Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Featured Image

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call.

Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili. Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wanafanya.

Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa. Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili (Receptors) vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.

Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani, automatic, kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha Ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa Ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo. Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika kuvumilia kidogo ili afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena na kujikuta muda mdogo tu….mtu tayari kaloanisha nguo yake.

Mpenzi msomaji, mtu kujibana na kupuuzia kwenda kukojoa husababisha uwezo wa kibofu cha mkojo kujitawala (control) upotee. Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi misuli maalumu ya kubana mkojo (sphincter) itashindwa kuachia na matokeo yake mtu ataendelea kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu ambacho ni hatari kwa afya yake. Endapo mkojo huu utashindwa kutoka, utatengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection). Magonjwa ya kibofu cha mkojo ni pamoja na U.T.I (Urinary Tract Infections), pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na mchafuko wa damu, bacteremia.

Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu, yawezekana alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila akinywa maji au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka bombani, basi atahisi kwenda kukojoa.

Mpenzi msomaji, ni vyema tukawa wasikivu pale mtu unapobanwa na mkojo, hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo, usisite kuonana na wataalamu wa afya.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Dalili za kuharibika kwa Mimba

Dalili za kuharibika kwa Mimba

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni... Read More

Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids.... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia tango

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia tango

Tango ni tunda na ni mboga pia na ni chanzo kizuri cha potasiamu na vitamini nyingi ambazo zina k... Read More

Faida za kula mayai asubuhi

Faida za kula mayai asubuhi

Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku wat... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi za usoni kwa kutumia Parachichi na asali

Jinsi ya kutibu chunusi za usoni kwa kutumia Parachichi na asali

Unahitaji:

a)Kijiko kimoja cha asali
b)Parachichi 1

Hatua kwa hatua namna ya ... Read More

Mambo 10 yanayosababisha wanawake washindwe kupata mimba au wawe wagumba

Mambo 10 yanayosababisha wanawake washindwe kupata mimba au wawe wagumba

Ugumba ni nini ?
Hii ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito. Ugumba unaweza kua... Read More

UJUE NA UFAHAMU MFUMO WA MOYO (CARDIOVASCULAR SYSTEM)

UJUE NA UFAHAMU MFUMO WA MOYO (CARDIOVASCULAR SYSTEM)

Mfumo huu wa moyo una kazi zifuatazo:-

👉kupampu damu Mwilini pia kusafirisha gas, taka n... Read More

Faida za mafuta ya nazi kiafya kwenye mwili

Faida za mafuta ya nazi kiafya kwenye mwili

Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu

Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’en... Read More

Madhara ya kuwa mnene kupindukia

Madhara ya kuwa mnene kupindukia

Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara makubwa kiafya hata ... Read More
Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka

Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka

Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamin... Read More

Mambo ya Msingi kuyajua kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu

Mambo ya Msingi kuyajua kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu

Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupi... Read More
Jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia ugonjwa wa moyo

Jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia ugonjwa wa moyo

Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu ku... Read More