Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kuweka Mipango ya Pamoja na Malengo katika Mahusiano yako

Njia za Kuweka Mipango ya Pamoja na Malengo katika Mahusiano yako

Mahusiano ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Kama tunavyojua, ili kufanikiwa katika mahusiano yetu,... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Uwazi katika Familia: Kuweka Nafasi ya Mazungumzo na Ufahamu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Uwazi katika Familia: Kuweka Nafasi ya Mazungumzo na Ufahamu

  1. Familia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu na inaweza kuathiri sana maendeleo yet... Read More

Kuhamasisha Mawasiliano Bora na Kusikilizana katika Familia Yako

Kuhamasisha Mawasiliano Bora na Kusikilizana katika Familia Yako

Kuhamasisha Mawasiliano Bora na Kusikilizana katika Familia Yako

Ili kuwa na familia yenye... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Mipaka na Heshima katika Mahusiano

Kujenga Ushirikiano wenye Mipaka na Heshima katika Mahusiano

Kujenga Ushirikiano wenye Mipaka na Heshima katika Mahusiano

Kutafuta mtu ambaye tutaweza ... Read More

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

  1. Kuwasiliana kwa Ukaribu Ha... Read More

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kila mtu anatamani furaha katika mape... Read More

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Ubunifu katika Mahusiano yako

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Ubunifu katika Mahusiano yako

Mahusiano ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Hata hivyo, mahusiano hayawezi kuwa ya ... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ukaribu wa Kihisia katika Mahusiano yako

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ukaribu wa Kihisia katika Mahusiano yako

Mahusiano ni jambo muhimu sana katika maisha yetu na yanahitaji kipaumbele cha kujenga ukaribu wa... Read More

Je, nini imani ya watu katika kutumia michezo ya ngono/kufanya mapenzi kama njia ya kuimarisha uhusiano wako?

Je, nini imani ya watu katika kutumia michezo ya ngono/kufanya mapenzi kama njia ya kuimarisha uhusiano wako?

  1. Je, ni sahihi kutumia michezo ya ngono/kufanya mapenzi kama njia ya kuimarisha uhusiano wak... Read More
Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi

Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mapenzi, il... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na maadili ya familia

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na maadili ya familia

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na maadili ya familia ni muhimu kwa kujenga msingi imara k... Read More
Njia za Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Njia za Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Leo, tutajadili njia za kuunda uhusiano mzuri na wa furaha na msichana. Kuwa na uhusiano mzuri na... Read More