Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Featured Image

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana

1. Kama uko shule au chuo soma na usicheze ukifeli unajipotezea muda. Soma sana utafanikiwa…

2. Jifunze kuweka akiba ya pesa. Pia jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa,bajeti vizuri na jiwekee akiba bank au popte unapoona panafaa.

3. Jitengenezee good character yaani tabia yako njema ili uwe tofauti na wengine.. Jitofautishe na wengine, uwe mfano bora

4. Jifunze kufanya kazi tofauti tofauti. Fanya hiki ama kile ili angalau uweze kuishi popote kwani dunia inabadilikaa na huwezi jua kesho yako

5. Anza kununua na kumiliki vitu kama kitanda godoro vyombo na ardhi au kiwanja. Kumbuka msingi mzuri wa maisha ni fikra za ujana na kujiwekea mali

6. Kama utaweza kapange ujifunze maisha. Anza kujitegemea ili kujipa confidenece na maisha.

7. Weka falsafa yako katika maisha na uiishi. Falsafa ni dira ya kukuongoza. Mfano unataka kumiliki nini katika maisha? Unataka mke au mume wa aina gani? Aina gani ya maisha unaipenda? Hiyo ndiyo falsafa…

8. Tengeneza mahusiano yaliyotulia na weka malengo. (Kwa wale wa ndoa) Jichagulie kijana au binti aliyemzuri katika wengi, kijana au binti wa moyo wako, mpende… Kipindi hiki ni cha kuwa na mwenza aliyetulia kama unafikiri kuoa au kuolewa. Ukicheza ukafikisha 30 bila kuwa na mtu maaalumu basi utaoa au kuolewa bora mradi ila siyo na mtu wa ndoto yako..

9. Kuwa na marafiki imara, jichagulie katika wengi marafiki kadhaa waliotulia wenye nidhamu ya maisha na wanaopenda uende mbele. Kijana chunga marafiki ulionao wengi leo wanajuta kwaa urafiki m'baya uliowapoteza… a

10. Kumbuka ibada na kumshukuru Mungu. Kipindi hiki ni cha misukosuko na mihemko mingi. Usiache mafundisho ya imani yako, usimsahau Mungu. Mshukuru Mungu kwa uhai na kila jema au baya likupatalo.

11. Jitume katika kazi, watu waliofanikiwa wanajua thamani ya juhudi na kujituma. Usikate tamaa hata kama unapata kidogo. Fanya kazi kama vile kesho haipo. Matunda utayaona

12. Zingatia kujiweka safi. Kuwa msafi na mtanashati huanza na ubongo, muonekano wako ndivyo watu watakavyo kuchukulia. Jiweke safi na jitunze..

13. Kula kwa afya, wengi wanachukia miili yao. Wanauchukia aidha unene au wembamba, ila ukila kwa afya, ukafanya mazoezi unatengeneza afya bora ya sasa na baaadae..

14. Vaa kwa heshima, usivae kama mcheza disko au teja. Kumbuka thamani yako kwa Mungu. Kwanini uvae nguo za machukizo mbele yake! Kwanini ukubali kuwa wakala na kutumiwa na shetani kuwaaangamiza wengine kwa kuvaa ovyo? Vaa kwa heshima..

15. Pendelea kusafiri maeneo tofauti na ujifunze! Asafiriye hupata maarifa na hujifunza mengi. Penda kusafiri, tembelea maeneo tofauti utakuwa na mengi ya kujifunza.

16. Kumbuka kupumzisha mwili. Kuishi kwetu kupo katika chembe ya uhai iliyopo mwilini. Upe mwili na ubongo chakula chake cha kupumzika. Nenda maeneo yatakayofanya mwili na akili vipumzike angalau kila baada ya miezi kadhaa..

17. Jifunze kuamua mwenyewe. Usisubiri kila kitu kumshirikisha mtu ndio uamue. Jifunze kuwa mwamuzi wa mambo yako mwenyewe haijalishi kwa gharama ipi. Watu wawe washauri ila ubaki kuwa mwamuzi mwenyewe.

18. Kuwa mtu wa kutunza siri. Jitahidi kuwa na shingo nzito na akili yenye kuweka siri. Usiwe mtu wa kusema kila uonacho au uambiwacho.

19. Jfunze na zitawale hisia zako. Hisia ziwe za hasira, mapenzi au ugomovi zitawale na utaishi miaka mingi. Asiye tawala hisia zake hata awe mkubwa bado ni mdogo…

20. Jitolee kwaajili ya wengine, fundisha kemea saidia. Unaweza kufundisha kupitia facebook wasap nk. Kemea ukiona mtu anafanya kitu kibaya, saidia wenye shida wakumbuke wagonjwa yatima wazee na wenye mahitaji. Wewe ni yatima, mzee, au muhitaji wa kesho.. Weka akiba ya wema

21 Jenga mazingira ya kuishi na watu vizuri. Usijione mzuri au HB sana ukadharau wengine. Ishi na kila mtu kwa upendo hata kama wanakuchukia..

22. Tunza muda, muda ni mali huwezi kuurudisha, kuusimamisha au kuuzuia. Ukishapotea ndio basi tena. Tambua thamani ya muda na fanya vitu kwa wakati..

23. Pendelea kusoma hasa vitabu vya dini, kuhusu mali, elimu, mchumba, afya, maisha, uongozi, hekima, busara, utu, uchaji, utii, maarifa, utajiri, heshima, uvumilivu, matumaini, upendo, na kila kitu vimo katika Biblia na Qur'an ..soma uchote hekimaa…

24. Acha kujifunza matumizi ya pombe, sigara , dawa za kulevya. Kama unatumia jitahidi uache, kama unajifunza acha na kama kuna mtu anakushawishi kataa. Afya ni mali na mtaji usichoshe na kuumiza uhai wako kwa pombe sigara na madawa ya kulevya…

Inafaa ukishare kwa wengine wajifunze maarifa haya..
*Maisha ni maamuzi yako wewe*
Kuamua kufanikiwa au kushindwa,
kuamua utajiri au umasikini yote ni mipango na hutokana na fikra zako..

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Ukitaka kujua Simu ya Kichina utajua tu jinsi ilivyo na makelele mengiiiii sana wakati wa kuitaâ€... Read More

Mambo 7 ambayo mwanamme hapaswi kumfanyia mke wake

Mambo 7 ambayo mwanamme hapaswi kumfanyia mke wake

Mambo 7 ambayo mwanaume apaswi kumfanyia mke wake..
1. Usimpige.
2. Usimtukane na kumshushi... Read More

Kuwa na msimamo katika mahusiano

Kuwa na msimamo katika mahusiano

Sio Kila EX Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha! Wengine Huomba Kurudi Ili Wakutesti Tu Jinsi Uli... Read More

Jinsi ya Kukuza Heshima na Uaminifu katika Mahusiano ya Familia

Jinsi ya Kukuza Heshima na Uaminifu katika Mahusiano ya Familia

Mahusiano ya familia ni muhimu sana kwani ndiyo yanayotufanya tuwe na furaha na amani katika mais... Read More

Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Mahusiano ya familia ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Kuwa na heshima na uwiano ka... Read More

Je, inawezekana kujisikia huru kuelezea tamaa zako za ngono/kufanya mapenzi kwa mwenza wako?

Je, inawezekana kujisikia huru kuelezea tamaa zako za ngono/kufanya mapenzi kwa mwenza wako?

Karibu kwenye makala hii kuhusu swali la iwapo inawezekana kujisikia huru kuelezea tamaa zako za ... Read More

Uhusiano wa Kudumu: Siri za Furaha ya Ndoa ya Muda Mrefu

Uhusiano wa Kudumu: Siri za Furaha ya Ndoa ya Muda Mrefu

Uhusiano wa kudumu ni jambo muhimu sana katika mahusiano ya ndoa. Ndoa ya muda mrefu ni ngumu san... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Ukarimu na Upendo katika Familia yako

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Ukarimu na Upendo katika Familia yako

Familia ni muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunapata upendo, msaada, na faraja. N... Read More

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiri... Read More

Jinsi ya Kusaidiana katika kujenga na kudumisha afya na ustawi na mpenzi wako

Jinsi ya Kusaidiana katika kujenga na kudumisha afya na ustawi na mpenzi wako

Kusaidiana katika kujenga na kudumisha afya na ustawi na mpenzi wako ni muhimu kwa uhusiano wenye ng... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kushughulikia matatizo ya kifamilia

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kushughulikia matatizo ya kifamilia

Karibu sana katika makala hii ambapo tutaangalia jinsi ya kusaidiana na mpenzi wako katika kushug... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Mahusiano ... Read More