Jinsi ya kutengeneza mbolea ya maji ya kunyunyiza kwenye majani

Mbolea ya kunyunyiza ni nzuri kwani inasaidia kuupa mmea virutubisho moja kwa moja kupitia kwenye majani au shina ambapo ndipo chakula kinahitajika.

Faida za mbolea ya maji ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha mavuno, uwezo wa mimea kukabiliana na wadudu pamoja na magonjwa, kuvumilia ukame, na kuongeza ubora wa mazao.

Jinsi ya kuandaa mbolea ya maji kwa kutumia samadi

Mbolea ya maji hutengenezwa kwa kuchukua kiroba kilichojazwa samadi, aina mbalimbali ya mimea yenye virutubisho na inayoaminika kuwa dawa ya mimea. Kiroba hicho kinafungwa kwenye kijiti, na kutumbukiza kwa kuning’inia kwenye pipa lililojazwa maji.

Kiroba hicho ni lazima kichukue kati ya kilo 30-50 za samadi pamoja na aina nyingine za mimea kwa maji lita 200 (tazama mchoro). Unaweza kushika upande mmoja wa mti na kunyanyua na kushusha kila baada ya siku tano ili kuchanganya na kuharakisha kutolewa kwa virutubisho zaidi.

Kwa kawaida mchanganyiko huo unakuwa na harufu kali sana maana Nitrojeni nyingi inayopatikana hugeuka kuwa Amonia. Ni vizuri kufunika pipa ili kuzuia kuyeyuka kwa nitrojeni. Harufu ikishaisha, ujue mbolea yako ipo tayari kwa matumizi.

Ongeza maji na utingishe vizuri kabla ya kutumia. Nyunyizia mimea yako kila wiki mpaka utakapoona mabadiliko.

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya maji kwa kutumia mimea peke yake (Majani fresh)

Mbolea hii hutengezwa kwa kuchukua majani mabichi na kuyakatakata na kisha kuyachanganya na maji kidogo.

Baada ya kuchanganya na maji unaacha kwa siku tatu au nne ambapo utatikisa mchanganyiko wako kila siku.

Baadae utatikisa na kuchanganya na maji na kunyunyiza shambani.

Vilevile Unaweza kutumia mbolea ya majani ambayo itakuwa kama dawa ya kuulia wadudu, kwa kutumia aina ya mimea kama vile mivule, mibangi mwitu, majani ya minyanya, mwarobaini, mashona nguo, pamoja na vitunguu saumu. Aina hii ya mimea inasaidia sana katika kuzuia magonjwa, wadudu na kutoa virutubisho muhimu kwa mimea vinavyosaidia mkulima kupata mazao bora bila gharama ya ziada ya kununua virutubisho.

Vigezo vya kunyunyiza mbolea ya maji

Ili upate matokeo mazuri wakati wa kunyunyiza mbolea ya maji unatakiwa kufuata vigezo vifuatavyo:
β€’ Inashauriwa kutumia mbolea iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea.
β€’ Acha maji utakayotumia kuchanganyia mbolea yako nje katika pipa lililowazi usiku kucha, hii inasaidia kutoa madini hatarishi, na kufanya mchanganyiko wenye faida kwa mimea.
β€’ Unatakiwa kutingisha vizuri mbolea yako ya maji kabla ya kunyunyiza. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
β€’ Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
β€’ Unatakiwa kunyunyizia mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.

Angalizo
Kabla ya kunyunyiza dawa au mbolea uliyoitengeneza mwenyewe shambani nyunyiza kwenye eneo dogo au mimea michache kwanza ili uone kama inaunguza au haiunguzi. Kumbuka kuwa mchanganyiko mwingine ukiwa cream au ukikolea sana unaweza kuchoma. Kwa hiyo kuepuka hili nyunyiza mahali padogo kwanza.

Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku

Mbinu hizo ni hizi zifuatazo;

Namna ya kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa banda la kuku kuzuia magonjwa

Ukaguzi wa Kila siku
β€’ Hakikisha unasafisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.
β€’ Ondoa kinyesi kwa kuku.
β€’ Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao. Yaani ili kutambua kama kuna mwenye ugonjwa

Ukaguzi Kwa wiki
β€’ Ondoa matandazo machafu na kuweka mapya ili kuzuia kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa.

Ukaguzi kwaKwa mwezi
β€’ Angalia uwepo wa wadudu na chawa, kisha utibu kama kuna ulazima.

Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng’ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo hayo ni haya yafuatayo;
1. Hakikisha unaondoa matandazo yote ndani ya nyumba,
2. Ondoa vyombo vya kulishia na kunyweshea.

3. Ondoa uchafu wote unaoonekana bandani.
4. Safisha banda lote kwa kutumia maji na dawa.
5. Suuza na uache likauke.
6. Puliza dawa ya kuua wadudu.
7. Weka matandazo mapya,
8. Weka viombo vya kulishia na kunyweshea.

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa

2. Nyumba ya kuku iwe na nafasi za kupitisha hewa ya kutosha ili kuepuka joto na unyevunyevu ambao unachangia uwepo wa magonjwa kwa kuku

3. Hakikisha unaondoa matandazo na takataka zote kwenye banda wakati wote hasa yenye unyevu.

4. Fagia banda na kuhakikisha ni safi wakati wote. Weka matandazo mapya mara kwa mara.
5. Weka sehemu za kutosha kuku kupumzikia.
6. Weka viota vya kutosha.
7. Weka maji sehemu ambayo ni rahisi kusafisha.
8. Hakikisha unaondoa wanyama kama panya na wadudu nyemelezi kwenye sehemu ya malisho ya kuku kwani wao hubeba vimelea vya magonjwa.

Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa

1. Zingatia chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo.
Chanjo huanza katika wiki ya kwanza (mfano chanjo ya kuzuia sotoka) na inaweza kurudiwa baadaye.

2. Epuka kuweka kuku wengi mahali pamoja.
Ni rahisi magonjwa kuenea kwa haraka kuku wanaporundikana.

3. Kumbuka kutenganisha vifaranga na kuku wakubwa (isipokuwa kutoka kwa mama) kwa sababu vifaranga ni rahisi na wepesi sana kushambuliwa na magonjwa.

4. Hakikisha unaweka mipaka na madaraja ya sehemu za kuku kuzunguka/kucheza.

Namna ya kulisha kuku ili wasipatwe na magonjwa

Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea kila siku. Osha, sugua vizuri, kisha suuza kuondoa utando unaobeba bakteria.

Kuku wanahitaji wapewe chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote. Unaweza kuwaongezea majani, makombo, nafaka, mchanga laini, au maganda ya mayai.

Wapatie kuku maji safi muda wote. Wafugaji wengi wameripoti kuwa na matokeo mazuri baada ya kuchanganya dawa ya kuua vimelea kwenye maji ya kunywa.

Nunua chakula kwa wauzaji wazuri na wanaoaminika ili kuepuka minyoo na sumu hatarishi. Usiwape kuku chakula chochote kinachoonekana kuoza au kunuka uvundo.

Hifadhi chakula cha kuku katika sehemu kavu isiyo na joto na isiwe kwa zaidi ya miezi mitatu ili kuepuka kuharibiwa na fangasi.

Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku

Hakikisha unamuona mtaalamu wa mifugo mara uonapo dalili zozote za kuumwa kwa mifugo wako.

Tenga na wapatie tiba au kuwaua na kuteketeza kabisa kuku wagonjwa kuepuka kuenea kwa magonjwa.

Ondoa ndege waliokufa mara moja, uwafukie au kuchoma moto. Usile kuku aliekufa. Baadhi ya magonjwa ya ndege yanaweza kuambukizwa kwa binadamu.

Endapo kuna mlipuko wa ugonjwa katika eneo lako, usiruhusu watu kutembelea banda lako. Watu wanaweza kuleta maambukizi kwa miguu yao katika mabuti, nguo na mikono.

Pia magari yanaweza kuleta madhara kwa mabanda yako kupitia matairi na upakuaji wa mizigo.

Namna ya kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa banda la kuku kuzuia magonjwa

Ukaguzi wa Kila siku
β€’ Hakikisha unasafisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.
β€’ Ondoa kinyesi kwa kuku.
β€’ Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao. Yaani ili kutambua kama kuna mwenye ugonjwa

Ukaguzi Kwa wiki
β€’ Ondoa matandazo machafu na kuweka mapya ili kuzuia kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa.

Ukaguzi kwaKwa mwezi
β€’ Angalia uwepo wa wadudu na chawa, kisha utibu kama kuna ulazima.

Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina ya mbegu ya kuku yenye sifa ya kutaga mayai mengi kama haitapewa matunzo mazuri Β basi sifa yake ya utagaji itapotea.

Kwa kawaida Tetea anatumia muda wa masaa 24 – 27 (siku moja) kutengeneza yai. Hakuna njia ya kupunguza muda huu (yaani atengeneze mayai miwili katika siku moja). Hiyo ndio asili yake. Njia Nzuri ya kumfanya kuku atage muda mrefu ni kumfanya awe na furaha na afya.

Njia za kuwafanya kuku wawe na furaha na afya:

1. Wape chakula bora chenye virutubisho vya kutosha. Usichakachue chakula chao hawatataga.

2. Viota vyao viwe safi. Safisha viota vyao mara kwa mara ili watage sehemu safi.

3. Wawe na sehemu ya wazi ya kuzunguka zunguka na kuparua parua.

4. Wawekee calcium ya kutosha kwenye chakula chao ili mayai wanayotaga yawe na gamba gumu.

5. Wachunguze mara kwa mara
kama wana dalili za kuumwa, na endapo dalili zipo watibu mara moja.

6. Wapatie maji safi kila siku. Pia safisha vyombo vyao kwa sabuni kila siku.

7. Hakikisha banda lao ni safi muda wote ili kusiwe na wadudu kama viroboto, chawa na papasi. Wadudu hawa huwasumbua kuku na kuwafanya wapunguze kutaga.

8. Hakikisha kuku hawapati msongo/stress, mfano kusiwe na wanyama wa kuwatisha wanaopita au kuingia bandani kwao.

9. Chagua aina ya kuku wanaotaga mayai mengi.

10. Umri wa kuku. Kuku wenye umri wa miezi 6 – 18 wanataga sana. Wakiwa na miezi 19 – 24 wananyonyoka manyoya (Annual Molt), hivyo hupunguza kutaga, na wakianza kutaga tena, wanataga mayai makubwa na machache kuliko mwanzo.

11. Wasihamishwe hamishwe banda. Kuku hutaga vizuri zaidi wakiwa kwenye mazingira waliyoyazoea.

12. Walishe mboga za majani za kutosha.
Kumbuka: Kuku wenye furaha na afya ndio watakaotaga sana kwenye maisha yao.
Note: Wakati mwingine inadhaniwa kwamba Jogoo anaweza kumsaidia Tetea kutaga mayai mengi. Jogoo hawezi kuongeza utagwaji wa mayai, lakini anahitajika kuyarutubisha mayai (kuyafanya yawe na mbegu). Kama kuku wako anataga mayai machache, kuongeza Jogoo hakutamfanya Tetea atage mayai mengi.

Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Muhogo Inazuia Minyoo na vidukari.

Hatua za Kutayarisha dawa

  • Toa maji ya matunda kwa kuponda mizizi;
  • Pima k i w a n g o kimoja cha maji ya m a t u n d a sawa na maji ya kawaida (1:1).
  • Nyunyiza haraka ukitumia lita nne kwa mita moja za mraba, inasemekana kuwa na athari kubwa.
  • Subiri kwa siku ishirini kabla ya kupanda.

Angalizo:Β Tafuta ushauri wa mtaalamu wa kilimo kabla ya kutumia dawa yoyote ya asili

Jinsi ya kutumia mashonanguo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Mashonanguo kwa kiingereza ni Blackjack au kwa kisayansi yanajulikana kama (Bidens
pilosa)
Mashona nguo yanazuia wadudukama vile Vidukari, Siafu, bungo, katapila, chenene (crickets), nyenyere, siafu na inzi weupe.

Jinsi ya Kutayarisha na kutumia mashonanguo

  1. Jaza kikombe kilichojaa mbegu ambazo zimekomaa na maji;
  2. Chemsha kwa dakika kumi au loweka kwenye maji kwa saa ishirini na nne, kisha upooze.
  3. Ongeza lita moja ya maji na kijiko kimoja kidogo cha sabuni;
  4. Kisha unyunyizie mimea.

Matumizi mengine

  1. Mbegu zinaweza kutawanyishwa karibu na vichaka kuvutia mchwa.
  2. Mmea waweza kupondwa au kufikichwa kisha maji yake yatumike kunyunyizia mimea.

Angalizo: Kiasi kingi cha dawa hii chaweza kudhuru baadhi ya maua ya mimea.

Jinsi ya kuandaa mbangimwitu kama Dawa ya magonjwa na ya kuulia wadudu shambani

Mbangi mwitu au kwa kisayansi ni African marigold / (Tagetes erecta) Unazuia Bakteria, fungusi na wadudu kama vile Siafu, bungo pamoja na aina nyingine za wadudu.

Hatua za Maandalizi ya dawa na kutumia

  1. Ponda gramu 100-200 za matawi, mizizi na maua;
  2. Weka lita moja ya maji yaliyochemka;
  3. Loweka kwa masaa ishirini na nne;
  4. Ongeza lita moja ya maji baridi,
  5. Nyunyiza kwenye mimea au mchanga.

Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Maharagwe yanapandwa kwenye kabichi yanafanya kazi zifuatazo;

Kudhibiti wadudu (mtego).

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Kuboresha udongo.

Maharagwe yanaongeza nitrojeni kwenye udongo

Chakula cha mifugo.

Maharagwe yanaweza kutumika kulishia mifugo kama ng’ombe mbuzi na kondoo.

Matandazo.

Maharage yanaweza yakatumika kama matandazo kwenye shamba kusaidia kulinda unyevu.

Kutengenezea mbolea.

Maharagwe yakioza yanaweza kuwa mbolea nzuri ya shamba lako

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.

Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.

Safu za mbaazi zimekuwa zikitumika kulinda nyanya, viazi, kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharagwe yanapandwa kama mtego kwenye kabichi lakini yanafanya kazi ya kudhibiti wadudu (mtego), kuboresha udongo, chakula cha mifugo, matandazo au kutengenezea mbolea.

Vile vile wigo wa mimea ni makazi ya wanyama/wadudu wanaowinda.

Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na wengi. Gharama yake ni ndogo kiasi kulinganisha na mingine. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni wa gharama nafuu. Mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga Yya aina hii mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala.

 

Mzinga wa Top bar

Faida ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)
β€’ Ni rahisi kukagua asali iliyo tayari.
β€’ Ni rahisi kuvuna asali kuliko kuvuna toka kwenye mzinga wa kienyeji.
β€’ Ni rahisi kuwatunza nyuki wakati wa kiangazi na inapokuwa hakuna maua. Kwa mfano unaweza kuwapatia nyuki chakula ili kuongeza uzalishaji wa asali.
β€’ Ni rahisi kurina asali ukilinganisha na mizinga ya magogo inayotundikwa juu ya mti, kwa kuwa haihitaji vifaa maalumu.
β€’ Aina hii ya mizinga huwekwa kwa kuninginia jambo ambalo siyo rahisi kushambuliwa na wadudu/wanyama wanaokula asali kwa kuwa Inajaa haraka sana wakati ambao ni msimu wa asali kutengenezwa kwa wingi.

Hasara ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)
β€’ Kichane kwenye mzinga wa boksi hakina kishikizo hivyo huvunjika kwa urahisi sana kama hakitashikwa kwa uangalifu.
β€’ Masega huvunwa pamoja na asali, kwa hiyo nyuki wanalazimika kutengeneza tena masega mengine ambapo husababisha kupungua kwa uzalishaji wa asali.

Mzinga wa Langstroth

Mzinga wa Langstroth unaweza kukupatia asali zaidi kulinganishwa na mizinga mingine Hii ni aina nzuri na rahisa sana ya mzinga. Mizinga hii hufahamika kama mzinga wa fremu, kwa kuwa ina fremu ambazo vichane vya masega hujishikiza. Chumba kikubwa ambacho malkia hutagia mayai. Malkia anazuiliwa kuhama kwenda chumba kingine kwa kutumia waya. Kwenye chemba maalumu ya kutagia juu yake pana chemba ya kuhifadhia asali.

 
 

Mzinga wa Langstroth

Vichane vya masega vinatengezwa kwenye fremu na si kwenye nguzo kama ilivyo kwenye Top bar. Ili kuvuna asali, mfugaji akiwa na masega yaliyojaa asali, hutumia vifaa maalum kwa ajili ya urinaji na kuhifadhi asali bila kupata tabu.

Mzinga wa Langstroth ni gharama kiasi kulinganisha na mizinga mingine.Unaweza kuipata kutoka katika taasisi zinazojiusisha na uuzaji wa mizinga, taasisi na karakana binafsi, au wakala wa Serikali.

Mambo 5 ya muhimu kuzingatia kuhusu mahali unapotaka kuweka mizinga ya nyuki

Ukitaka kujua kuwa eneo unalotaka kuweka mizinga ya nyuki ni sahihi unatakiwa kuzingatia yafuatayo:

1. Haishauriwi kuweka mzinga shambani au karibu na shamba. Unatakiwa uweke umbali wa mita 150-200 kutoka kwenye mazao au nyumbani. Hii ni Kulingana na hali ya kujilinda ya nyuki wa Afrika

2. Mzinga ni lazima uwekwe sehemu ambayo haitasababisha upotevu wa nyuki wanaporudi kutoka nje ya mzinga. Mfano wasiingie kwenye kundi lisilokuwa lao.

3. Mizinga inatakiwa isiwekwe mbalimbali sana ili kuepusha usumbufu wa kutembea mbali kwa mfugaji wakati anapokagua.

Sifa ya eneo la kuweka mizinga
β€’ Iwe Kimya na mbali ya jumuia kama vile hospitali, shule, na viwanja vya michezo vile vile isiwe karibu na maeneo ya biashara au viwanda.
β€’ Karibu na maji masafi-kandokando ya mto, mabwawa ya samaki, mabeseni ya maji au sehemu ya matone.
β€’ Sehemu ya kuweka mizinga Iwe ni karibu na chakula cha nyukimimea inayochanua, miparachichi, nazi, euculptus, migunga n.k
β€’ Iwe sehemu ambayo ni kavu na isiwe sehemu ya tindiga kwani unyevu unyevu husababisha ugonjwa wa ukungu (magonjwa ya fangasi yaani fungal disease) na pia huzuia utengenezaji mzuri wa asali.
β€’ Mahali pa mizinga pawe mbali na watu waharibifu na iliyojificha kuepuka waharibifu.
β€’ Sehemu ya kuweka mizinga ni lazima iwe inafikika kirahisi kwa kipindi chote cha mwaka ili iwe rahisi kuhamisha nyuki pale inapohitajika.
β€’ Panatakiwa pawe kivuli cha kutosha hasa wakati wa mchana jua linapokuwa kali, na kusiwe na upepo mkali.

4. Mizinga ya nyuki Iwe mbali na mashamba, ambapo dawa za kuulia wadudu zinatumika.

5. Vichaka au wigo unaotenganisha mizinga na kuzuia wavamizi ni muhimu ili kupunguza ukali wa nyuki.

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Mtaalamu wa nyuki

Unapohitaji unahitaji kufuga nyuki ni lazima uwe na uelewa wa mzunguko wa maisha ya nyuki. Unapoanza ni lazima uulize mtaalamu wa nyuki, wafugaji wenzako ambao wana uzoefu wa kutosha, au kujiunga katika kikundi cha ufugaji ili apate ufahamu zaidi juu ya ufugaji wa nyuki.

Sehemu salama kwa ajili ya mzinga

Unahitaji kutafuta mahali pazuri, salama, na penye sifa ya kufugia nyuki. Vifaa vyote vikishapatikana kinachofuata ni kuchagua mahali gani pa kuweka mzinga. Hakikisha sehemu hii ni mahali ambapo makundi ya nyuki hukusanyika mara kwa mara.

Uwekaji Bora wa Mizinga

Ukishatafuta ya sehemu ya kuweka mizinga, kinachofuata ni kuandaa mizinga kwa ajili ya kuweka panapotakiwa.

Mambo ya muhimu ya kuzingatia
β€’ Kwanza Safisha mzinga kuondoa uchafu wote, utando wa buibui na aina nyingine za wadudu.
β€’ Kisha Weka chambo kwenye mzinga (maranyingi nta hutumika kama chambo) kwa kuipaka katika kuta za mzinga kwa ndani.
β€’ Halafu Mzinga unaweza kutundikwa kwenye mti, kwenye nguzo, kuweka kwenye jukwaa au kwenye miamba. Hii inategemea wewe mwenyewe anapendelea njia ipi.

Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.

Umuhimu wa kutifua udongo ni kama ifuatavyo
1. Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
2. Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.
3. Kunawawezesha viumbe hai waliopo kwenye udongo kufanya kazi zao ipasavyo.
4. Kunasaidia Kuandaa sehemu ya kuwekea mbegu.
5. Kutifua kunauongeza uwezekano wa maji kupenya kwenye udongo na kupunguza uyeyukaji wa maji.
6. Kuchanganya mabaki ya mimea na samadi kwenye udongo

Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi

Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.

Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?

Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.

SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Hii ndio ndoto ya harusi ya kila msichana anayotamani

GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee…
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome…
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula….
GIRL: Enhee…na sisi??

BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas….halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart…halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo

Mume mgonjwa kazua mpya baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali alipokuwa kalazwa

John aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya
Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na
nyumbani kwake, akaulizwa kwako unapakumbuka?

akajibu ndio nyumba yangu ilee, mara wakatoka
watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto
wangu walee wanakwenda shule..
Akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee,
Ghafla akatoka mwanaume john akasema mimi
yuleeeeeeee…. naenda kazini!! JE, NI KWELI
AMEPONA??

Huyu mchaga kazidi sasa, angalia anavyomfanya huyu mbuzi

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!

Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About