Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kwa nini vijana wanakatazwa kujamiiana?

Featured Image

Ujana ni kipindi cha mabadiliko kutoka utotoni kuelekea utu uzima, wakati wa kipindi hiki kijana hupata mabadiliko ya kimwili, kiakili na kimtazamo. Mwili na akili hupevuka. Ni kipindi muhimu cha kuweka msingi wa maisha ya baadaye. Vijana wanakatazwa kujamiiana kwa sababu matatizo mengi yanaweza kutokea kutokana na tendo hilo.

Kwanza kabisa kwa kujihusisha na kitendo cha kujamiiana vijana wanapoteza nguvu na muda ambao wangeweza kutumia kwa shughuli za maendeleo. Kwa mfano, kusoma, kufanya kazi, kushiriki katika shughuli za vikundi katika jamii au kucheza michezo.
Pili, matatizo ya mimba katika umri mdogo ni mengi. Mojawapo ni msichana kufukuzwa shule, au hata jamii kumtenga. Matatizo mengine ni ya kiafya kutokana na mwili wa msichana bado kuwa haujakomaa vyema.
Tatu, vijana wanakuwa bado hawajajiandaa kwa uzazi au kujitegemea. Sababu nyingine ya kuwakataza vijana kujamiiana ni ile ya hatari ya kuambukizana magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na Virusi vya UKIMWI. Magonjwa haya ni mabaya sana yanaweza kusababisha maumivu makali, ugumba au hata kifo.
Unapofikiria sababu zote hizo utaona kwamba kujamiiana katika umri mdogo kunaweza kuleta madhara mengi kwa afya yako na malengo yako maishani. Hivyo basi unapokatazwa kujamiiana ni kwa sababu ya matatizo haya. Hata hivyo, kama kwa vyovyote huwezi kuacha kujamiiana, hakikisha kwamba unajikinga wewe na mpenzi wako kwa kutumia kondomu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, ni kweli kwamba mwanamke akikaa muda mrefu akiwa bikira ni shida sana kuvunja kizinda akijamiiana kwa mara ya kwanza?

Je, ni kweli kwamba mwanamke akikaa muda mrefu akiwa bikira ni shida sana kuvunja kizinda akijamiiana kwa mara ya kwanza?

Ile ngozi ndani ya uke i inabakia kuwa nyembamba na laini sana, hata mwanamke akiwa bikira katika... Read More

Nikishatambua kwamba nina mimba, nifanye nini?

Nikishatambua kwamba nina mimba, nifanye nini?

Ukishatambua kwamba una mimba kuna mambo mbalimbali tofauti ya kufanya. Kwanza kabisa mweleze mwe... Read More

Kutahiriwa kwa wanaume ni sawa na ukeketaji?

Kutahiriwa kwa wanaume ni sawa na ukeketaji?

Hapana. Ukeketaji na kutahiriwa kwa mwanaume havifanani.
Kama kutahiriwa kwa mwanamume ni sa... Read More

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

Ndiyo, lakini ni mwanzo tu na kwa muda mfupi; hii ni kwa
sababu mwanzoni nikotini iliyomo ka... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano Mazuri ya Simu na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano Mazuri ya Simu na Msichana

Kama una nia ya kuimarisha uhusiano wako na msichana, ni muhimu kuwa na mawasiliano mazuri ya sim... Read More

Jinsi ya Kuomba Msichana Awe Rafiki Yako

Jinsi ya Kuomba Msichana Awe Rafiki Yako

Kuomba msichana awe rafiki yako si jambo rahisi kama inavyoweza kuonekana kwa wengi. Hata hivyo, ... Read More

Je, Ni Vipi Kujilinda na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende?

Je, Ni Vipi Kujilinda na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende?

Je, Ni Vipi Kujilinda na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende? 😊

Karibu, vijana wapendwa!... Read More

Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Wapo baadhi ya Albino wenye macho ya kuchezacheza na
ambayo hayawezi kulenga pamoja. Hii ina... Read More

Je, ni sahihi kuzungumza na wenzio/ marafiki juu ya uhusiano wangu wa kimapenzi?

Je, ni sahihi kuzungumza na wenzio/ marafiki juu ya uhusiano wangu wa kimapenzi?

Kama unavyohusisha rafiki zako katika mihemuko mingine, inaeleweka kama utataka kuwashirikisha ka... Read More

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hupunguza mawazo?

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hupunguza mawazo?

Bangi hupunguza mawazo kwa muda mfupi kwani huleta hisia za furaha na utulivu. Lakini hata hivyo ... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano? Swali hili ni mo... Read More

Kinga ya mwili ni nini?

Kinga ya mwili ni nini?

Kinga ya mwili ni mpangilio wa mwili kujikinga na maradhi. Chembechembe nyeupe zilizopo katika damu ... Read More