Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Featured Image

Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu
amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya
kilicho karibu mara moja. Vinginevyo ongozana na rafiki
yako kwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa kuhusu jambo
lililotokea. Polisi watampa fomu ambayo ataipeleka kwa mtoa
huduma. Ni muhimu usijioshe kwa maji kabla hujachunguzwa na
mtaalamu wa afya kwani kufanya hivyo kutaondoa ushahidi wa
kubakwa.
Kwa kuwa kupitia utaratibu huu
inakuwa vigumu mwathiriwa
anahitaji msaada wa karibu
na uangalizi. Mzazi au rafiki
anahitajiwa aongozane naye
na kumsaidia, kwa mfano
kuhakikisha kuwa katika kituo
cha polisi msichana ahojiwe na
polisi wa kike.
Mtu aliyebakwa anahitaji
kusaidiwa kihisia ili aweze
kusahau mawazo na jambo
liliomtokea. Kwa mwathirika, ni
muhimu apewe ushauri nasaha
ili aendelee kujihisi kwamba yeye bado yupo kama mtu wa
kawaida. Ni muhimu pia kuzishughulikia habari za mwathiriwa
kwa siri. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu
ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au
mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana
ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa
utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha.
Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa.
Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kujilinda na Mimba Bila Kusababisha Madhara ya Kiafya?

Jinsi ya Kujilinda na Mimba Bila Kusababisha Madhara ya Kiafya?

Jinsi ya Kujilinda na Mimba Bila Kusababisha Madhara ya Kiafya? 😊🌼

Karibu kijana! Le... Read More

Vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha vidonda vya tumbo?

Vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha vidonda vya tumbo?

Wanawake wengine wanapata vidonda vya tumbo, lakini haya hayana uhusiano na vidonge vya kuzuia mi... Read More

Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Imani hiyo si kweli kabisa. Inawezekana ni kupotoshwa kwa
makusudi wa ukweli kuhusu jambo hi... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia muda mrefu katika kujenga msisimko kabla ya kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia muda mrefu katika kujenga msisimko kabla ya kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki yangu? Leo nataka kuzungumzia suala ambalo limekuwa likiwasumbua wengi kwa mud... Read More

Nifanye nini nikipata hamu ya kujamiiana au kufanya mapenzi?

Nifanye nini nikipata hamu ya kujamiiana au kufanya mapenzi?

Unapofikia ujana unaanza kuwa na hisia za upendo na kujisikia kupata mvuto au msisimko ambao sio wa ... Read More
Mtu anaweza kurithi uvutaji wa bangi?

Mtu anaweza kurithi uvutaji wa bangi?

Hapana, huwezi ukarithi uvutaji wa bangi. Lakini mara nyingi watoto huiga tabia za wazazi wao. Wa... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kusisimua na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kusisimua na Msichana

Kama mvulana, unajua kuwa mazungumzo na msichana yako yanaweza kuwa magumu sana. Unaweza kuwa na ... Read More

Je, Ni Sahihi Kutumia Dawa za Kuzuia Mimba?

Je, Ni Sahihi Kutumia Dawa za Kuzuia Mimba?

Je, Ni Sahihi Kutumia Dawa za Kuzuia Mimba? 🌼😊

Tunaelewa kwamba vijana wetu ni kikun... Read More

Watu wanaoishi na ulemavu wanapewa huduma za upasuaji hasa wakati wa kujifungua?

Watu wanaoishi na ulemavu wanapewa huduma za upasuaji hasa wakati wa kujifungua?

Upasuaji unafanyika kwa wanawake wote ambao wamegundulika
kuwa na tatizo la kujifungua kwa n... Read More

Kwanini Albino wanakuwa na mabaka meusi kwenye ngozi zao?

Kwanini Albino wanakuwa na mabaka meusi kwenye ngozi zao?

Ngozi ya Albino haina jinsi ya kujilinda na mionzi ya jua. Inaungua
sana baada ya kupatwa na... Read More

Njia za Kudumisha Mapenzi katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kudumisha Mapenzi katika Uhusiano wako na Msichana

Mapenzi ni muhimu katika uhusiano wowote wa kimapenzi. Ni muhimu kuchukua hatua za kudumisha mape... Read More

Vidokezo vya Kuweka Uhusiano wako na Msichana Hai

Vidokezo vya Kuweka Uhusiano wako na Msichana Hai

Mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu, na kwamba uhusiano wa kimapenzi ni s... Read More