Updated at: 2024-05-25 17:56:17 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
USIJIONE MJUAJI SAAAA…NA. Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika nyumbani.
kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao. Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi, akawaambia "hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani" mama"hee embu tuoneshe mwanangu" jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu "ngapi?" wazazi"moja" akainua wa pili "ngapi?" wazazi "mbili" akawarudisha akisema"wazee wangu nadhani japo shule hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu mezani" baba"mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA"
Updated at: 2024-05-25 16:52:33 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ulishawahi kutana na hii…. Issa: mambo Jeni:poa vp Issa:poa nambie:
Jeni:poa aje ww: Issa:poa nambie Jeni:poa Issa :bas poa Jeni:poa…. Issa:poa badee basi Jeni:haya Issa:bai 😂😂😂😂……..HII KIITALIANO INAITWA LACK OF SOUND ENGINEERING NA HII INASABABISHWA NA UOGA……
Updated at: 2024-05-25 16:53:49 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndoto zingine bwana usiombe zikupate
Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.
Updated at: 2024-05-25 16:57:53 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi
_ 1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniua… It's Over!!! _ 2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It's over! _ 3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. It’s over!! _
4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It's over! _ 5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, It’s over! _ 6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.
Updated at: 2024-05-25 17:05:58 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
SIFA MBAYA… Jamaa alikuwa ndani ya daladala Mara simu ikaita alikuwa ni mkewe kwa sifa jamaa akaweka loud speaker ili watu wasikie wanavyopendana. JAMAA;wife Mara hii umenimiss jaman WIFE; kwa nini umekunywa uji wa mtoto?!!! 😂😂😂😂😂