Updated at: 2024-05-25 16:53:01 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
πππππππππππ
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii β¦β¦β¦mnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
Updated at: 2024-05-25 17:57:23 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO.
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Updated at: 2024-05-25 18:05:58 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!
Updated at: 2024-05-25 17:10:00 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jana wakati naangalia taarifa ya habar mtangazaji akasema "mpenz mtazamaji nataka nikupeleke moja kwa moja had marekani" nikazima TV kwa haraka nikaenda kuvaa viatu. Hadi sahv bado nmekaa hapa seblen nahisi bado wanaihangaikia Visa yangu
Updated at: 2024-05-25 16:54:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuoa vijijini raha sana Hata ukiulizwa unafanya kazi gani ukiwaambia mimi ni admin basi daaaah wanaona wewe ni bonge la bossππππππππππππππππππππ
Updated at: 2024-05-25 18:10:22 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mdaku alishangaa kila siku mchungaji anaingia nyumba ya jirani yake ambaye hana mume, akawa anajiuliza anakwenda kufanya nini? Uzalendo ukamshinda akamuuliza "Mwenzangu, mbona kila siku mchungaji anakuja kwako, vipi anakuja kukuombea?" Akajibiwa "Nyoo, umbea tu! Mbona kwako kila siku anakuja mwanajeshi kuna vita! chefuuuu π³π³π³π³π³
Updated at: 2024-05-25 17:04:59 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimefika hapa Polisi Station nimefarijika sana na Kustuka baada ya kumkuta Askari hapa Kaunta anasoma Biblia nikajisikia fahari kuona anasoma neno kituo cha Polisi. Nikamuukiza Afande ni Nani alimuua Goliathi? Akasema Muulize Afande Mwita mlango namba 2 ndo anausika na Kesi za Mauaji.ππ