Wachaga wana mambo mbele ya hela, angalia hii bili ilivyomchanganya MASSAWE
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000
Kitime 15,000
Updated at: 2023-04-29 22:52:15 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo: Manka 35,000 Marieta 20,000 Kekuu 30,000
Kitime 15,000 Kinabo 10,000 TOTAL 110,000/= MASSAWE akaicheki akasema "Wote nitawalipia lakini huyo "TOTAL" Yesuu simlipii. Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyewe…
Updated at: 2024-05-25 17:10:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tulikua kwa basi tunaelekea arusha,ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari, nikaenda kumziba macho nkamuuliza otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana NA SASA HIVI NIMEZINDUKA NIMEONA ABIRIA WOTE TUPO WODI NAMBA 3 HAPA KCMC MOSHI. 🤕🤕🤕🤕 SODA ZA WAGONJWA PLIIIZ!!! 🙏🙏🙏🙏🙏
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Updated at: 2024-05-25 18:00:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI” Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”! Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”! Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”! Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”! Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”! Simu ya 7 – “Me too”! Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Updated at: 2024-05-25 17:55:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku? Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni? Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbele😂😂😂😂😂
Ujanja alioutumia msichana wa kazi ili apandishiwe mshahara na mama mwenye nyumba
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshahara….. Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Updated at: 2023-04-29 22:52:53 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Msichana wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshahara….. Mama mwenye nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa mshahara.
Msichana: Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia? Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili? Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mume wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni Shamba boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatu…….