Mahusiano: Mapenzi ya Mbali

Jinsi ya kumjua mwanamke ambaye hajatulia a.k.a kicheche

Kumjua mwanamke ambaye hajatulia unaangalia mambo haya yafuatayo

Siyo rahisi kupenda

Dalili ya kwanza ya mwanamke kicheche mi kwamba huwa huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano na mambo ya kupendana, wanataka siku zote wawe huru hata mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye. Utasikia akisema tuwe Marafiki tuu.

 

Anachukulia mahusiano kama njia ya kujinufaisha

Wanawake vicheche huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako. Yupo tayari kufanya chochote hata kama kinamgarimu ilimradi apate kile anachokitaka.

Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo na kwa mtu yoyote

Kwa kawaida mwanamke kicheche, pale tu utapomfurahisha na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka. Na hii hutokea kwa kila mwanaume anayemkuta ambaye anaweza kumpa kile anachotaka basi atamfanyia chochote huyo mwanaume anachotaka.

 

Anamarafiki wakiume kwa manufaa

Mwanamke kicheche huwa na Marafiki wengi wa kiume kila mmoja kwa ajili ya faida. Mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo tatizo, ila tatizo linakuja pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume ambao kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale. Unakuta Marafiki hao wote kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo ni kicheche.

 

Ni rahisi kuvunja mahusiano usipompa anachotaka

Mwanamke kicheche anakasirika haraka usipompa kile anachokitaka. Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe wiki nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake. Ukishindwa kabisa kumpa anachokitaka basi anavunja uhusiano na wewe na kutafuta mtu mwingine anayeweza kumpa anachokitaka.

Unaweza kuwafahamu wanawake zaidi kupitia Kitabu hiki cha SIRI ZA WANAWAKE. Unaweza kudownload kitabu hiki moja kwa moja hapa

Read and Write Comments

Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako “Romantic”. Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe.

💞
Wanawake wa siku hizi wengi, kwa mfano umemtoa out kidogo mkapate walau msosi sehemu nzuri, mkianza kula mpaka mnamaliza hakumbuki hata kukulisha kidogo kimahaba. Unakuta anakula msosi kimpango wake utafikiri anakula na kaka yake. Mnatoka kidogo mnatembea unakuta anatembea na wewe utafikiri anatembea na kaka yake; yani unaweza ukamuacha nyuma kidogo au akawa mbele yako anashindwa kujiongeza kupitisha mkono wake kwenye kikwapa chako na kukushika kimahaba.
💞
Wakati mwingine anakuona jasho linakutoka usoni anashindwa hata kukufuta kimahaba anakutazama tu utafikiri wewe ni kinyago cha mpapure. Wakati anakuaga anaondoka utafikiri anamuaga kaka yake hakupigi hata busu. Mwanamke unazungumza nae hakushiki hata ndevu zako kimahaba, mwanamke unakuwa nae hakufunyii massage wala hakukati mara moja moja kucha zako kimahaba.
💞
Wakati mwingine unakuta umekaa nae mwaka mzima kwenye mahusiano lakini hajawahi kukwambia neno “Nakupenda”mpaka wewe uanze kumwambia kwanza.
💞
Wanawake wengi wa siku hizi wanapenda kudekezwa, kubembelezwa na kupewa pesa ndio maana wengi utasikia wakisema “nataka mwanaume Romantic na mwenye pesa” lakini hawajiulizi je, wao ni Romantic? Au sisi wanaume hatuhitaji hayo mahaba ya wanawake?
💞
Asili ya mwanamke ni mfariji mkuu wa mwanaume lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa stress kwa wanaume.
💞
Note: Hakuna mwanaume mbahili kwa mwanamke Romantic.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Read and Write Comments

Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana

1. Kama uko shule au chuo soma na usicheze ukifeli unajipotezea muda. Soma sana utafanikiwa…

2. Jifunze kuweka akiba ya pesa. Pia jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa,bajeti vizuri na jiwekee akiba bank au popte unapoona panafaa.

3. Jitengenezee good character yaani tabia yako njema ili uwe tofauti na wengine.. Jitofautishe na wengine, uwe mfano bora

4. Jifunze kufanya kazi tofauti tofauti. Fanya hiki ama kile ili angalau uweze kuishi popote kwani dunia inabadilikaa na huwezi jua kesho yako

5. Anza kununua na kumiliki vitu kama kitanda godoro vyombo na ardhi au kiwanja. Kumbuka msingi mzuri wa maisha ni fikra za ujana na kujiwekea mali

6. Kama utaweza kapange ujifunze maisha. Anza kujitegemea ili kujipa confidenece na maisha.

7. Weka falsafa yako katika maisha na uiishi. Falsafa ni dira ya kukuongoza. Mfano unataka kumiliki nini katika maisha? Unataka mke au mume wa aina gani? Aina gani ya maisha unaipenda? Hiyo ndiyo falsafa…

8. Tengeneza mahusiano yaliyotulia na weka malengo. (Kwa wale wa ndoa) Jichagulie kijana au binti aliyemzuri katika wengi, kijana au binti wa moyo wako, mpende… Kipindi hiki ni cha kuwa na mwenza aliyetulia kama unafikiri kuoa au kuolewa. Ukicheza ukafikisha 30 bila kuwa na mtu maaalumu basi utaoa au kuolewa bora mradi ila siyo na mtu wa ndoto yako..

9. Kuwa na marafiki imara, jichagulie katika wengi marafiki kadhaa waliotulia wenye nidhamu ya maisha na wanaopenda uende mbele. Kijana chunga marafiki ulionao wengi leo wanajuta kwaa urafiki m’baya uliowapoteza… a

10. Kumbuka ibada na kumshukuru Mungu. Kipindi hiki ni cha misukosuko na mihemko mingi. Usiache mafundisho ya imani yako, usimsahau Mungu. Mshukuru Mungu kwa uhai na kila jema au baya likupatalo.

11. Jitume katika kazi, watu waliofanikiwa wanajua thamani ya juhudi na kujituma. Usikate tamaa hata kama unapata kidogo. Fanya kazi kama vile kesho haipo. Matunda utayaona

12. Zingatia kujiweka safi. Kuwa msafi na mtanashati huanza na ubongo, muonekano wako ndivyo watu watakavyo kuchukulia. Jiweke safi na jitunze..

13. Kula kwa afya, wengi wanachukia miili yao. Wanauchukia aidha unene au wembamba, ila ukila kwa afya, ukafanya mazoezi unatengeneza afya bora ya sasa na baaadae..

14. Vaa kwa heshima, usivae kama mcheza disko au teja. Kumbuka thamani yako kwa Mungu. Kwanini uvae nguo za machukizo mbele yake! Kwanini ukubali kuwa wakala na kutumiwa na shetani kuwaaangamiza wengine kwa kuvaa ovyo? Vaa kwa heshima..

15. Pendelea kusafiri maeneo tofauti na ujifunze! Asafiriye hupata maarifa na hujifunza mengi. Penda kusafiri, tembelea maeneo tofauti utakuwa na mengi ya kujifunza.

16. Kumbuka kupumzisha mwili. Kuishi kwetu kupo katika chembe ya uhai iliyopo mwilini. Upe mwili na ubongo chakula chake cha kupumzika. Nenda maeneo yatakayofanya mwili na akili vipumzike angalau kila baada ya miezi kadhaa..

17. Jifunze kuamua mwenyewe. Usisubiri kila kitu kumshirikisha mtu ndio uamue. Jifunze kuwa mwamuzi wa mambo yako mwenyewe haijalishi kwa gharama ipi. Watu wawe washauri ila ubaki kuwa mwamuzi mwenyewe.

18. Kuwa mtu wa kutunza siri. Jitahidi kuwa na shingo nzito na akili yenye kuweka siri. Usiwe mtu wa kusema kila uonacho au uambiwacho.

19. Jfunze na zitawale hisia zako. Hisia ziwe za hasira, mapenzi au ugomovi zitawale na utaishi miaka mingi. Asiye tawala hisia zake hata awe mkubwa bado ni mdogo…

20. Jitolee kwaajili ya wengine, fundisha kemea saidia. Unaweza kufundisha kupitia facebook wasap nk. Kemea ukiona mtu anafanya kitu kibaya, saidia wenye shida wakumbuke wagonjwa yatima wazee na wenye mahitaji. Wewe ni yatima, mzee, au muhitaji wa kesho.. Weka akiba ya wema

21 Jenga mazingira ya kuishi na watu vizuri. Usijione mzuri au HB sana ukadharau wengine. Ishi na kila mtu kwa upendo hata kama wanakuchukia..

22. Tunza muda, muda ni mali huwezi kuurudisha, kuusimamisha au kuuzuia. Ukishapotea ndio basi tena. Tambua thamani ya muda na fanya vitu kwa wakati..

23. Pendelea kusoma hasa vitabu vya dini, kuhusu mali, elimu, mchumba, afya, maisha, uongozi, hekima, busara, utu, uchaji, utii, maarifa, utajiri, heshima, uvumilivu, matumaini, upendo, na kila kitu vimo katika Biblia na Qur’an ..soma uchote hekimaa…

24. Acha kujifunza matumizi ya pombe, sigara , dawa za kulevya. Kama unatumia jitahidi uache, kama unajifunza acha na kama kuna mtu anakushawishi kataa. Afya ni mali na mtaji usichoshe na kuumiza uhai wako kwa pombe sigara na madawa ya kulevya…

Inafaa ukishare kwa wengine wajifunze maarifa haya..
*Maisha ni maamuzi yako wewe*
Kuamua kufanikiwa au kushindwa,
kuamua utajiri au umasikini yote ni mipango na hutokana na fikra zako..

Read and Write Comments

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
Read and Write Comments
Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    🏠 Home 🔒 Login 📝 Register 💡 Tools