Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Vichekesho vya kukuondoa mawazo leo

Featured Image

Soma vichekesho hivi;

Mwizi wa atm

Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu "sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.

Cheka kidogo

Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.

Mlizi mbio mbio

Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.

13, 13…

Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,….. akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14……

WATAALAM

Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa?
Jamaa: Sijafa bwana
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.

Ya leo mgonjwa

Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening'inizwa mikono juu akauliza "dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?"
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.

4WD

Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza "si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?" Mume akajibu "unadhani wapi ntapata rav4 feki?"

Ajali ilivyotokea

Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali "ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika." Dereva akajibu "hata sikumbuki nlifumba macho"

Faini ya kukojoa

Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa?
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
Polisi: Faini yake elfu tano.
Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
Polisi: Basi kojoa tena…

Mume anaenda kazini

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini…

Hasira za mtoto

Baba na mtoto:
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
Mtoto: Naenda chooni.
Baba: Chooni? Kufanya nini?
Mtoto: Kusafisha.
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.

Mgonjwa na Dokta

Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua.
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.

Pilau la bachela

Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.

Mwizi na chizi

Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.

Chemsha bongo

Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea "haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?" Mtoto akajibu "hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner"

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Hamida (Guest) on June 28, 2015

Haha, hii ni ya kuhifadhi! πŸ“Œ

Jane Muthui (Guest) on June 12, 2015

πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜†

Mary Njeri (Guest) on June 4, 2015

Nimecheka hadi nimesahau shida zangu! πŸ˜…πŸ˜Š

Lydia Mzindakaya (Guest) on June 2, 2015

πŸ˜‚ Nitaiiba hii bila shaka!

Henry Sokoine (Guest) on May 23, 2015

πŸ˜‚πŸ˜‚

Hellen Nduta (Guest) on May 9, 2015

😁 Hii ni dhahabu!

Rose Kiwanga (Guest) on April 28, 2015

Hii imenifurahisha hadi ninacheka kwa sauti! πŸ˜„πŸ˜…

George Mallya (Guest) on April 27, 2015

Hii imenibamba sana! πŸ˜…πŸ€£

Rabia (Guest) on April 4, 2015

πŸ˜… Nilihitaji kicheko hicho!

Related Posts

Wavuta bangi wa Colombia watoa mpya

Wavuta bangi wa Colombia watoa mpya

Asubuhi ya leo huko nchini Colombia baada ya serikali kuidhinisha matumizi ya bangi kuwa halali ... Read More

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi

_
1. Mi... Read More

Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba

Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba

Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana

..unaenda kuoga, unakumbuka k... Read More

Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake

Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake

Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl aka... Read More

Wadada lenu hili. Mimi sipo

Wadada lenu hili. Mimi sipo

Wadada kama una sura mbaya subiri NEEMA YA BWANA..Sio kutuambia mna uzuri wa Ndani usioonekana..... Read More

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji... Read More

KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri

KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri

Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe,... Read More

Haya nayo ni maajabu mengine kwa wazazi wa mabinti

Haya nayo ni maajabu mengine kwa wazazi wa mabinti

BABA MWEUSI
MAMA MWEUSI

na ww walikuzaa mweusi lakini umefikisha miaka 20 umeanza kua ... Read More

Faida 3 za uvutaji wa sigara

Faida 3 za uvutaji wa sigara

Ni hizi

1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara ny... Read More

Hapo sasa akili itakuja

Hapo sasa akili itakuja

Pale unapo gundua kuwa yule ulie mtukana kwenye bajaji ndio boss anaeenda kukufanyia inte... Read More

Tofauti kati ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo mwanamme anapotoka kuoga

Tofauti kati ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo mwanamme anapotoka kuoga

Tofauti ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo pale ambapo Mwanaume wake atokapo kuoga.

Bi... Read More

Huyu mme ni shida

Huyu mme ni shida

MKE..mume wangu unaweza kuua simba kwasababu yangu???

MME: Hapana mke wangu, sema kingineRead More