Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

Featured Image

Sikiliza, hakuna haja ya kuketi chini ili kuelewa ujumbe huu: Ukweli unabaki kwamba wengi wanajihusisha kupita kiasi na yale yasiyo ya msingi katika safari yao ya mafanikio. Kuna msemo wa kiingereza unaosema "mind your own business," tunapaswa kujiuliza tufanyeje na ushauri huu. Fikiria, unaifuatilia maisha ya Ali Kiba kwa kina kiasi kwamba unajua hata mambo ya faragha kama vile bafuni mwake, unazifahamu ratiba zake za ziara za mwaka mzima, hata zingine unataka kumwekea mipango. Je, ni kweli wewe ni mwanamziki au?





Umeona eee Uko bize kujua simba na yanga mara mbeya city……. Hivi unataka kuwekeza kwenye soka?? Cha ajabu wewe ni mwalimu tena wa Bible knowledge halafu Uko bize na simba mara yanga. Uko kwenye biashara lakini unafatilia Lini bunge litakua live sijui unataka utangaze biashara yako bungeni . Mara Lema ataachiwa Lini, wewe ni mwanasiasa?? See hauko serious kufatilia biashara yako ya vitunguu ina Changamoto zipi, faida, lugha gani utumie kwa wateja au msimu wa soko ni Lini??





Mimi sijawahi kumuona Dewji ana comment kwenye page ya east Africa TV kuchangia Mada zisizohusiana na biashara zake. Unajua matajiri wako bize kufatilia yanayo wafanya kutajirika zaidi wewe Je?? Masikini unafatilia mambo ya kimasikini siyataji unayajua…….





Nimeshindwa kufahamu iwapo utakuwa na mafanikio katika kujua mahali anapoishi Lady Jaydee siku hizi. Wakati huo huo, vitunguu vyako viko nje katika ghalani Iringa, na viko hatarini kuharibiwa na wadudu bila wewe kujua jinsi ya kuchukua hatua ili kupata soko. Muda wako mwingi unaupoteza kwa kutumia vifurushi vya intaneti vya mega mix kutoka Tigo kufuatilia udaku wa Sudy Brown. Inashangaza kuona unajiona kama miongoni mwa waandishi wa umbea wa Shilawadu.





Utaishia kusoma story za mafanikio ya akina Mengi, Dewji, Dangote, shigongo lakini yako itakua tu HISTORIA YA MAREHEMU KWA UFUPI ulisoma darasa la kwanza hadi Saba shule ya msingi mwembengoma……
Historia inafutika hapo hapo….


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

BADILIKA: Anza kupiga hatua ya maendeleo sasa

BADILIKA: Anza kupiga hatua ya maendeleo sasa

Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza.Read More

Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida

Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida

1.💥Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2.... Read More

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadam... Read More
JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUD... Read More

Elimu ya biashara

Elimu ya biashara

Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo... Read More

Ujumbe kwa leo

Ujumbe kwa leo

Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika…Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia…Kuna HELA huwezi kuzipata... Read More

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inataki... Read More

Ilinde ndoto yako

Ilinde ndoto yako