Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Faida za kula karanga mbichi

Featured Image

Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama nitakavyokujuza leo katika makala haya.

1. Kwanza kabisa karanga husaidia katika kutibu magonjwa ya moyo.

Kama ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya monounsaturated fats’ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular heart disease).

Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la ā€˜Journal of Nutrition’ ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.

Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa kinga kwenye moyo, karanga pia, zinaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyotoa kinga ya mwili (antioxidants) kuliko hata kile kinachopatikana kwenye tunda la epo na karoti!

Ili kupata kinga hiyo dhidi ya aina hizo mbili za ugonjwa wa moyo, ambao unatesa watu wengi duniani na kugharimu pesa nyingi kwa matibabu, unashauriwa kula karanga pamoja na bidhaa zake kama vile peanut butte, angalau kijiko kimoja cha chakula, mara nne kwa wiki.

2. Kinga dhidi ya kiharusi.

Ugonjwa mwingine hatari unaosumbua watu wengi hivi sasa ni kiharusi au stroke’, lakini unaweza kujikinga nao kwa kuwa na mazoea ya kula karanga tu.

Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya Resveratrol ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu (red wine). Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry),

umeonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.

3. Kinga dhidi ya magonjwa ya moyo.

Faida nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya folic acid, phytosterols, phytic acid’ (inositol hexaphosphate) na resveratrol’ vinavyopatikana kwenye karanga, huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.

Zaidi utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa karanga hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia 27 kwa wanaume. Kwa maelezo hayo kuhusu faida za karanga mwilini bila shaka chakula hiki kinapaswa kupewa kipaumbele katika orodha ya vyakula tunavyokula.

kila siku na hakika Mungu ametupenda sana kwakutupa kinga dhidi ya maradhi yote yanayotukabilikwa njia ya vyakula.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha k... Read More

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho n... Read More
Faida za kunywa juisi ya ubuyu

Faida za kunywa juisi ya ubuyu

Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni ... Read More

Tabia 10 zinazoweza kuharibu figo

Tabia 10 zinazoweza kuharibu figo

1.Kubana mkojo kwa muda mrefu
2.Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
3.Kutumia chumvi n... Read More

Sababu, dalili na matibabu ya tatizo la kuziba kwa mrija wa mkojo

Sababu, dalili na matibabu ya tatizo la kuziba kwa mrija wa mkojo

Mrija wa mkojo (urethra) ni kiungo muhimu kinachotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu. Mri... Read More

Tikiti maji kama dawa ya kutibu nguvu za kiume

Tikiti maji kama dawa ya kutibu nguvu za kiume

Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ā€˜Potassium’, ā€˜Magnesium’ na virutubis... Read More

PROSTATE GLAND (TEZI DUME) TATIZO SUGU KWA WANAUME

PROSTATE GLAND (TEZI DUME) TATIZO SUGU KWA WANAUME

-Hii ni tezi ya wanaume yenye sifa zifuatazo.
~Ina umbo km yai(oval shape)
~Ina ukubwa ... Read More

Sababu ya meno kubadilika rangi

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao y... Read More

Suluhisho rahisi la nguvu za kiume hili hapa

Suluhisho rahisi la nguvu za kiume hili hapa

NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya n... Read More

Visababishi, dalili, matibabu na kinga ya presha ya kushuka

Visababishi, dalili, matibabu na kinga ya presha ya kushuka

Hypotension ndio jina linalotumika kuelezea presha ya kushuka ambayo mpaka sasa chanzo chake hakijaw... Read More
Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu w... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek)

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek)

Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mba... Read More