Ulishawahi kupenda kwa namna hii??!!
Ushawai kumpenda dem na kumfia mazima kiasi kwmb anakwambia ye ana msela lkn we huelewi..unamkazia!!
Inabidi dem asisitize,”I HAVE ONLY ONE HEART,PLZ, I CANT LOVE TWO MEN”
Nawewe unaona haiwezekan,unamwambia ‘NIPENDE ATA NA KIDNEY’ππππππππ
BREAKING NEWS!!! Nyoka wa ajabu agundulika
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea⦠huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiβ¦
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Mambo makuu matatu waafrika tusiyoyajua
NIMEKAA NIKAWAZA ππΌ KUWA KUNA MAMBO KAMA MATATU HIVIππ» WAAFRIKA HATUYAJUI π
KAMA TUNGEKUWA TUNAYAJUA HATA HAWA WAMAREKANI,πΊπΈWACHINAπ―π΅ NA HATA WATU WA ULAYA TUNGEKUWAπ½πͺ TUNAWAPITA KIMAENDELEO
MAMBO YENYEWE,,
HATA MIMI SIYAJUI MAANA NA MIMI NI MWAFRIKA ππππ
Ushauri kuhusu mwanamke wa kufaa kuoa
Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara. Yote hayo ni ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Wekeni wivu pembeni na Yafuateni haya;
1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.
2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia “Mimi ni mume wa mtu” au ninae mtu tayari.
3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, “wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao”
4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!
5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.
6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!
7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.
8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!
9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc
10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.
MBARIKIWE SANA WANAUME WOTE WENYE BUSARA..
Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE ili uweze kuwafahamu zaidi wanawake
-
Familia, Mapenzi na Mahusiano
πKitabu cha SIRI ZA MWANAMKEπ§ππ
Original price was: Sh7,500.Sh3,000Current price is: Sh3,000. Download Now
Elimu ya biashara
Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo kwa muda mrefu yamkini unaona panakufaa and you are settled lakini ukweli ni kwamba sio pako na haukutengenezwa kuwa hapo. Hata kama tai ataonekana kwenye banda la kuku lakini ukweli ni kwamba tai kaumbiwa kuwa angani tofauti na kuku aishie bandani. Jiulize hapo ulipo ni pako??
Na ndio maana kwenye maisha, mafanikio ya leo ni matokeo ya tulichojifunza kutoka kwa waliopita, baada ya wao kukosea mahali nasi tukaboresha, na kwa hakika vizazi vijavyo navyo vitaendelea kurekebisha pale tunapokosea sisi na hii yote ndiyo huleta ladha ya maisha. Ukipitia Changamoto mwenyewe na ukapambana kujikwamua mwenyewe, utapata somo litakalokufunza zaidi kuliko kusimuliwa changamoto walizopiti wengine.
Maisha ni Maamuzi, aliyekula Sahani mbili za wali mchana ili usiku asile tena, anaweza kuwa sawa na aliyeamua kutokula Mchana ili usiku ale sahani mbili za wali, japo hawa hawawezi kuwa sawa sawia na aliyeamua kula sahani moja ya wali mchana na moja ya wali usiku, Ijapokua mwisho wa siku wote wamekula sahani Mbili za wali kwa siku. Jumapili Njema kwenu nyote.
JIKUNG’UTEβ¦.JIPANGEβ¦..ANZAβ¦β¦
BADILIKA: Anza kupiga hatua ya maendeleo sasa
Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza.
Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili.
Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:
Swali: “Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka”?
Siku moja wakati nasoma biblia niliona Mungu alipotaka kumtumia Mussa kuokoa wana wa Israel akamuuliza-
βUna nini mkononi mwakoβ-
Mussa akajibu
kwa kudharau alichonacho kuwa βNina fimbo kavu tu ya kuchungia mifugoβ.
Ndipo Mungu alianza kumuonyesha miujiza kutumia fimbo ambayo siku zote
alikuwa nayo na kujidharau ndiyo ambayo ikatumika kwenda kuokoa wana wa Israel.
Watu wengi sana wanashindwa kuanza kwa sababu huwa wanajiuliza-
“Hivi ninakosa nini ili niweze kuanza”
badala ya ‘Hivi nina nini cha kuanzia’.
Cha kuanzia sio lazima iwe pesa-Inawezekana ni uwezo wa kufanya jambo fulani la kipekee,inawezekana ni
mahusiano mazuri uliyonayo na watu fulani(mtandao wako),inawezekana ni uzoefu ulionao,inawezekana ni kipaji n.k
Leo unapoanza siku yako naomba ijiulize-
βNina nini mkononi mwangu ambacho naweza kutumia katika
hatua ya kwanzaβ?.
Kumbuka hakuna mtu ambaye hana
kitu kabisa-KITAFUTE HADI UKIPATE NA ANZA KUKITUMIA KUCHUKUA HATUA.
Share ili wengine wajifunzeβ¦..uwe na Jumatatu njemaβ¦β¦..
Mungu ni mwenye upendo, Huruma na Rehema hasa kwa Wenye dhambi
Mungu ni mwenye upendo Huruma na Rehema hasa kwa Wenye dhambi.
Mungu yupo tayari kumsikiliza mtu yeyote mwenye dhambi kama ameutambua, amekiri na Kutubu makosa yake.
Mungu akishamsamehe mtu uovu wake anambariki.
Hakuna mtu ambaye hatasamehewa na Mungu kama Ametubu, amekiri na Kuomba msamaha wa makosa yake.
Mungu wakati wote yupo akisubiri wenye dhambi waende kwake kwa Toba ili awasemehe.
Lakini tatizo ni la watu wengi wanazani kua wakati wakiwa dhambini Mungu anakua amewakasirikia, Ukweli ni kwamba unapokua dhambini Mungu anakuonea Huruma na anatamani umrudie yeye.
Unaweza ukawa umetenda dhambi lakini hujamuasi Mungu, Kumuasi Mungu ni pale Unapoona kuwa Mungu hana nafasi katika maisha yako tena. Lakini ukiwa dhambini huku unamtumaini Yeye basi bado upo katika njia yake kwa kuwa yeye ni sawa na Baba kwako na kumkosea Baba yako sio kumuasi kama tuu utarudi Kuomba msamaha na Kuheshimu nafasi yake katika maisha yako.
Upendo wa Mungu Kwa Wenye Dhambi
Mungu ni mwenye upendo, huruma, na rehema hasa kwa wenye dhambi. Biblia inatufundisha kwamba Mungu hachoki kuwakaribisha wenye dhambi wanaotubu kwa dhati. Mungu yupo tayari kumsikiliza mtu yeyote mwenye dhambi ambaye ameutambua, amekiri, na kutubu makosa yake. Huruma na rehema zake haziishi kamwe, na anasubiri kwa shauku kubwa kuona wanae wakirudi kwake kwa toba.
“Basi, Bwana, Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli.” (Kutoka 34:6)
“Acha waovu na watu wanaodharau sheria wamrudie Bwana, naye atawahurumia. Warudi kwa Mungu wetu, maana atawasamehe kabisa.” (Isaya 55:7)
“Wote wanaokuja kwangu sitawatupa nje kamwe.” (Yohana 6:37)
Msamaha na Baraka za Mungu
Mungu akishamsamehe mtu uovu wake, anambariki. Hakuna mtu ambaye hatasamehewa na Mungu kama ametubu, amekiri, na kuomba msamaha wa makosa yake. Hii inaonyesha upendo wa ajabu wa Mungu kwa wanadamu wake, upendo ambao haujali ukubwa wa dhambi, bali ukubwa wa toba ya mtu.
“Tubu basi, geuka ili dhambi zako zifutwe.” (Matendo 3:19)
“Na dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kamwe.” (Waebrania 10:17)
“Maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitakumbuka tena.” (Yeremia 31:34)
Mungu Anasubiri Wenye Dhambi Warudi Kwake
Mungu wakati wote yupo akisubiri wenye dhambi waende kwake kwa toba ili awasamehe. Huu ni ujumbe wa matumaini kwa kila mtu anayehisi ameanguka mbali na neema ya Mungu. Mungu ni kama baba anayesubiri mwanae mpendwa arudi nyumbani. Ana shauku ya kumsamehe na kumrejesha kwenye familia ya kiroho.
“Bwana si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa fadhili, husamehe uovu na makosa, lakini hatahesabu kuwa hana hatia mwenye hatia.” (Hesabu 14:18)
“Mkiungama dhambi zenu, yeye ni mwaminifu na mwenye haki, atasamehe dhambi zenu na kuwasafisha na udhalimu wote.” (1 Yohana 1:9)
“Furahini pamoja nami, kwa sababu mwana wangu alikuwa amekufa, naye amerudi tena kuwa hai; alikuwa amepotea, naye ameonekana.” (Luka 15:24)
Wakati wa Dhambi: Huruma ya Mungu
Tatizo ni kwamba watu wengi wanadhani kuwa wakati wakiwa dhambini Mungu anakua amewakasirikia. Ukweli ni kwamba unapokuwa dhambini, Mungu anakuonea huruma na anatamani umrudie yeye. Unaweza ukawa umetenda dhambi lakini hujamuasi Mungu, Kumuasi Mungu ni pale unapomkataa kabisa na kuona kuwa hana nafasi katika maisha yako tena.
“Nanyi mtarudi, na kuona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.” (Malaki 3:18)
“Hata kama dhambi zenu ni nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji.” (Isaya 1:18)
“Bwana ni mwingi wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, ana wingi wa fadhili. Hata mshika hasira yake daima, wala hatawakemea milele.” (Zaburi 103:8-9)
Kurejea kwa Mungu kwa Toba
Ukiwa dhambini huku unamtumaini Mungu, basi bado upo katika njia yake kwa kuwa yeye ni sawa na baba kwako. Kumkosea Baba yako sio kumuasi kama tu utarudi kuomba msamaha na kuheshimu nafasi yake katika maisha yako. Toba ya kweli inarejesha uhusiano wetu na Mungu, na anatupokea kwa mikono miwili.
“Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.” (Zaburi 103:13)
“Nikaribieni mimi, nami nitawakaribia ninyi, asema Bwana.” (Yakobo 4:8)
“Heri wenye huruma, maana hao watapata rehema.” (Mathayo 5:7)
Kwa hivyo, tunapokuwa dhambini, tunapaswa kukumbuka kwamba Mungu anatuona kwa macho ya huruma na upendo. Yupo tayari kutusamehe na kutubariki, mradi tu tutambue dhambi zetu, tukiri, na kutubu kwa dhati. Tunapomrudia Mungu kwa toba, tunapokea huruma na neema zake zisizo na kipimo.
Jipe moyo kamwe usikate tamaa
Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana mmoja juu ya Matokeo ya mchezo.
Kwa tabasamu, alijibu “Wako mbele yetu 3-0”!
Nikasema, Kweli!
Mbona huonekani kukata tamaa..?
“Kukata tamaa?
“Yule mvulana aliuliza kwa mshangaoβ¦.”!?
Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho?
Nina imani na timu yangu na meneja wa timu; Nina hakika tutashinda!
Na kweli, mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele!
Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa, mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; such beautiful faith;
Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi:
“Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?”
Maisha ni kama mchezo.
Kwanini ukate tamaa wakati mwenyezi Mungu ndiye meneja wako?
Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako?
Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa?
Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho.
Lakini maadamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha.
Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.
Usijipulizie kipenga chako cha mwisho we mwenyewe.
JIPE MOYO USIKATE TAMAA!
KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.
KAMWE USIKATE TAMAA.
Ujanja alioutumia msichana wa kazi ili apandishiwe mshahara na mama mwenye nyumba
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshaharaβ¦.. Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatuβ¦β¦.
Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaumeβ¦halafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike.
Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 – 300 ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo).
Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.
Umewahi kuwaza kuhusu hili vizuri?
Yaani ulishindana mbio hizo ukiwa huna macho na ulishinda, ulishindana bila elimu na ukashinda,ulishindana bila hata cheti chochote wala msaada wa yeyote β¦.na UKASHINDA.
Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Tena sasa uko na macho yote, miguu, sasa Unamjua Mungu, sasa ukiwa na mipango,ndoto na maono.
Kumbuka ULISHASHINDA toka tumboni huna sababu ya kuwa na hofu yeyote, PAMBANA
SMS ya kumtumia mpenzi wako kumtakia mahangaiko mema ya kazi
Ukipata tutakula na wala usijali mpenzi wangu.
Ukikosa tutalala na hiyo itabaki siri yanguuuuuuuu.nakupenda mpz
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
SMS nzuri kwa umpendaye asubuhi
, – .(. – .
‘. .’
‘ . . . ‘ Napenda tunda hili likupoze makali uliyo nayo moyoni, Nimeliosha kwa maji safi na salama kwa ajili yako lipo tayari kuliwa.
“APPLE” Ni tunda lenye ishara ya UPENDO, AMANI & FURAHA. napenda liwe zawadi kwako siku hii ya leo.
SALA KWA MT. YOSEFU KUOMBA KUFAHAMU WITO WAKO
Ee uliye Mkuu, Mt. Yosefu, uliyatii kabisa maongozi ya Roho Mt. Unijalie neema ya kufahamu aina ya maisha ambayo Mungu anapenda mimi niishi. Usiniache nidanganyike katika jambo muhimu kama hili, ambalo furaha yangu hapa duniani inalitegemea, na hata pia wokovu wa roho yangu.
Unijalie, nikiangazwa na matakwa matakatifu na nikiwa mwaminifu katika kuyatimiza, nikumbatie aina ya maisha ambayo Mungu ameniandalia na yatakayoniongoza kwenye furaha ya milele.
Amina.
Sala kwa wenye kuzimia
Ee Yesu mwenye huruma, mpenda roho za watu, nakuomba kwa ajili ya kuzimia kwa Moyo wako Mtakatifu, na kwa ajili ya Mama Yako asiye na doa, uwatakase kwa damu yako, watu wote wenye dhambi wanaokufa sasa, na watakaokufa leo.
Moyo wa Yesu uliozomia, uwahurumie watu wanaokufa X3.
Majitoleo ya asubuhi kwa Bikira Maria
Ee Yesu, kupitia mikono safi ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, kazi, masumbuko, na furaha zangu zote za siku hii ya leo, kwa ajili ya nia za Moyo wako Mtakatifu, Ee Yesu ufalme wako utufikie!
Baba Yetuβ¦.
Salamu Maria, β¦..
Nasadiki β¦β¦.
Amri za Mungu β¦β¦
Amri za Kanisa β¦β¦
Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya
KWAHERI MWAKA JANA. UMENIFUNZA MENGI.
Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuingia mwaka mwingine lakini yapo mengi
niliyojifunza mwaka huu na pengine ningepesha
kushare:
1. Kwamba si lazima sana kuwa na rundo la
marafiki kama hawaleti positive effects kwenye
maisha yako. Urafiki wa maongezi yasiyoleta
maendeleo ni uzamani chakavu.
2. Matumizi madogomdogo yasiyo ya lazima
huchelewesha maendeleo makubwa yenye kiu na
mimi. Nmekuwa na matumizi yasiyo ya lazima na
ndio matundu hayo madogo yamezamisha meli.
3. Mungu ndio kila kitu. Anza na maliza siku na
Mungu. Ukikosacho hakukupangia, usiumie,
muombe akuletee atakacho.
4. Harusi zinaumiza. Usipojiwekea kiwango
maalum na idadi ya harusi za kuchangia kwa
mwaka na kwa umuhimu utakuja kujenga nyumba
kwenye harusi za wenzako.
5. Lawama ni muhimu sana ili maisha yaende,
usiogope hasa pale unapokuwa unasimamia lililo
la kimaendeleo kwako. Kumridhisha kila binadam
ni ngumu. Kuna muda ni kwa maendeleo yako
inabidi uwe mbinafsi.
6. Mapenzi ni mazuri ila yasikuzidi ‘kimo’, vipo
vyamaana vya kulilia sio mapenzi. Kikulizacho
ndicho ulichokipa kipaumbele. Mtu aamuapo
kukuliza na wewe ukalia basi umemtukuza.
Mapenzi yasiyosumbua na yaliyojaa mijadala ya
kimaendeleo ndiyo mapenzi yenye afya.
7. Watu waliowengi hasa kwenye mitandao ya
kijamii wana matatzo na ukichaa, usibishane nao
hasa kwenye mambo yasiyokuletea wewe
maendeleo. Usione hasara kuwafanya wajione
washindi.
8. Wazazi ni Muhimu sana, sala zao ni muhimu
kwako. Usipende kuhonga mpita njia akuachaye
siku yeyote ukawasahau wazazi wako. Wapo
watu sikukuu hizi wametumia maelfu ya shilingi
kuhudumia wanawake zao au wanaume zao
wapitaji wakasahau wazazi wao hata kwa pesa
ya dawa.
9. Kuahirisha mambo ni ugonjwa wa kuridhika na
dhiki. Uahirishapo atakaye uwe chini anafurahi.
Muaibishe shetani kwa mipango thabiti.
10. Panga kwaajili ya MWAKA kabla haUjafika,
kupanga kunakupa nafasi ya kujihakiki.
Mpya mwaka wa kucheza na ‘altenatives’.
SEASON GREETINGSβ¦..HAPPY NEW YEAR.
Kukosa hela sio tatizo bali ndio kigezo ya kutafuta hela
Ukimonyesha mtu fursa akakwambiaΒ hana helaΒ mwambie hiyo ndio sababu ya wewe kumonyesha fursa ili awe na hela tukumbukeΒ kuwa hela haitokani na helaΒ hela inatokana na fursa
Nijukumu la mtu asiye na hela kutafuta njia ya kuwa na hela watu wengi tunachelewa kufanikiwa kwa kutojua majukumu yetu ili kupambana naΒ UMASIKINIΒ mwombe MwenyeziΒ MUNGUΒ kwa imani yako akufungue akiliβ¦
To ur Success!
Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida
1.π₯Umejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2.π₯Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3.π₯ Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
4.π₯Umeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.
5.π₯Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.
6.π₯Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema “umefulia”
7.π₯Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.
8.π₯Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako.
9.π₯Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.
10.π₯Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.
ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!
Recent Comments