KAMA UMEOA SOMA HII: Jinsi ya Kuishi na Mke wako

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

Kupewa nafasi na kipaumbele.

Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.

 

Kuheshimiwa

Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.

Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa

Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.

 

Nafasi ya kuongea na kujieleza

Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.

 

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao

Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

Kubembelezwa

Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.

Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE

Jinsi ya kuamsha mahaba na mapenzi katika mahusiano

Hizi hapa njia za kuamsha na kudumisha uhusiano mzuri kati yako na mpenzi wako hasa baada ya kuwa mmeshazoeana sana na kuhisi kuchokana.

Dumisha faragha katika mahusiano yenu

Hakikisha kunakua na faragha katika mahusiano yako na mpenzi wako. Vile vile itahakikisha kuwa wewe na mpenzi wako mnakuwa na wakati wa kutosha kustarehe bila wasiwasi. Usiruhusu siri zako na mwanamke zitoke nje kati yenu.

 

Tenga muda wa kustarehe pamoja

Ili kudumisha mahusiano na mwanamke lazima kuwepo na mda wa kuwa pamoja na kufanya mambo yenu mnayoyataka kwa kuridhika bila kupungukiwa na muda. Kwa mfano ni muhimu kupumzika mapema kitandani ili kuhakikisha mnakuwa na wasaa wa kutosha wa kufanya mapenzi.

Ongeeni pamoja kwa uhuru kuhusu suala la tendo la ndoa

Ni muhimu kujadili na kukubaliana na mwanamke kuhusu swala la kufanya mapenzi. Ni vyema muongee kuhusu suala la mapenzi na jinsi ya kuwasha moto wa mapenzi baada ya kuchokana. Mwanamke anatakiwa apewe uhuru wa kusema kile anachokihitaji.

 

Pangeni miadi ya usiku

Mwanamke huridhika zaidi katika mapenzi kwa kuandaliwa ipasavyo hii ikiwa ni pamoja na kuwa na utayari wa kufanya mapenzi. Hivyo ni vyema kupanga miadi ya usiku ili mwanamke awe tayari na ili kumridhisha mwanamke.

Badilisha mazingira

Njia nyingine ya kuamsha mapenzi ni kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi. Kwa mfano mnaweza kuacha kitanda chenu cha nyumbani na kulala katika chumba cha hoteli iwapo uamuzi huo utaboresha mapenzi kati yenu.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Mchumba anayefaa kufunga naye ndoa

Maisha ya ndoa yanahitaji maandalizi mazuri, kama waswahili wasemavyo nyote njema huonekana asubuhi, asubuhi ya maisha ya ndoa ni kipindi cha uchumba. Ndugu zangu, kipindi cha uchumba ni lazima tukitumie vizuri na kwa makini na kila jambo, ukitambua hakuna jambo dogo wa kubwa, kila jambo uliangalie katika mapana yake na katika uzito wake.

Hivyo basi huyo anayetaka kuwa na wewe jiulize maswali haya juu yake;

1. Je anamtambua Mungu na kuishi maisa ya kumpendeza Mungu, katika matendo yake na maneno yake?
2. Je huyo mchumba wako yupo tayari kukusaidia wewe kufikia malengo yako katika maisha?
3. Je huyo mchumba wako anakuheshimu na kukusikiliza au mtu anayekudharau?
4. Je mchumba wako anakushirikisha kila jambo kuhusu maisha yake na pia kuwa na utayari wa kupokea mawazo yako?
5. Je mchumba wako ana mawasiliano na wewe kwa kiasi kikubwa na kukujulia hali mara kwa mara?
6. Je mchumba wako yupo tayari kujitoa kwa ajili yako kwa hali na mali ili kufikia malengo yenu ya pamoja?
7. Je unatambua mazuri na mapungufu ya mchumba wako, hasa tukitambua hakuna mtu ambaye ni mkamilifu na namna gani mnasaidiana katika madhaifu yenu
8. Je mchumba wako ni msikivu au ni mtu ambaye anapoamua jambo ndilo analotaka hawezi kukusikiliza wala kupokea mapendekezo yako?
9. Je mchumba wako ni mwaminifu na anajitunza kwa ajili yako wewe tu au ni mtu ambaye haeleweki heleweki?
10. Je mchumba wako yupo tayari kukusamehe unapomkosea au kuomba msamaha anapokosea, au ni mtu mbishi
Haya ni mambo machache ambayo ni lazima kuyatafakari kuhu mchumba wako kama anakufaa kuunga naye NDOA? Usikurupuke.

Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana

1. Kama uko shule au chuo soma na usicheze ukifeli unajipotezea muda. Soma sana utafanikiwa…

2. Jifunze kuweka akiba ya pesa. Pia jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa,bajeti vizuri na jiwekee akiba bank au popte unapoona panafaa.

3. Jitengenezee good character yaani tabia yako njema ili uwe tofauti na wengine.. Jitofautishe na wengine, uwe mfano bora

4. Jifunze kufanya kazi tofauti tofauti. Fanya hiki ama kile ili angalau uweze kuishi popote kwani dunia inabadilikaa na huwezi jua kesho yako

5. Anza kununua na kumiliki vitu kama kitanda godoro vyombo na ardhi au kiwanja. Kumbuka msingi mzuri wa maisha ni fikra za ujana na kujiwekea mali

6. Kama utaweza kapange ujifunze maisha. Anza kujitegemea ili kujipa confidenece na maisha.

7. Weka falsafa yako katika maisha na uiishi. Falsafa ni dira ya kukuongoza. Mfano unataka kumiliki nini katika maisha? Unataka mke au mume wa aina gani? Aina gani ya maisha unaipenda? Hiyo ndiyo falsafa…

8. Tengeneza mahusiano yaliyotulia na weka malengo. (Kwa wale wa ndoa) Jichagulie kijana au binti aliyemzuri katika wengi, kijana au binti wa moyo wako, mpende… Kipindi hiki ni cha kuwa na mwenza aliyetulia kama unafikiri kuoa au kuolewa. Ukicheza ukafikisha 30 bila kuwa na mtu maaalumu basi utaoa au kuolewa bora mradi ila siyo na mtu wa ndoto yako..

9. Kuwa na marafiki imara, jichagulie katika wengi marafiki kadhaa waliotulia wenye nidhamu ya maisha na wanaopenda uende mbele. Kijana chunga marafiki ulionao wengi leo wanajuta kwaa urafiki m’baya uliowapoteza… a

10. Kumbuka ibada na kumshukuru Mungu. Kipindi hiki ni cha misukosuko na mihemko mingi. Usiache mafundisho ya imani yako, usimsahau Mungu. Mshukuru Mungu kwa uhai na kila jema au baya likupatalo.

11. Jitume katika kazi, watu waliofanikiwa wanajua thamani ya juhudi na kujituma. Usikate tamaa hata kama unapata kidogo. Fanya kazi kama vile kesho haipo. Matunda utayaona

12. Zingatia kujiweka safi. Kuwa msafi na mtanashati huanza na ubongo, muonekano wako ndivyo watu watakavyo kuchukulia. Jiweke safi na jitunze..

13. Kula kwa afya, wengi wanachukia miili yao. Wanauchukia aidha unene au wembamba, ila ukila kwa afya, ukafanya mazoezi unatengeneza afya bora ya sasa na baaadae..

14. Vaa kwa heshima, usivae kama mcheza disko au teja. Kumbuka thamani yako kwa Mungu. Kwanini uvae nguo za machukizo mbele yake! Kwanini ukubali kuwa wakala na kutumiwa na shetani kuwaaangamiza wengine kwa kuvaa ovyo? Vaa kwa heshima..

15. Pendelea kusafiri maeneo tofauti na ujifunze! Asafiriye hupata maarifa na hujifunza mengi. Penda kusafiri, tembelea maeneo tofauti utakuwa na mengi ya kujifunza.

16. Kumbuka kupumzisha mwili. Kuishi kwetu kupo katika chembe ya uhai iliyopo mwilini. Upe mwili na ubongo chakula chake cha kupumzika. Nenda maeneo yatakayofanya mwili na akili vipumzike angalau kila baada ya miezi kadhaa..

17. Jifunze kuamua mwenyewe. Usisubiri kila kitu kumshirikisha mtu ndio uamue. Jifunze kuwa mwamuzi wa mambo yako mwenyewe haijalishi kwa gharama ipi. Watu wawe washauri ila ubaki kuwa mwamuzi mwenyewe.

18. Kuwa mtu wa kutunza siri. Jitahidi kuwa na shingo nzito na akili yenye kuweka siri. Usiwe mtu wa kusema kila uonacho au uambiwacho.

19. Jfunze na zitawale hisia zako. Hisia ziwe za hasira, mapenzi au ugomovi zitawale na utaishi miaka mingi. Asiye tawala hisia zake hata awe mkubwa bado ni mdogo…

20. Jitolee kwaajili ya wengine, fundisha kemea saidia. Unaweza kufundisha kupitia facebook wasap nk. Kemea ukiona mtu anafanya kitu kibaya, saidia wenye shida wakumbuke wagonjwa yatima wazee na wenye mahitaji. Wewe ni yatima, mzee, au muhitaji wa kesho.. Weka akiba ya wema

21 Jenga mazingira ya kuishi na watu vizuri. Usijione mzuri au HB sana ukadharau wengine. Ishi na kila mtu kwa upendo hata kama wanakuchukia..

22. Tunza muda, muda ni mali huwezi kuurudisha, kuusimamisha au kuuzuia. Ukishapotea ndio basi tena. Tambua thamani ya muda na fanya vitu kwa wakati..

23. Pendelea kusoma hasa vitabu vya dini, kuhusu mali, elimu, mchumba, afya, maisha, uongozi, hekima, busara, utu, uchaji, utii, maarifa, utajiri, heshima, uvumilivu, matumaini, upendo, na kila kitu vimo katika Biblia na Qur’an ..soma uchote hekimaa…

24. Acha kujifunza matumizi ya pombe, sigara , dawa za kulevya. Kama unatumia jitahidi uache, kama unajifunza acha na kama kuna mtu anakushawishi kataa. Afya ni mali na mtaji usichoshe na kuumiza uhai wako kwa pombe sigara na madawa ya kulevya…

Inafaa ukishare kwa wengine wajifunze maarifa haya..
*Maisha ni maamuzi yako wewe*
Kuamua kufanikiwa au kushindwa,
kuamua utajiri au umasikini yote ni mipango na hutokana na fikra zako..

Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

1. Ukija kijiweni au pub au kwenye nyama choma acha zile stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, sijui una madigirii mangapi. Piga stori nyingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa.

2. Tembea na keshi mfukoni kama vipi, stori za kadi yangu ya benki imegoma sio ishu.

3. Punguza mambo yako ya kuvaa sana kipapaa. Sometimes ibuka na pensi na jinsi tu mwana.

4. Punguza kukesha nje mfululizo, iwe umeoa, una mpenzi au upo upo. Kikanuni kabisa usikae nje hadi usiku wa manane siku tatu mfululizo labda uwepo mchongo wa maana sana. I mean wa maana sana.

5. Epuka sana mchezo wa kujipiga tattoos. Kuna watu wamekosa wake au michongo hevi in life kisa hizo mambo.

6. Nasisitiza sana epuka kumtaka mpenzi wa zamani wa mshikaji wako. Pigia mstari hii pointi. Kwani lazima upite palepale? Tusiishi kikondoo bro.

7. Jiunge walau na mtandao mmoja wa kijamii. Keep in touch na washikaji. Kuna wana toka mmemaliza primary hamjachekiana, utawakuta mitandaoni. Unaweza kupata mchongo au kujifunza ishu mbili tatu, au kuwa fala zaidi ukiamua.

8. Maisha mafupi sana, jitahidi kupunguza kukunja ndita. Jiachie mara moja moja.

9. Ukifika baa uwe tayari unajua unakunywa nini. Sio Mhudumu anakuja kukusikiliza unawaaaaaza. Inaonyesha hujisomi na huna mipango. Samahani lakini.

10. Kama hujaalikwa kwenye ishu, usiende mwanangu. Sometimes hata ukialikwa usiende pia. Unaweza kualikwa ili useme no, kiushahidi tu.

11. Halafu tumechoka wewe kuwa kituko ukilewa. Kama pombe huziwezi ziache, piga juisi tu au maji wakati wana tunapiga monde, sio kesi, ni uwezo tu wa kuhimili.

12. Toa tip bila kuomba namba ya baamedi basi mwanangu. Jifanye kama umetoa tu msaada. Hata simba sio swala wote huwa anawala porini, wengine anawacheki anapita zake.

13. Punguza kutumia simu sana, tena wakati mwingine kwa ishu ambazo hazina mpango.
Ukumbuke juzi juzi hapa wataalamu wamesema simu zinaleta ugumba.

14. Nunua tumiwani twa jua twa bei bei hivi, inakupa mwonekano wa kijentlomani sometimes.

15. Piga push-ups walau 50, sit ups na dips kabla ya kuoga asubuhi, hii afya tumeazimwa tu, jiweke fit.

16. Toka out na washikaji zako at least mara moja kwa mwezi mpige msosi na kinywaji. Wife au demu wako na wanao waache home! Sio kila kona kila siku uko nao kama mkoba, kichwa kitatia kutu.

17. Julikana walau hata baa mbili tatu au sehemu mbili tatu. Baa, basketball ground, soccer ground, acha kujikunyata home. Wewe mtoto wa kiume man.

18. Jifanye mjuaji sometimes, then jifunze baadaye. Sio kila kitu wewe ni “I don’t know”.

19. Beer moja au glass moja ya wine baada ya mlo haiwezi kukuvurga, kama hutaki, kunywa majuisi yako basi ulete inzi, au misoda ujijazie magonjwa.

20. MTOTO WA KIUME HAPIGI SELFIE OVYO OVYO NA KUBINUA MIDOMO na KULAMBA LIPSI. PIGA SELFIE KWENYE ISHU MUHIMU. FAMILIA HIVI, DEMU MKALI, etc. Umenisoma?

21. Ukiweza miliki hata panga ghetto, maana bastola najua ngumu. Sio nyumba nzima huna hata kasilaha kadogo.

22. Ridhika. Hamna hata siku moja utakuwa na kila kitu. Jifunze kushukuru kwa ulicho nacho.

23. Sometimes agiza matunda badala ya chipsi.

24. Ukikutana na demu mzuri kiwanja yuko peke yake, muongeleshe.

25. Miliki walau suti moja kabla hujapitisha miaka 30 bro. Please. Na tupafyumu.

26. Kuwa na mpenzi moja
kwa wakati mmoja. Anatosha sana. Trust me.

27. Ukitaka kujilinganisha, jilinganishe wewe wa jana na wewe wa leo. Utafika mbali. Ukijilinganisha na wana utapasuka kichwa.

28. Piga picha nyingi kwa camera (again, sio selfies) tunza kumbukumbu.

29. Ukialikwa kwenye party usiende mikono mitupu. Nenda walau na kachupa kamoja ka mvinyo.

30. Date demu nje ya wale unaokutana nao club au baa mara wa mara. Utakuja kuniambia faida zake.

31. Huwezi kuwa mpenzi wa pombe au sigara kwa sababu hivyo vitu havitakaa vikupende.

32. Hata siku moja usirudiane na demu aliyekuacha kisa huna mkwanja. Kaenda kutafuta kakosa ndio maana kakurudia labda baada ya kuona umepata. Siku akikutana na mwenye chambi kukuzidi? Jibu kaa nalo.

33. Sometimes jitoe out mwenyewe, kaa mahali piga msosi wako na kinywaji chako, tafakari ishu zako. Alone.

34. Jisomee ukiwa na time. Inakupa chance kuazima ubongo wa mtu mwingine lakini pia inakupa matirio kwenye maongezi, ila stori za kuja kwenye joint na washikaji na kuanza kusema oh nimesoma kitabu hiki na kile kausha!

35. Puuza wanaozomea. Huwa wamekaa viti vile vya bei rahisi.

36. Hata siku moja usiseme “Ndo hivyo bwana, hamna namna tena”. Ipo namna bro.

37. Usi-bet kama ukipoteza buku 5 we ni mtu wa kulia lia kindezi.

38. Muombe na Mshukuru Mungu wako. Kama huna Mungu jishukuru mwenyewe, kiazi wewe.

39. Kumbuka, sheria hufuatwa na wajinga lakini huwaongoza wenye busara.

Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
Shopping Cart