Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

FUNZO: Maisha ni kuchagua

Featured Image

Siku hizi kuna tangazo moja la kampuni ya simu za mikononi, Tigo, likimuonesha mama akiwa _busy_ na pembeni yupo mwanae mdogo apo akijisemesha na akatamka maneno ambapo mama akaona ni kama ameanza kuongea. Kwa furaha anampigia simu mumewe akimtaka amsikilize mwanae akiongea. Hapo mama anamtaka mwanae aseme "mama" na baba naye anavutia kwake akimtaka aseme "baba". Kwa maajabu kabisa mtoto anawapotezea wote na kutamka "ni Tigo peesa". Wazazi wakashikwa na butwaa lakini huku wakitabasamu.

Ukiitazama vizuri kazi ya ubunifu iliyotumika katika tangazo hili unaweza kupata funzo, pamoja na mengine, kwamba mtoto alikua na chaguzi lake ambalo ni tofauti na yale ambayo wazazi walikua wamempa. Lakini zaidi, pamoja na kuwa amekuwa na chaguzi lake binafsi, pasipo kufuata alichoagizwa na baba au mama, bado wazazi wanatabasamu kwani wanaona mwanao kafanya jambo jema.

👉Unaona unavyofanya kazi bila furaha kwa kua ulifanya chaguo la kazi hiyo kwa kusikiliza ndugu au marafiki.

👉Unaona unavyo _struggle_ katika biashara kwani halikua chaguo lako bali ni la ndugu au marafiki

👉Unakumbuka ulivyoshindwa kusomea kile unachopenda kwa kusikiliza ndugu au marafiki
9
👉Unakumbuka ulivyoshindwa kuishi na yule mwenzi uliyempenda na mkapendana naye kwa kusikiliza ndugu na marafiki

Unaweza kushauriwa, na ushauri ukawa ni mzuri kabisaa na ukaona ni vyema uufuate kwa kua hata wewe umeambiwa na ukachanganya na akili yako ukaona inafaa.

Jana nilitoa semina kwa wanafunzi wote wa Shule ya Sekondari Chang'ombe, pamoja na mambo mengine nikawataka kupima sana marafiki walio nao na kuona kama ni washauri wazuri na kama sivyo waachane nao na kuwa na marafiki wapya wenye mawazo chanya ya kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Kuna hii daladala imeandikwa nyuma *_Marafiki wengi mjini hasara_*. 😃. Mie nakuambia sio marafiki tu, hata ndugu pia. Kikubwa ni kuwapima wale ulio nao karibu na kuona kama bado ni wa msaada kwako. Wapime na chukua hatua. Kumbuka Mheshimiwa JK aliwahi kutuasa " _Akili za kuambiwa, changanya na za kwako_ ".

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Hii ndio inaitwa mbinu ya biashara

Hii ndio inaitwa mbinu ya biashara

Anakuja Mchina anasema anahitaji Paka🐈,
ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi
wan... Read More

Kukosa hela sio tatizo bali ndio kigezo ya kutafuta hela

Kukosa hela sio tatizo bali ndio kigezo ya kutafuta hela

Ukimonyesha mtu fursa akakwambia hana hela mwambie hiyo ndio sababu ... Read More

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hu... Read More

Njia 8 za kupata mtaji kwa ajili ya Biashara yako

Njia 8 za kupata mtaji kwa ajili ya Biashara yako

Njia hizo ni kama ifuatayo!!

✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni ... Read More

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

KWAHERI MWAKA JANA. UMENIFUNZA MENGI.

Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuin... Read More

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadam... Read More
Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inataki... Read More