Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Featured Image
Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

Zifutazo ndizo dalili za upungufu wa maji mwilini;


Dalili za upungufu wa maji kwa mtoto.


Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:



  1. Kukojoa mara chache sana

  2. Mdomo na ulimi kukauka

  3. Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.

  4. Mtoto kutokuwa mchangamfu

  5. Macho, tumbo au mashavu kubonyea


Dalili za upungufu wa maji kwa wazee.


Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.
Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Dalili za upungufu wa maji kwa wajazito.


Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:

  1. Kukojoa mkojo wa njano nyeusi

  2. Kuumwa na kichwa.

  3. Mwili kukosa nguvu.

  4. Kichefuchefu na kutapika.

  5. Kukaukwa na mdomo.


Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution) . Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu?

Hivyo wito wetu kwako kuendelea kunywa maji mengi ya kutosha kadri uwezavyo hii itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwa na afya bora
AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu

Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu

Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chem... Read More
Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum , ambaye pia huitwa spirochetes kutokan... Read More
Dondoo muhimu za afya

Dondoo muhimu za afya

Tafadhali soma na uwapelekee wengine.

Dr. Chriss Mosby wa Tanzania amegundua kensa mpya kwa... Read More

Faida za kutumia maji ya uvuguvugu na asali

Faida za kutumia maji ya uvuguvugu na asali

Ili uweze kuwa na siku nzuri basi unashauriwa kuanza siku yako kwa kutumia mchanganyiko wa maji y... Read More

Faida za mnyonyo na mazao yake

Faida za mnyonyo na mazao yake

Nyonyo Mbarika (Castor)
Mnyony(KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka(KiRusi) ni mmea wa jamii ... Read More

Mambo usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa Pumu

Mambo usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa Pumu

Asthma /pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu... Read More
Faida 13 za kunywa juisi ya miwa

Faida 13 za kunywa juisi ya miwa

Unapopita maeneo mengi ya mijini na pembezoni wa miji utakutana na wafanyabiashara wa miwa wanaou... Read More

Faida za kula Tende kiafya

Faida za kula Tende kiafya

Zifutazo ni faida zitokanazo na ulaji wa tende; 1. Tende huongeza nguvu kutokana na kuwa na sukari ... Read More
Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito

Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito

Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzi... Read More

Njia bora za kumfanya mtu aache kuvuta sigara

Njia bora za kumfanya mtu aache kuvuta sigara

Ni kazi ngumu kidogo kuacha uvutaji wa sigara. Uvutaji ni tishio kwa maisha yetu. Yawezekana hufa... Read More

Matumizi ya mbaazi kama dawa

Matumizi ya mbaazi kama dawa

Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza k... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia aloe vera

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia aloe vera

Mshubiri au Aloe Vera kama ilivyozoeleka na namna nzuri kwa wale wote wanaotaka kubaki na ngozi ... Read More