahiriwa baada ya Kuwa tayari mtu wa Mungu kwa Imani yake na sio kwamba Kutahiriwa ndio kulifanya mtu wa Mungu.
Tumekombolewa kwa Imani na sio kwa Sheria. Wagalatia 5:18 “Lakini Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”
Hatumtumikii Mungu ili tuwe watu wa Mungu bali tukishakua watu wa Mungu ndio tunamtumikia Mungu.

Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa lini?
Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa aliposulubiwa, akionekana na Wayahudi wenzake kama kwamba amelaaniwa:
β€œKristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa: β€˜Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti’; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” (Gal 3:13-14).

Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni vipi?
Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni Injili 4 zilizoandikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohane.
Ndio moyo wa Maandiko Matakatifu yote, kwa kuwa ndizo shuhuda kuu juu ya maisha na mafundisho ya Yesu.
Yeye β€œamepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili” (Eb 8:6-7).

Tueleweje Maandiko Matakatifu?
Tuelewe Maandiko Matakatifu kwa kuzingatia hasa Mungu alitaka kusema nini kuhusu wokovu wetu kupitia waandishi wengi aliowaongoza kuyatunga kwa lugha na mitindo mbalimbali.
Lakini ebu, β€œYamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na Maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe” (2Pet 3:16).
Utitiri wa madhehebu yanayoshindana yakidai kushikilia Biblia tu unathibitisha uwekezano mkubwa wa kuipotosha kwa namna moja au nyingine.
β€œUtakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo” (2Tim 4:3-4).
Njia pekee ya kukwepa fujo hiyo ni kuelewa Maandiko ndani ya Kanisa, kadiri ya Mapokeo yake hai.
β€œLakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu” (1Kor 11:16).
Biblia nje ya Kanisa ni kama samaki nje ya maji.

Tupokeeje ufunuo wa Mungu?
Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,
β€œAwasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” (Lk 10:16).
β€œSisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” (1Thes 2:13).

Neno “BIBLIA” maana yake ni nini?
Neno “BIBLIA” ni neno linalotokana na neno la Kigiriki “Biblion” lenye maana ya vitabu.
Biblia ni Mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vya dini vilivyochaguliwa na kuidhinishwa kua vyafaa kutumika.

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.
Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.
Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.
Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?
Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.
Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?
Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.
Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?
Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.
Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia
Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hivi…”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”…Kwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?
Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.
Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu
Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.
Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?
Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..”Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu “…
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?

Biblia ina sehemu kuu ngapi?
Biblia ina sehemu kuu 2 (mbili) ambazo ni
1. Agano la Kale (A.K)
2. Agano Jipya (A.J)

Agano la Kale lina vitabu vingapi?
Agano la Kale lina vitabu 46

Agano Jipya lina vitabu vingapi?
Agano Jipya lina vitabu 27

Biblia nzima ina vitabu vingapi?
Biblia nzima ina vitabu 73

Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Vitabu vya Musa (5)
2. Vitabu vya Historia (16)
3. Vitabu vya Hekima (7)
4. Vitabu vya Manabii (18)

Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu ngapi?
Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume
3. Nyaraka mbalimbali (21)
4. Kitabu cha Ufunuo

Vitabu vya Musa ni vipi?
Vitabu vya Musa ni
1. Mwanzo
2. Kutoka
3. Walawi
4. Hesabu
5. Kumbukumbu la Torati

Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni wakina nani?
Wainjili wanne Katika Agano Jipya ni
1. Mathayo
2. Marko
3. Luka
4. Yohane

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni
1. Cha kwanza ni Kitabu cha Mwanzo
2. Cha mwisho ni Kitabu cha Malaki

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni vipi?
Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni
1. Kitabu cha kwanza ni Injili ya Mathayo
2. Kitabu cha mwisho ni Kitabu cha Ufunuo

Injili ni nini?
Injili ni Habari njema ya wokovu iliyoletwa na Yesu Kristo

Watoto wawili wa Adamu na Eva walkikuwa wepi?
Walikuwa ni Kaini na Abeli

Watoto wa Nuhu ni wepi?
Watoto wa Nuhu ni Shemu, Hamu na Nefteli

Mababu watatu wa Imani Katika Biblia ni wakina nani?
Mababu wa Imani ni Ibrahimu, Isaka na Yakobo

Watoto wa Yakobo ni Wepi?
Watoto wa Yakobo ni
1. Reubeni
2. Simeoni
3. Lawi
4.Yuda
5. Dani
6. Naftali
7. Gadi
8. Asheri
9. Isakari
10. Zabuloni
11. Yosefu
12. Benjamini

Nani aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi?
Musa ndiye aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi

Mungu alimpa Musa Amri Kumi wapi?
Mungu alimpa Musa Amri Kumi katika mlima wa Sinai

Vitabu vya Historia katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Historia katika Biblia ni
1. Yoshua
2. Waamuzi
3. Ruthu
4. 1 Samweli
5. 2 Samweli
6. 1 Wafalme
7. 2 Wafalme
8. 1 Mambo ya Nyakati
9. 2 Mambo ya Nyakati
10. Nehemia
11. Ezra
12. Tobiti
13. Yudith
14. Esta
15. 1 Wamakabayo
16. 2 Wamakabayo

Vitabu vya manabii katika Biblia ni vipi?
Vitabu vya Manabii ni
1. Isaya
2. Yeremia
3. Maombolezo
4. Baruku
5. Eekieli
6. Danieli
7. Hosea
8. Yoeli
9. Amosi
10. Obadia
11. Yona
12. Mika
13. Nahumu
14. Habakuki
15. Sefania
16. Hagai
17. Zekaria
18. Malaki

Vitabu vya Hekima Katika Biblia ni Vipi?
Vitabu vya Hekima ni
1. Yobu
2. Zaburi
3. Mithali
4. Mhubiri
5. Wimbo ulio Bora
6. Hekima ya Solomoni
7. Yoshua Bin Sira

Nyaraka za Mitume katika Biblia ni zipi?
Nyaraka za Mitume ni;
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike
9. 2 Wathesalonike
10. 1 Timotheo
11. 2 Timotheo
12. Tito
13. Filemoni
14. Waebrania
15. Yakobo
16. 1 Petro
17. 2 Petro
18. 1 Yohane
19. 2 Yohane
20. 3 Yohane
21. Yuda

Je, Bikira Maria alikua na watoto wengine Mbali na Yesu?
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Baba wa Yesu Kristo ni nani?
Baba wa Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe

Baba Mlishi wa Yesu Kristu ni nani?
Baba mlishi wa Yesu Kristo ni Yosefu Mtakatifu (Mt 1:18-20)

Yesu Kristu alizaliwa wapi?
Yesu Kristu alizaliwa Bethlehemu pangoni (Lk 2:4-7)

Nini maana ya Jina Bethlehemu?
Bethlehemu maana yake ni
Nyumba ya mkate

Yesu Kristu aliishi wapi kabala ya kuanza kazi yake?
Yesu Kristu Aliishi Nazareti kabla ya kuanza kazi yake

Mtangulizi wa Yesu Kristu ni nan?
Mtangulizi wa Yesu Kristu ni Yohani Mbatizaji

Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni nani?
Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni Zakaria na Eizabeti

Wazazi wa Bikira Maria ni nani?
Wazazi wa Bikira Maria ni Yoakimu na Anna

Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?
Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo
6. Barttholomayo
7. Mathayo
8. Thomaso
9. Yakobo wa ALfayo
10. Thadayo (Yuda Thadey)
11. Simoni Mkanaani
13. Yuda Iskarioti – Aliyemsaliti

Baba Mtakatifu wa kwanza ni nani?
Baba Mtakatifu wa Kwanza ni Mt. Petro

Nani ni Mitume wa Mataifa?
Mitume wa mataifa ni Paulo na Barnaba

Nani ni shahidi wa kwanza katika Agano Jipya?
Shahidi wa Kwanza ni Mt Stefano

Yesu Alianza kuhubiri injili kwa maneno gani?
“Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili” (Mk 1:15)

Yesu alitukomboa kwa hatua zipi?
Yesu alitukomboa kwa Hatua Mbili (2) ambazo ni;
1. Mafundisho yake
2. Mateso, Kifo na Ufufuko wake

Sentesi saba za Yesu msalabani ni zipi?
Sentesi saba za Yesu Msalabani ni;
1. Baba uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya (Lk 23:34)
2. Nakuambia Hakika leo utakuwa pamojanami Mbinguni (Lk 23:43)
3. Mama huyu ndiye mwanao (Yoh 19:26)
4. Tazama huyu ndiye Mama yako (Yoh 19:27)
5. Eloi, Eloi, lema Sabakthani (Mk. 15:34) Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?
6. Naona kiu (Yoh 19:28)
7. Yametimia (Yoh 19:30)

Soma hii, kama wewe ndio mzazi wa huyu msichana ungefanyaje?

Wewe ni mzazi mwanao anasoma kidato cha tatu mkoani umemsafirisha leo kwenda shule baada ya masaa matano ukasikia gari alilo panda mwanao limepata ajali wamekufa watu wote upo ktk harakati za kuandaa msiba,

mwanao anakupigia simu baba/mama mimi mzima sijafa mpenzi wangu ABDUL aliniambia nishuke Chalinze ili niwe nae kwa siku mbili alafu niende shule je, wewe mzazi unge mfanyaje mwanao?

Ujumbe mzuri wa kumtumia mpenzi wako kumtakia usiku mwema

“””””Yule””””” Anipendezae lazima nimkumbuke”” “”nimpe salamu “”moyo”” wangu “”uridhike”” “”Nimuombee kwa MWENYEZI “”MUNGU”” mabaya yamuepuke”” “”na kila lililo la kheri kwake lisiondoke”” “”nakutakia”” “ucku mwema”

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Ufugaji wa nguruwe na faida zake

Na, Patrick Tungu

Utangulizi

Nguruwe ni mnyama amabaye hutumika kama chakula / mbonga na pia ni zao la biashara kwa mfugaji, mjasirimali na mfanyabiashara.

NGURUWE HUTEGEMEA SANA MAMBO YAFATAYO

1 . Bada imara na rafiki kwake
2. Usafi ni muhimu sana katika bada la Nguruwe
3 Mchaganyo bora wa chakula
4. Tiba bora na kinga
5. Maji na Lishe ( access ya vyakula Muhimu kwake )

CHANGAMOTO

KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KUNACHAGAMOTO ZAKE LAKINI ZAWEZA KUTATULIWA KWA KUFATA MAMBO KADHAA.

Katika ufugaji wa nguruwe kunachagamoto ya vifo vya nguruwe wachanga ambao hupunguza faida ya biashara ya nguruwe kwa kupunguza idadi ya nguruwe wazima wa kuuzwa lakini utunzaji mzuri wa nguruwe wachanga huepusha vifo vinavyotokana na shida kama:

Matatizo ya kupumua

Ni kifo kinachosababishwa na mama anapomlalia nguruwe mchanga.chagamoto hii inaweza kutatuliwa kwa kuwatega au kuwa na mabanda makubwa ya kulelea watoto.

Baridi

Nguruwe wachanga huathiriwa na baridi haswa katika majuma mawili au matatu ya mwanzo. Hii ni kwa kuwa wana kiwango kidogo cha utando wa mafuta wa kuwakinga.
Unashuriwa kuwaweka katika hali ya joto, wape matandiko na utumie vipasha joto kama vile kuasha globu za joto kama utakuwa umewaweka kwenye mabada ya kuta au nyumba yenye sakafu baridi.

Namna bora utunzaji wa nguruwe wachanga

Nguruwe moja wa kike ana uwezo wa kuzaa watoto 12. Namna ifuatayo itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya nguruwe wachanga:
1.Pale nguruwe awapo na kidonda nyunyizia dawa ya ayodini 5% kwenye kovu ili kuzuia kuambukizwa kwa magonjwa.
2.Wawekee matandiko (nyasi kavu au maganda ya miti) mahali pa mapumziko ili wapate joto au utumie globu za joto.
3Wadunge sindano ya madini ya chuma (iron) siku ya tatubaada ya kuzaliwa ili kuzuia upungufu wa damu.
3. Yalainishe meno ya vichaga kabla ya masaa 24 ili kuzuia uharibifu wa matiti wakati wanaponyonya.
4. Watie vibandiko au utoboe masikio ili uwatambue na uhifadhi rekodi zao kama kuna umuhimu kama vile wafanyavyo wafugaji wa ng’ombe.
5. Wapime uzani wanapozaliwa na uhifadhi rekodi hiyo itakusaidia kujua ukuaji wao na maendeleo yao
6. Wahasi wale wa kiume juma la tatu, wale ambao hawafai katika kuendeleza kizazi kwa kutumia mtindo wazi (open method) kama unaona inafaa.
7. Wapatie dawa ya kuzuia minyoo pia zipo dawa za asili kama unga wa mkaa na majivu pia zipo za kitaalamu, wasiliana na wataalamu wa mifugo
8.Waachishe kunyonya katika juma la nane au wafikapo kilo 14 hadi 20 hii itasaidia kujitegemea na kukua kwa haraka.

Nguruwe Walioachishwa Kunyonya

1.Walioachishwa kunyonya wawekwe makundi ya 10 hadi 12 kulingana na uzito au ukubwa wao kwenye eneo ambalo watajitosheleza.
2.Watenganishe wakubwa kwa wadogo ili kuzuia kupigana.
3.Wakati wa kuwaachisha kunyonya mwondoe mama yao kutoka kwa watoto ili kupunguza usumbufu.
4Watoto wa nguruwe wa mama tofauti wasiwekwe pamoja maana hii husababisha mapigano kati yao na
5.Unapowachanganya watoto wa mama tofauti wapake mafuta ya gari yaliyotumika kwenye ngozi yao au mafuta ya kula ili kuiondoa harufu ya kutambulika ili wasipigane

FAIDA YA UFUGAJI WA NGURUWE

Faida kuu ya nguruwe ni zao la chakula lakini pia ni zao la kukuongezea kipato ukiwa kama mjasirimali / mfanyabiashara.
Lengo langu nikueleza namna unavyoweza kufuga na kutupa faida, Steps zifatazo ni muhimu kuzigatia.

JIPE MTAJI WA MILLION 4 / 3.5 KWA NGURUWE 50

UANDAAJI WA BADA WEKA MAKADILIO YA LAKI TANO (800,000/=) .
Hapo nazugumzia banda lenye heru U yenye mstatili ikiwa na kitako kirefu
Eneo lenye ukubwa wa mita 50 kwa 50 litafaa zaidi ili kuhakikisha usalama wa nguruwe wako na ukuaji bora.
1. Tafuta mabati used kwa bei ya 5000 mfano mabati 20 ya futi 10 /10 = 100,000/=
2. Tafuta mabazi ya futi 10 kwa 2000 kila moja utapata mabazi pic 100 = 200,000/=
3. Tafuta miti ya nguzo na kechi ya 1000 na 2000 miti ya 1000*70 na 2000*3 = 120,000/=
4. Tafuta chagalawe / moramu trip 10*3000 =30000/=
5. Cement mifuko kwa ajiri ya sakafu na mashimo ya kulishia 5 *18000 = 90,000/=
6. Misumari ya aina 4, nch 6 kg5,nch 3 kg5 nch 5 kg10 na nch4 kg10, Bawaba na komeo =100,000/=
7. Malipo ya fundi 75000 fundi uashi na 75000 fundi seremala =150,000

JUMLA HAPO INAKUWA 790,000/= MAKADILIO INAKUWA 800,000/=

UNUNUZI WA NGURUWE WA KUANZIA .

Nguruwe wadogo wadogo ni vinzuri zaidi kuanza nao kwa sababu watakuzalia watoto wengi na kwa muda mrefu . Chukua mfano MILLION 2.5 . Nguruwe wadogo wa dogo wanauzwa 50000 au 40000 inategemeana na mahala na maelewano . Milioni 2.5 inakupa vitoto 50 au 55 . Hivyo unawexa kuwa na vitoto jike 50 na vidume 5. baadaye ukaongeza madume matano ya kuazima au kukondi kwa ajiri ya kupandishia

MAANDALIZI YA CHAKULA

Mchaganyiko wa chakula cha nguruwe na gharama zake tunaweza ukadilia kujitosheleza kwa laki tatu kwa mwenzi mmoja kwa nguruwe hao 50, kwa 300,000/= , ambapo itajumuisha tiba / kinga, lishe, vyakula vya nguruwe vinaweza kuwa pumba ya mpunga ile laini,pumba ya mahindi, mashundu, mabaki ya magada ya vianzi amba mabaki ya chakula yaliyosalama

MALIPO YA MSIMAMIZI NA ENEO LA KUWEKEZA

Katika kipengele hiki makadilio ya juu ama ya chini kwa msimamizi wa kazi yako waweza mlipa 100,000/= ama chini yake pia kwa mwenye eneo huwa nimaelewano tu aunaweza pata kwa fair au kukakodi kwa laki tatu, 300,000/= kwa mika miwili.

HIVYO JUMLA YOTE YA GHARAMA ZA UAZISHAJI UWEKEZAJI WA NGURUWE 50 ZITAKUGHARIMU MILLION 4 AMA MILLION 3.5 KWA MAANA KUWA HAPO JUU NIMETUMIA MAKADILIO YA JUU NA UKIINGIA KWENYE UHALISIA KAMA MJASIRIMALI LAZIMA IPUNGUE NA KUFIKIA 3.5

N:B ikumbukwe hapo nyuma nilitoa mchaganuo wa nguruwe 40 ndiyo maana makandilio yalikuwa kwenye million 3.5 ama 3 kamili.

KIPATO AU FAIDA YA UFUGAJI NGURUWE

Nguruwe wanafaida ya haraka na nimradi wa uhakika kabisa, ukipitiia mchanganuo hapo juu wa nguruwe 50 utatupa faida kama ifatavyo

Nguruwe huzaa Mara mbili kwa mwaka na huzaa watoto zaidi ya watanoyaani huzaa watoto 12 ama nane .
Basi chukua nguruwe 50 * vitoto 5 yaani ufanye kuwa nguruwe wako 50 wakupatie vitoto vitano vya uhakika
Nguruwe 50*5 = 250 ukijumlisha na wale 50 wa mtaji umakuwa nao 300 . Chukua zao la nguruwe la 250 na uza kwa 200000 kwa kila nguruwe yaan bei ya kawaida kabisa. Utapata Million 50. Hivyo zao la kwanza ndani ya robo tatu ya mwaka inakutegenezea million 50 pia na mienzi sita ijayo inakupa tena 50 na zaidi ili kukamilisha uzao wa pili hii inkupa uhakika wa kutegeneza million 100 za uakakika ndani ya mwaka mmoja na nusu ama miaka miwili ukijipa timeframe work lakini kumbuka hapo tumefanya kwa hesabu ya uzao wa chini kabisa ambapo tumeangalia na hasara ya vifo kama vifo visipotokea na uzao ukawa mkubwa utakuwa na uhakika wa kutegeneza million 150 kwa miaka miwili.
Kwenye hesabu ya kuwale unaweza kuwaza sana kuwa itaongezeka na kukughalimu sana jibu ni hapana mpka kufikia kuuza hawatokugharimu zaidi ya million 7 je million 7 kwenye million 150 ni kitu kisicho nafaida ?

NB . jambo lolote linahitaji umakini naa dhamira ya dhati pia kushirikisha wataalamu na wenye uzoefu ili kufikia leng Ewe ndugu kila kitu kinawezekana UTAYARI WAKO / UTHUBUTU WAKO, UAMINIFU .NA MAAMZI YAKO.
chukua kalamu na karatasi fanya hesabu mwenyewe kwa mtaji wako na namna unavyoweza usipopata faida nipigie simu pia ukipata faida nipigie simu kwa maelezo zaidi na msaada zaidi

POINT TO NOTE, pia kwa wale wanaohitaji kufanya hii project hawana eneo wala uhakika wa chakula na lishe na usimamizi thabiti wa kitaalamu na wenye tija. tuwasiliane Kwa msaada zaidi.

NYOGEZA

Nguruwe 20 wanaweza kukugharimu million mbili unapoanzisha mradi na kukupa faida isiyopungua million 20 kwa uzao wa kwanza na uzao wa pili utapata uhakika wa jumla ya million 40 ukitoa gharama zote hazitozidi milio 5.5
Nguruwe 10 wanaweza kukugharimu million moja na point unapoanzisha mradi na kukupa faida na kukupa faida ya million 10 kwa uzao wa kwanza ukijumlisha na uzao wa pili utapata uhakika wa kuwa na million 20 ukitoa gharama zote hazitozidi million 4.5
Nguruwe 5 wanaweza kukugharimu laki tano na point unapoanzisha mradi na watakupa faida ya zaidi ya million5 kwa uzao wa kwanza na uzao wa pili watakupa jumla ya million 10 ukitoa gharama zote hazitozidi million 3

Kumbuka hesabu zangu zote nimeweka kwa makadirio ya juu hivyo ukienda kwenye uhalisia nakufata kanuni za ujasirimali lazima zipugue asilimia 5 au 10 ya jumla yote niliyotoa.

SMS nzuri sana ya kutakia usiku mwema

Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana

“Cannibalism,”
Kudonoana kwa kuku ni tatizo linalo wa sumbua wengi, ni moja ya athari ya lishe duni. Ni kisema lishe duni na maanisha chakula wanacho kula kukosa vurutubisho muhimu vya madini au kuku kutokula chakula cha kutosha.

Hizi ni moja ya sababu zinazo pelekea kuku kudonoana.

1.Kuku kukaa wengi kwenye eneo dogo

2. Tabia yao

3.Ubaguzi wa rangi

Hii Mara nyingi hutokea kwa kuku weusi ukiwachanganya na kuku mweupe au rangi ingine tofauti, kuku weusi Mara nyingi huwa ni wakali sana Kwahiyo ukiona kuku bandani kwako kadonolewa chunguza kwa makini chanzo ninini! Kama ni ubaguzi wa rangi unaweza watenga hao weusi.

4. Kuku kutokupata chakula cha kutosha

5.Upungufu wa madini ( protini)

6. Kukosa kitu walicho kizoea au kuboreka

Kwa mfano kuku ukiwazoesha kuwa changanyia Damu kwenye chakula , siku utakapo punguza kipimo au kuacha kabisa kuwa changanyia damu ambayo umewazoesha kuwa changanyia lazima watadonoana.

Kuku ukiwa zoesha kuwa fungia mchicha hasa wale kuanzia mwezi mmoja hadi wa miezi 4 siku utakapo acha kuwafungia mchicha inaweza sababisha wakadonoana.

Kuku hupenda kuparuaparua na kuzunguka zunguka. Wakikosa nafasi na vitu vya kudonoa donoa huanza kudonoana wenyewe kwa wenyewe.

7. Mwanga mkali

8. Msongo

Banda lenye joto sana na lisilo pitisha hewa vizuri huwapatia msongo/stress kuku, na kuku huweza kuanza kudonoana.

9. Uhaba wa vyombo bandaniπŸ‘‡

Hii hutokana na kuwa na kuku wengi halafu vyombo vichache vya chakula , Kwahiyo wakati wa kula lazima watagombania na kudonoana

Kuku wa umri tofauti kuwekwa kwenye banda moja

Tiba Kinga

Tiba

Tumia Protini (Amino Acid) stahiki kulingana na tatizo.

Mfano: (methionine , lysine nk)

Kinga

Changanya Proteni kiwango kizuri kwenye chakula cha kuku,chakula cha kuku kijumuishe virutubisho vyenye asili ya wanyama ambavyo ni chanzo kizuri cha Proteni

Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye eneo la kutosha . hii inategemea aina ya kuku na umri wake.

Stori inayogusa!!

Habari ya mama aliyeuguliwa ghafla na mtoto wake majira ya SAA 2 usiku, mtoto alibanwa na kifua(asthma), hali ilikuwa mbaya na mama akaenda kuomba msaada kwa jirani yake aliyekuwa na gari, akamjibu gari haina mafuta, akaenda kwa mchungaji ili amsaidie, akamjibu nina wachungaji toka USA, hivyo sitaweza kuwaacha peke yao, mama hakuwa na jinsi aliamua kumbeba mtoto ili amuwahishe hospitali akiwa na hofu asije kufa kama baba yake aliyefariki miaka michache kwa ugonjwa huo.

Β 

Huyo mama alikuwa na tatizo la mguu na mtoto alikuwa mzito, mama alianguka Mara kadhaa na akainuka kuendelea na safari. Njiani alikutana na watu waliotoka kazini aliomba wamsaidie walimpuuza na alijaribu kusimamisha magari hayakusimama. Kichaa mmoja mchafu aliyekuwa akizungukazunguka mitaani na jalalani alipomuona yule mama anavyohangaika na mtoto akamwendea na kumchukua mtoto, kisha akamweka begani, mama hakuwa na la kusema ila kumwelekeza Hospitali, yule kichaa alielewa akaenda haraka hadi Hospitali. Ma doctor walipomuona yule kichaa na mtoto wakajua kuna dharura, wakamchukua mtoto na kumhudumia haraka, baada ya dk.10, mama wa mtoto akawasili, kisha ma doctor wakatoa taarifa kuwa, mtoto angecheleweshwa dk 5 angekufa. Mungu alimtumia yule kichaa mchafu kuokoa maisha ya mtoto. Hivyo usimteegemee Mch, jirani, wenye magari, matajiri nk. Mungu huweza kuinua MTU usiyemdhania kukubariki. Mwamini Mungu atakubariki. Usitumainie wanadamu hakuna baraka kwao. Mungu huinua vinyonge ilI kuangusha vyenye nguvu. Tuma ujumbe huu wa BARAKA kwa watu japo wanne ili kushiriki BARAKA hizi za Mungu, ujumbe huu waweza tena nitumia nami ktk kutakiana BARAKA za MUNGU WETU.

Kisa kilichombadilisha mume tabia

Mume alirejea nyumbani na kukuta ujumbe juu ya meza umeandikwa “NIMEONDOKA” ilikuwa jioni, alienda jikoni na kukuta kukavu, aliwaita watoto na kuwauliza wakasema walimuona Mama akiondoka na begi lakini hakuwaambia anaenda wapi. Mume alichanganyikiwa, alijaribu kuchukua simu kumpigia lakini ilikuwa haipatikani, kabla hajafanya chochote mtoto wao wa mwaka mmoja alikuja akilia na kusema ana njaaa.

Ilibidi kuingia jikono na kutaka kupika huku akitukana matusi yote, kila kitu kilikuwa hakuna, hapo ndipo alipokumbuka kua asubuhi mkewe alimuomba pesa ya kununua chakula akamuambia hana afanye maarifa. “Ataondokaje ghafla namna hii, huyu mwanamke mshenzi kabisa..” Aliwaza lakini alikumbuka kuwa asubuhi hiyo hiyo baada ya kumnyima mkewe pesa ya chakula mke alilalamika kua amechoka maisha yale na yeye akamjibu “Kama umkechoka si uondoke, wanawake wako wengi ukiondoa kitu na weka kitu…”

Akili yake iliwaza sana akakumbuka mchepuko wake, aliupigia simu uje nyumbani, lakini ulistuka kuhusu Mama watoto, akamuambia ameondoka na kamuachia watoto wote wa nne. Mchepuko ulijifanya hausikii vizuri na baada ya muda ukazima simu. Sasa alikuwa amechanganyikiwa, alitaka kupiga simu Kijijini ndipo alikumbuka kuwa hata namba ya Mama mkwe wake alikuwa hana, hakuwa na kawaida ya kuongea nao na mara chache alipoongea ni pale ambapo mkewe alipiga simu na kumuambia kuwa aongea na familia.

Alikumbuka ana namba ya rafiki wa mke wake, akampigia kumuuliza mkewe yuko wapi akasema hajui lakini mara ya mwisho alipompigia alimuambia kuwa “ANAENDA KUPUMZIKA”. Alizidi tena kutukana, alitoka jikoni nakuwachukua watoto kwenda kwenye mgahawa alizunguka nao mpaka kupata sehmu ya kula, watoto walifurahi sana siku hiyo kutoka na Baba yao, waliongea na kucheka kula nnje ya nyumbani, kidogo alipata faraja na kutabasmau lakini bado alikuwa akiwaza kuhusu mkewe.

Baada ya kumaliza chakula aliwarudisha watoto nyumbani alitaka kwenda kuwalaza lakini walikataa na kutaka kuogeshwa. Kimbembe kilianza katika kuwaogesha wale wadogo. walihtaji kuoga kwa maji ya moto, alienda moja kwa moja kuwasha jiko la umeme akakuta haliwaki. Akaanza kutukana ndipo alipokumbuka miezi mitatu iliyopita liliharibika na mkewe alipomuambia alisema watumie mkaa, akaenda kwenye jiko la gesi, hata hakuwasha kwani alikumbuka kuwa siku tatu zilizopita mkewe alimuomba hela ya gesi akamtukana mwanamke gani mvivu kuwasha mkaa, anatumia tu hela wakati hana chakufanya.

Alichanganyikiwa zaidi, akaenda kuwalaza watoto kwa lazima lakini ile na yeye anapanda kitandani mtoto mdogo akaanza kulia kwa sauti ya juu, joto, alitaka kuoga, ilibidi kunyanyuka kutaka kuwasha mkaa, atauwashaje hata mafuta ya taa hajui yako wapi labda angeweka ili uwake. Ilibidi kunyanyuka kuwasha TV watoto waliangalia mpaka walipopitiwa na usingizi, hata hakuwanyanyua yeye na watoto walilala, pale pale kwenye kochi mpaka asubuhi. Wote walipitiwa, asubuhi alistuka ameichelewa kazini na watoto walitakiwa kuandaliwa kwaajili ya shule.

Kichwa kilizidi kumuuma, hakujua aanzie wapi aishie wapi, akanunue vitafunwa au apike chai lakini atapika na nini? Akawaambia siku hiyo hakuna kwenda shule, akawasha gari kwenda kununua gesi na vitu vya nyumbani. Bado mkewe alikuwa hapatikani. alinunua jiko na kuja kupika chai akawapa watoto, akaanza kumtumia meseji mkewe za kumuomba msamaha, kumuomba arejee nyumbani kwani peke yake asingeweza kuwale watoto lakini meseji hasikupokelewa.

Simu ilianza kuita, ilikuwa namba ya bosi wake, alikuwa akimhitaji kupeleka taarifa ofisini, aliamua kumtafuta mdogo wake aje akae na wanae lakini naye alikuwa bize na kazi zake. Ili bidi kuwaacha watoto nyumbani na kwenda ofisini hivyo hivyo. Alifika ofisini na kukabidhi taarifa, baada ya muda meseji simu ilipiga kelele kuashiria kuwa meseji alizomtumia mkewe ziliingia, simu ilikuwa imewashwa.

Harakaharaka alinyanyua simu na kupiga, ilipopokelewa alianza kuomba msamaha aliongea maneno mengi ya kujilaumu na kumtaka mkewe kurejea nyumbani. “Wewe ndiyo mume wake?” Upande wapili uliuliza. “Ndiyo! Ndiyo Mimi! Kuna nini kimetokea! Mke wangu kafanya nini?” Aliuliza maswali mfululizo lakini kwa utaratibu upande wapili ulisikika unasema “MImi ni nesi nipo hapa Temeke Hospital mwenye hii simu ame…”

Hakusubiri wala amalizie alianza kupiga kelele kulia kwa uchungu, nguvu zilimuishia na kukaa juu ya kochi la mapokezi. Wafanyakazi wenzake walimsogelea kutaka kujua ni nini, bado alikuwa ameshikilia simu, walichukua na kuongea na mtu wa upende wapili. Baada ya muda alisikia wakimuambia “Unalia nini sasa yaani baada ya ufurahi unalia, Hongera mke wako amejifungua mtoto wa kiume..” Alishtuka sana kwani alihisi ni kitu kibaya, hapo ndipo alipokumbuka kuwa mke wake alikuwa mjamzito.

Alikuwa akimuona kila siku lakini kwakuwa alikua hajali hata alikuwa hajui kuwa ujauzito wa mkewe ulikuwa na muda gani? Akili yake ilishatekwa na mchepuko kiasi cha kuisahau familia yake. Aliendelea kulia kwa uchungu uliokuwa umechanganyika na furaha, alifurahia kuwa mkewe yuko salama lakini alipata uchungu kwa ukatili wake kiasi kwamba ameshaau hata kua mkewe alikuwa amekaribia kujifungua.

Haraka haraka aliingia kwenye gari, akaenda hospitallini kumuomba mkewe msamaha,. watuwa lishangaa kumuona amepiga magoti analia kama mtoto mdogo. mkewe alimuambia nilishjakusamehe muda mrefu, naamini sasa unafahamu thamani ya familia. Alinyanyuka na kukuabli kweli sasa anafahamu maana ya familia, siku ile amejifunza mengi kuliko mambo aliyokuwa amejifunza kwa maisha yake yote. Wlikumbatiana na baada ya kuruhusiwa alirejea nyumbani kwake na mkewe, alibadili tabia na kuwa Mume na baba bora.

MWISHO

Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About